Kinachoikuta Congo DR tuna jambo la kujifunza

Kinachoikuta Congo DR tuna jambo la kujifunza

Lotus 123

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
3,151
Reaction score
5,513
Tumeona jinsi ambavyo DRC anahangaika na waasi kwenye eneo lake la mashariki.

Je, sisi kama taifa tuna mikakati Gani ya kulinda maeneo yetu ya magharibi Kwa matukio kama haya? Au tunajiaminisha kuwa tupo salama muda wote?
 
Yale mawese na dagaa kule Kigoma au senene Bukoba haviwezi kuleta shida kwetu. Shida ya Congo inaeleweka inatokana na nini.
 
Yale mawese na dagaa kule Kigoma au senene Bukoba haviwezi kuleta shida kwetu. Shida ya Congo inaeleweka inatokana na nini.
Kikichopo mashariki ya Congo kimsingi ndicho hichohicho kilichopo magharibi ya Tz, kabla ya kutokea kwa bonde la ufa ambamo ziwa Tanganyika limo hivi sasa ardhi ya mikoa ya kigoma na Katavi ilikuwa ni ardhi iliyoungana na ardhi ya mashariki ya DR congo na ndio maana sokwe waliopo Gombe na Mahale (kigoma) ni familia moja na sokwe waliopo Congo (wanazo genes za uhusiano) kilichosababisha watengane ni kujaa kwa maji katika ufa na kufanya ziwa Tanganyika maelfu ya miaka iliyopita, hii maana yake ni kwamba madini yanayopatikana mashariki ya Congo pia yanaweza kupatikana katika mikoa ya Kigoma na katavi ni exploration tu ndio haijafanywa kabisa.

Ninachotaka kusema ni kwamba kwa muda huu ni migebuka na dagaa lakini baadaye inaweza kuwa ni dhahabu, coltan, shaba nk ambazo hizo ni bidhaa zinazomezewa mate na mataifa makubwa ambayo ndio kimsingi hufadhili vita vya huko Mashariki ya congo kupitia mawakala wao wa siri ambao wengine hata inasemwa ni viongozi wakuu wa kisiasa wa nchi fulani.
 
Back
Top Bottom