Kina mama wajane acheni tamaa ya kukodisha hati za nyumba zenu ili zikopewe kwa ujira mdogo

kimarabucha

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
791
Reaction score
621
Leo katika taarifa ya habari ya saa 1 kupitia kituo cha Channel 10 kuna mama mjane alihojiwa na kituo hicho akilalamika nyumba yake kuuzwa na Benki na mnunuzi kuibomoa na kusababisha yule mama kulala nje kwa miezi 5.

Kutokana na hali hiyo Afisa Mtendaji wa mtaa amesema kuwa ni kweli nyumba hiyo iliyopo Mbezi imeuzwa na kutokana na mama kushindwa kulipa deni.

Akifafanua Afisa huyo amesema mjane huyo amekuwa na tabia ya kukodisha hati hiyo kwa mtu mmoja ambaye mara ya kwanza alirejesha mkopo huo lakini mara ya pili ameshindwa kurejesha na kusababisha nyumba hiyo kuuzwa.

Nawashauri hawa wajane waache tamaa ya kukodisha hati kwa kupewa fedha kidogo matokeo yake ndio kama yaliyompata huyo mjane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…