MREJESHO: KIMO CHA MIMBA KUWA TOFAUTI NA UMRI WA MIMBA .
Ndugu zangu, wiki kadhaa zilizopita nilileta Uzi huu, kiukweli nawashukuru sana maana asilimia kubwa nilifuata ushauri wenu na hatimaye Jana mke wangu aliumwa uchungu nikamuwahisha hospitali na hatimaye Leo mida ya saa mbili asubuhi kajifungua mtoto wa kike bila shida yoyote.
Maajabu ninayoweza kuyaona katika uzazi wa mke wangu, yeye alizaliwa tar 03, mtoto wetu wa kwanza pia alizaliwa tar 03 na huyu pia kazaliwa tar 03 japo miezi tofauti.
Ndugu zangu nawashukuru tena na tena kwa ushauri mzuri.
Naomba tusaidiane sasa kumchagulia jina linaloanza na herufi B maana mtoto wangu wa kwanza anaitwa Beatrice natamani sana majina yao yaendane.
Mungu awabariki nasubilia comments za majina.