Linasafiri kutoka wapi mpaka lipite karibu na jua?.
Kwa hiyo kama halitapita karibu na jua halitaunguzwa na kuyeyuka?.
Natanguliza shukrani.
Kaka nisome kwa makini sana nitajaribu kuelezea kwa kutumia kiswahili japo nitachanganya na maneno ya kingereza kwani hata kama hivi vimondo vina majina ya kiswahili yatatuchanganya.....
Kwenye SPACE kuna nyota nyingi sana na zile sayari zinazojulikana, nyota zipo kubwa na ndogo na kuna nyota kubwa kuliko hata ukubwa wa hii dunia. Baadhi yake zimeundwa kwa mawe, namaanisha sakafu ya hizi nyota ni mawe na baadhi yake hizi nyota na sayari zina volcanic activity ambazo zipo active au zilishawahi kuwa active.
Kuna kitu kinaitwa METEOROID hili ni jiwe dogo linalosafiri kwenye Space, space ni nje ya dunia huko kwenye nyota na sayari zinapoelea,
Kuna mawe mengine yanaitwa asteroids, ni kitu kile kila kama meteoroid ila asteroid ni kubwa kidogo zaidi ya meteoroid, kuna jamii nyingine inaitwa comets.."icy dirty ball" hii comets ina mchanganyiko wa mawe,water ice na mchanganyiko wa baadhi ya gesi kama methane cabondioxide,monoxide.
Kaka sasa hii comet wakati inasafiri ikipita pembeni ya jua zile gesi zinayeyusha na ukali wa joto la jua na linatengeneza kitu kama tail. Unaweza ukaona nyota imepita kwa speed na mkia mrefu ...
Turudi kwenye Meteoroid, yenyewe nayo inasafiri kwa speed kali sana inaweza ikazidi 72,000km/h. Sasa kuna kitu hapa kinaitwa aerodynamic heating-is heating of an object produced by its high-speed passage through air, yani speed yake kali tu inakisababisha kipate moto kiungue na wewe unaona kama moto umepita angani fasta.
. Kaka nadhani umenipata kidogo .
Nisiendelee sana sitaki nikuchanganye.
Hayo mengine ni kudanganyana tu ila hii ndio concept.