Kimpa Vita, Muafrika aliyeuawa na wamisionari kwa kuwahubiria watu kuhusu imani ya kijadi ya Congo

Kimpa Vita, Muafrika aliyeuawa na wamisionari kwa kuwahubiria watu kuhusu imani ya kijadi ya Congo

kwisha

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2021
Posts
1,779
Reaction score
4,982
Mnamo tarehe 7/2/1706, Kimpa Vita aliuawa kwa kuchomwa moto na mishenari wa kikatoliki huko nchini Congo.

Kimpa vita aliuliwa kwa sababu tu ya kuwahubiria watu kuhusu imani ya kijadi ya Kongo na kuwashawishi wakongo kurejea katika imani na mila. Mwana mama huyu, pia aliwataka wakongo wa jamii ya Mbanza kurejea katika aridhi yao baada ya kuikimbia kwa muda mrefu kufuatia kuanguka kwa utawala wa VITA -A- NKANGA katika Vita maarufu ya Mbwila (Ambuila 1665).

Kimpa Vita aliuliwa kwa sababu alikuwa akiwashawishi wakongo kuachana na dini ya kikristo (katoliki) na kuwataka kurejea katika imani zao.

Alipokuwa mdogo, Kimpa Vita alibatizwa kwa jina la Ana Beatriz, lakini punde alipoanza harakati zake za kuwarejesha wenzie Katika imani ya nyumbani kwao, alilikataa jina hilo la kikristo na kubeba jina lake la asili la Kimpa Vita au kimpa Nkya Nvita maana yake 'Mbinu mpya za mapambano' huku akiwa amejikita katika mapambano ya kiimani/kiroho.

Kimpa Vita alichomwa moto na mishenari wa kikatoliki yeye pamoja na mwanaye akiwa amembeba mgongoni.

1668609633751.png

1668609665542.png
 
Ujue Ukristu ni "uzungu" yeye alikataa uzungu. Waliojifanya waeneza neno la Mungu ndio waliomuuwa. Hata sasa hivi ukijitokeza kupinga ukristu watakushangaa kwani ukristu upo kwenye damu za Waafrika. Walishafanikiwa kuteka mawazo ya Waafrika kiasi kwamba mila za jadi zimesahauliwa. Angalia ukame unatutesa na tunashindwa kuomba kwa kutumia Mila zetu kisa Ukristu!! You Africans, come out from the cave!! Remember the allegory of the cave (Plato).
 
  • Thanks
Reactions: ibn
Back
Top Bottom