Kinachoendelea kwenye 'Management' ya Simba sc ni Pata potea.

Kinachoendelea kwenye 'Management' ya Simba sc ni Pata potea.

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Baada ya kuona mwenendo wa timu yao siyo wa kuridhisha, Mashabiki na wanachama kindakindaki walipaza sauti wakishinikiza kujiuzulu kwa baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa timu yao.

Kweli baada ya siku kadhaa viongozi hao walitangaza kujiuzulu, lakini cha ajabu Mdhamini na Rais wa heshima wa timu hiyo akatangaza kuwarejesha viongozi hao, Tatizo lililopo ni endapo timu haitafanya vizuri, ikitokea timu ikafanya vibaya basi anaepaswa kuwa 'Answerable' ni Mo mwenyewe.

Tuendelee kuwa na subira, Muda utaongea.
 
Mo ameingia kwenye mtego ambao utamuadhibu vibaya sana. Hii movie ni marudio ya kesi ya Yanga asili na Yanga kampuni. Mangungu lazima ashinde vita hii.
 
Back
Top Bottom