Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Sintofahamu imezuka katika uchaguzi wa viongozi wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), baada ya wajumbe kumtilia shaka mmoja wa wagombea aliyekuwa akitoa nauli.
Uchaguzi wa Bavicha unaendelea katika ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Januari 13, 2025.
Pia, Soma: Mjumbe wa mkutano mkuu BAVICHA alilia posho ya kujikimu, 'tuliambiwa tutalipwa ila hadi sasa bado, kwa hali hii tunaweza kuepuka rushwa?'
Mashaka zaidi, yametokana na mgombea huyo kudaiwa kugawa nauli hizo katika eneo la kificho, wajumbe wakiuliza ana mamlaka gani ya kutoa fedha hizo.
Hali hiyo ilizua tafrani baada ya wajumbe kutoka ukumbini kwenda alikokuwa mgombea huyo, wakihoji yeye ni nani hadi atoe nauli kwa wajumbe.
Baadaye, msimamizi msaidizi wa uchaguzi huo, Salum Mwalimu aliwataka walinzi kuwaondoa watu wote kwenye korido za ukumbi huo.
Kisha, aliwaamrisha wajumbe waingie ndani kusikiliza sera za wagombea wa ujumbe wa baraza kuu waliokuwa wanajinadi.
Soma: Kinachoendelea katika Uchaguzi BAVICHA Taifa