Kinachoikuta Yanga leo kuikuta pia Simba

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Maandiko matakatifu yameandika kwamba " AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " , Vilabu vya Simba na Yanga vina utitiri wa wanachama ambao pamoja na wingi wao tena wakiwa na akili timamu , WAMEAMUA BILA AIBU KUWATEGEMEA BINADAMU WENZAO KUWAENDESHEA TIMU ZAO .

Naandika haya nikiwa na ushahidi wa namna matatizo ya kisiasa ya Yusuph Manji , binadamu pekee aliyekuwa mlipaji wa bili zote za Yanga yalivyochangia njaa kwenye timu kongwe kabisa nchini , kiasi cha kuwa kama MAHARAGE YA MBEYA , MAJI MARA MOJA , Watu wanajipigia tu watakavyo !

Ni aibu kubwa sana kwa uongozi wa Yanga kumtegemea Manji kulipa hadi mishahara ya viongozi wake .

Ukweli ambao watu wengi wanaujua lakini wanaunyamazia ni kwamba timu za Simba na Yanga hazina mipango yoyote ya Maendeleo wala hazina vyanzo vyovyote vya kupata hela na zinadaiwa kila kona ya nchi , vihela vyote vya milangoni vinaliwa na wajinga wachache sana wanaojifanya wana akili kupita kiasi .

Hata hii Simba yetu akiondoka Mohamed Dewji tu , wachezaji watakunywa chai kavu , au Mmesahau chapati za Kaduguda ?

......Itaendelea .....
 
Uko sahihi bro, ingawa ukweli mchungu. La kama kusingetokea kidudu mtu wachumia tumbo akiba akilimali na kundi lake kupiga kelele hadi kuzuia ule ukodoshaji wa Yanga. Huenda njaa na tabu iliyoko sasa isingekuwa hivi ilivyo. Leo hii yangu iko Hoi haonekani akilimali wala akili hasara.....??
 
Maandiko matakatifu yameandika kwamba " AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " , Vilabu vya Simba na Yanga vina utitiri wa wanachama ambao pamoja na wingi wao tena wakiwa na akili timamu , WAMEAMUA BILA AIBU KUWATEGEMEA BINADAMU WENZAO KUWAENDESHEA TIMU ZAO .

Naandika haya nikiwa na ushahidi wa namna matatizo ya kisiasa ya Yusuph Manji , binadamu pekee aliyekuwa mlipaji wa bili zote za Yanga yalivyochangia njaa kwenye timu kongwe kabisa nchini , kiasi cha kuwa kama MAHARAGE YA MBEYA , MAJI MARA MOJA , Watu wanajipigia tu watakavyo !

Ni aibu kubwa sana kwa uongozi wa Yanga kumtegemea Manji kulipa hadi mishahara ya viongozi wake .

Ukweli ambao watu wengi wanaujua lakini wanaunyamazia ni kwamba timu za Simba na Yanga hazina mipango yoyote ya Maendeleo wala hazina vyanzo vyovyote vya kupata hela na zinadaiwa kila kona ya nchi , vihela vyote vya milangoni vinaliwa na wajinga wachache sana wanaojifanya wana akili kupita kiasi .

Hata hii Simba yetu akiondoka Mohamed Dewji tu , wachezaji watakunywa chai kavu , au Mmesahau chapati za Kaduguda ?

......Itaendelea .....
Yanga bila manji simba bila mo basi Yanga nimasikini zaidi kuliko simba angalia misimu ilipita utaona simba hawakulialia kama wanavyoaibika vyura
 
Afu miaka yte simba hachukui mataji alikua hana mtu mwenye kutoa pesa ila hakua kma yanga walivo sasa, yan utadhan manji aliondoka mwaka 2011, pia simba haiwez kurud huko kma timu mo itakua yake ndio tofaut
 
Nilidhani unamaanisha kuwa hata Simba itakuja kufungwa mechi tatu mfululizo katika ligi Kuu, au itakuja kucheza dakika 90 bila kupata kona hata moja
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji13]
 
Sasa kawaambie wachezaji wa simba wagome kucheza mechi 2 zilizobaki kwa sababu simba itakuja kuwa kama yanga!!!
 
Nilidhani unamaanisha kuwa hata Simba itakuja kufungwa mechi tatu mfululizo katika ligi Kuu, au itakuja kucheza dakika 90 bila kupata kona hata moja
Hivi ni mechi tatu au nne? USM Algiers nayo ni timu, msiisahau.
 
Back
Top Bottom