DOKEZO Kinachofanywa na Vyama vya Ushirika Kusini kwa wakulima wa Korosho ni dhulma, wizi na utapeli

DOKEZO Kinachofanywa na Vyama vya Ushirika Kusini kwa wakulima wa Korosho ni dhulma, wizi na utapeli

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Tunaomba wahusika wafuatilie kuhusu vitendo vinavyofanywa na hawa watu wa ushirika kwenye malipo ya korosho huku Mtwara na Lindi. Umefanyika mnada wa kwanza wa korosho wiki 4 zilizopita na bei ilikuwa tsh 4170@kg 1 ya korosho, cha kushangaza ukifuatilia malipo unakuta bei zinazolipwa siyo zile zilizotangazwa siku ya mnada badala ya kulipwa 4170/ unakuta umeingizwa kwenye mnada wa pili ambao bei ilikuwa tsh 3780/=

Ukiuliza kwanini nalipwa hivyo majibu yake unaambiwa mzigo wako haukuwahi kwenye mnada wa kwanza wakati/kinachofanyika mnada wa kwanza pesa zikishalipwa na makampuni yalishinda mnada wao wanasubiri mnada wa pili bei kama itashuka ndipo wao wanatumia nafasi hiyo kulipa watu wa mnada wa kwanza wanaingizwa kwenye mnada wa pili ambao bei ipo chini

Tunaomba wahusika walifanyie kazi hili jambo
 
Mimi nimeliona hili nikajithibitishia kuwa hili zao la korosho ni zao la Kiki tu hamna kitu hapa

Imagine watu wa mnada wa kwanza mpaka Leo hawajalipwa

Korosho za zilizokatika vyama vya ushirika mpaka Leo nyingine hazijaenda kwenye ghala wanadai gari hazitoshi mzigo upo ndani wame hold

Hapa kinachokuja kutokea mtu umenunua korosho elfu 2 kwa kilo unakuja kuuza mnada wa tano ambao ni 1900 .mwisho wa siku unakuja kuona kama hili zao halina uhakika kumbe kuna watu wajinga ndio wanaongoza vyama kimazoea mno

Watu hawajui àbc zabiashara na wajinga ndio wamejaza humo


Wale wanajua wanachokifanya ndio hao wanashisha bei ili na wao wapate chichote kitu.

Wamekuwa watu wa kati.


Korosho ni zao la kishenzi ambalo lina vurugu nyingi sana sokoni


Japo wengi wanatokea humo kwenye korosho na wamekuwa matajiri
 
Back
Top Bottom