Philipo Mwakibinga
Senior Member
- May 13, 2013
- 110
- 175
TATIZO NI MDEE AU NI KUTOTII DEMOKRASIA?
Na. Philipo Mwakibinga
0758910403
Kwa muda sasa nimekua nikifuatilia minyukano inayoendelea ndani na nje ya Bunge kuhusu Wabunge 19 wa Viti maalumu wanaokataliwa na CHADEMA. Lakini kwa upande wangu naliona suala hili kwanamna hii;
CHADEMA wanapaswa kubeba Lawama katika hili. Hii ni kwasababu wanapambana kutaka kulifanya suala la kisheria kuwa la kawaida na lenyekupiganiwa kwa makelele kitu ambacho si sahihi.
CHADEMA wanajua kuwa walisusia matokeo na kutokuutambua uchaguzi wa Mwaka 2020 Octo, lakini cha ajabu wakajiingiza kwenye mchakato wa kuchambua majina ya viti maalumu. Huu ni uhuni kama Uhuni mwingine tu. Kama kusingekua na mchakato wowote unaohusu Viti maalumu ndani ya CHADEMA hasa kutokana na kutoutambua uchaguzi ule basi hii ya akina Nusrat 19 Isingetokea leo.
BAWACHA KUCHEZA NGOMA YA KIJINGA. Ukiwasikia Wanawake wa CHADEMA utagundua wanatumiwa bila wao kujijua na kujikuta wanakua vituko katika uwanja wa siasa hizi za mageuzi. Kwasababu hawa akina Bulaya 19 walishakata rufaa kwenye chama ili wajadiliwe na wakapate nafasi ya kusikilizewa, bali kwakua akina Mbowe na Mnyika wanajua Usanii walioufanya hawako tayari kuita Baraza Kuu la Chama wakijua kabisa wataumbuka.
Hali hii imesababisha kuwatumia BAWACHA kushambulia wenzao huku wakijua kabisa haki za Wanawake ndani ya CHADEMA zinayumbishwa na Wanaume wachache wasio kitakia mema CHADEMA kwa muda mrefu sana. Kwa mfano JOHN MREMA siyo MwanaCHADEMA halisi na wala hajawahi kuwa MwanaCHADEMA halisi bali ni MERCHANT ndani ya CHADEMA lakini, ndiye hupiga kelele na kuwaaminisha akina MBOWE kuwa mtu sahihi wakati anawazunguka wenzie.
Unapokuwa na chama cha Siasa ambacho kinawafukuza, kuwapoteza na kuwapuuza watu kama Dr Slaa, Silinde, Lwakatale, Komu, Selasini, na Kuwabeza watu kama Lowassa, Nyarandu, na Sumaye kwa kuwataja wachache halafu kinajivunia kusonga Mbele kwa Kubakia na HILDA NEWTON[emoji23][emoji23] ujue si chama tena bali ni kikundi cha uchuro.
Najua MDEE anayomengi na anajua mengi. Mnyika na Mbowe wanajua hilo. Wanajua wakiita Baraza Kuu hali itakua chafu zaidi ya hii na wenda ukawa ndiyo Mwisho wa wao kuaminiwa. Kwahiyo wanatafuta huruma ya makundi mbalimbali ili kuhitimisha salama suala la akina Matiko 19 wakati wanajua kabisa hakuna namna zaidi ya kuita BARAZA KUU LA CHADEMA. Hii inanikumbusha yale ya Maalimu (Mungu amlaze pema) na Lipumba Ibrahimu, pale ambapo team Maalim Walitumia hisia kushindwa dhidi ya Team Lipumba waliotumia katiba, miongozo na sheria za CUF kushinda.
Mbowe na BAWACHA acheni kuchafua wenzenu hawa akina Kishoa 19 kule bungeni ni matokeo ya ubabaishaji wenu. Ile tabia ya kujifanya mnagomea matokeo halafu usiku mnaandika vimemo sasa imewapa nguvu akina Mwaifunga 19 kuwalaza mdomo wazi.
KIMYA CHA MDEE NI HATARI KULIKO KELELE ZA SUZANI KIWANGA NA JOHN MREMA.
Asante.