Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Muda huu tarehe 10 Machi 2023, ninamuona Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makala akiongoza shughuli ya kumpongeza mama Samia kutimiza miaka 2 ya uongozi wake madarakani.
Kumpongeza Rais kwa kutimiza miaka miwili madarakani ni jambo la kumpongeza lakini ni muhimu sana kuzingatia usahihi wa namna ya kupongeza. Shughuli inayofanyika Diamond Jubilee imetumia bajeti ambayo sidhani kama ipo kwenye votes za bajeti iliyopitishwa na Bunge.
Kuna tatizo linalohusu madawati, ubovu wa barabara, tatizo la maji jijini na mambo mengine. Lakini nilidhani pesa hizi zinazotumika kufanya sherehe za kumpongeza mama zingemheshimisha sana endapo mkuu wa Mkoa na wasaidizi wake wangeelekeza nguvu kutatua baadhi ya kero kupitia hela hizo na badala yake zinatumika kufanya sherehe.
kwa namna ninavyofahamu viongozi wengi wa Dar, lazima hapo uchotaji wa fedha za umma kwa kigezo cha shughuli ya kumpongeza mama.
Tungempongeza mama kwa kufanyakazi za kujitolea, kukagua miradi ya serikali na kufanya mikutano ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Nakupongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka 2 madarakani na tunaamini safari inaendelea lakini wasaidizi wako wanaonekana kupwaya na hawakusaidii bali wanafanya uzidi kuwa mbali na wananchi wako.