Rashda Zunde
JF-Expert Member
- May 28, 2022
- 204
- 231
Kuondoka kwa hiari wafugaji wa jamii ya Kimasai kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ni faida kubwa zaidi ya hasara kwa usalama wa mazingira yetu ambayo kila kukicha yanakosa uendelevu.
Watanzania tuna kila sababu ya kulitunza eneo hilo kwa faida ya kizazi cha sasa na cha baadae kwani thamani yake ilionekana baada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kulitangaza kuwa urithi wa dunia mwaka 1979 kutokana na utajiri wake wa utamaduni na mambo ya asili uliosheheni mahali hapo.
Binadamu tunaendelea kuongezeka kila siku huku vitu vingine kama ardhi ikiwa vilevile, misitu tunafyeka kila siku huku upandaji miti ukiwa mdogo, viumbe hai tunawatumia kwa faida zetu hali inayoleta mabadiliko ya tabianchi duniani.
Mojawapo ya changamoto inayosababisha mabadiliko ya tabianchi yenye kuleta wasiwasi kwa mwanadamu ni misitu mingi duniani kutoweka kutokana na ongezekp la watu, maendeleo ya viwanda, kilimo na kupanuka kwa makazi ya watu ambapo kwa sasa idadi ya watu ikiwa ni zaidi ya bilioni saba.
Yanayofanywa na serikali kuwajengea makazi mapya huko Msomera wilayani Handeni mkoani Tanga wananchi wanaohama Ngorongoro ambazo sasa ni zaodo ya kaya takribani 100 ni la kupongezwa na uwekaji wa mipaka Loliondo ni kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo.