Kimondo ni kitu gani?


hio ni natural jet fighter ambayo haina rubani na man made ndo kama zile za mmarekani
 
Nimeona mchango wako hapo juu Asante, but wana Jf sikuhizi ni mizaha tu kila jambo kama wapo MMU au Chit chat vile

Buk7 wamelichafua jamvi. Hata kwenye mada elimishi wao huweka ushindani na mizaha.

Watawala hawana budi kulirejesha mahala pake.
 

Asante kwa kunipunguzia ujinga
 
Asante kwa kunipunguzia ujinga

Pamoja mkuu, nlivyoona hakuna mtu anayeuliza zaidi au kudadisi zaidi nikajua sijaeleweka, ujue hata darasani ukiona huulizwi swali ujue hujaeleweka au unaboa wanafunzi wako.
Waau ulizeni maswali wakuu tuelimishane zaidi
 
Mkuu hujalazamishwa kuamini ila huo ndo ukweli kwa mujibu wa vitabu vitakatifu hata nchi na nchi nyengine kuna mipaka sembuse ufalme wa mbingu
Lete uthibitisho ktk maandiko kwamba hiyo mipaka inalindwa na vimondo.
 
Duh, sasa Mkuu haya mawe chanzo chake ni kutoka sehemu gani?
 
Kimondo au kwa lugha ya wenzetu wanakiita shooting star. Ni mawe makubwa ambayo mara chache hupita kwenye uso wa dunia kwa kasi sana na kuacha miale ya mwanga kama moto kwa mvutano unatokea baina ya nguvu ya dunia na chenyewe.

Acha kupotosha jamii wewe
 

Napingana na wewe 100% vimondo/commets ni vinazunguka tu angani kutokana na some reactions and forces taking place there
 
Vimondo(meteori au meteroidi) ni magimba ya angani yanayozunguka jua ama sayari katika njia yake inayoitwa obiti(orbit). vimondo huzunguka jua ama sayari kwa spidi tofauti na inakadiriwa kimondo chenye mwendokasi mkubwa kuliko vyote ni kile chenye mwendo kasi wa 42 kilometa kwa sekunde.kuna aina tatu(3) za vimondo ambavyo ni;1.kimondo cha mawe kilichoundwa kwa mawe. 2.kimondo cha chuma kilichoundwa kwa madini ya chuma. 3.na kimondo cha mchanganyiko wa madini ya chuma na mawe.Kinachosababisha vimondo vishuke duniani ni muingiliano wa mzunguko wa kimondo karibu na dunia yetu hivyo kutokana na udogo wake huvutwa kwa nguvu kuelekea uso wa dunia na kutokana na spidi kubwa vinayotembea 20,000m/s vimondo vya mawe vyenye size ndogo husuguana na hewa kwa nguvu na hivyo huungua, kuwaka na hatimaye kwisha kabisa kabla havijafika ardhini,lakini vimondo vya chuma vyenyewe huvumilia joto la msuguano wa hewa hivyo huungua surface yake ya nje na kiasi kikubwa ubaki na kufanikiwa kudondoka kwenye uso wa dunia.
 
Duh, sasa Mkuu haya mawe chanzo chake ni kutoka sehemu gani?
Mengi yanatokana na dusts ya hizi sayari na star na mengine ni mawe yanayomeguka kutokana na nguvu za uvutano kwenye hizi sayari, mwezi na nyota
 
Well said brother.
 
Saizi ya vimondo hotofautiana na kidogo kabisa hukadiriwa kuwa ni saizi ya mchanga na haviwezi kuvuka ukubwa wa asteroids.Inakadiriwa karibu vimondo 100 vidogo vyenye uzito wa kilo kati ya (10-30)Kg hudondoka duniani na kufika ardhini kila mwaka. Mpaka sasa duniani kuna vimondo kumi tu ambavyo ni vikubwa kabisa kuwahi kudondoka na kikubwa kabisa kikiwa nchini Namibia katika kijiji cha otavi,kimondo hiki kina zaidi ya asilimia 90 madini ya chuma na elementi kama vile nikeli fosforasi na salfa ya jumla ya uzito wake wote.wakati kinadondoka kwa mara ya kwanza uzito wake ulikadiriwa kuwa tani 100 (100,000kilogramu) lakini kutokana na madini ya chuma kushika kutu na kulika,kwa sasa kinakadiriwa kuwa na uzito wa tani 60(60000Kg).Kimondo chetu watanzania kilichopo mbozi mkoani Mbeya ni cha sita(6) kwa ukubwa kati ya vile kumi kikiwa na uzito wa tani 12(12,000)Kg,urefu wa mita 3, upana wa mita 1.6 na kimo cha mita 1.22 kikiwa na madini ya chuma kwa 90.45%, 8.69%nikeli, 0.01%sulfa na 0.11%fosforasi.
 

well explained.
 
Vitabu gani? Waandishi wengi walikuwa wanabuni.
Bila ukweli wowote.
Ila ukitaka kuamini jiwe au kuabudi jua unadhani tutakukataza?

Mkuu imani ya dini kwako imekaa kushoto na mm imani ya wana science vilevile imekaa kushoto maana wanascience walishahi kuja na mada zao binaadamu alikuwa sokwe, washawahi kukisia mwisho wa dunia na mpaka leo dunia ipo na mashuleni tunamezeshwa mtu alikuwa sokwe so tusijaze uzi hata nikwambia vitabu gani still hautoamini mkuu over!!
 

Sawa kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…