Kuhesabiwa ni sehemu ya wajibu wa raia kisheria. Maana sense husaidia serikali kupanga mipango ya jinsi ya kuwahudumia watu wake ingawa kwa serikali yetu sensa yaweza kuwa dili la kuibia pesa ya wafadhili. Maana serikali yetu huwa haihudumii watu wake na badala yake ni kinyume.
Wananchi wanaibeba serikali kwenye kila upuuzi kuanzia ufisadi na safari zenye hasara za rais wetu. Hivyo, wanaopinga sensa kisheria wanavunja sheria hata kama serikali yenyewe ni ya hovyo. Ponda na wenzake wanatumia dini kujinufaisha kisiasa. Hawana sababu za msingi za kupinga sensa zaidi ya kutafuta umaarufu na ujinga wa kawaida.
Kingine kinchowapa kichwa akina Ponda ni ulegelege na uchafu wa serikali isiyo na maadili wala mipango madhubuti.