Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Maandiko matakatifu yameandika kwamba " AMELAANIWA MTU YULE AMTEGEMEAYE MWANADAMU " , Vilabu vya Simba na Yanga vina utitiri wa wanachama ambao pamoja na wingi wao tena wakiwa na akili timamu , WAMEAMUA BILA AIBU KUWATEGEMEA BINADAMU WENZAO KUWAENDESHEA TIMU ZAO .
Naandika haya nikiwa na ushahidi wa namna matatizo ya kisiasa ya Yusuph Manji , binadamu pekee aliyekuwa mlipaji wa bili zote za Yanga yalivyochangia njaa kwenye timu kongwe kabisa nchini , kiasi cha kuwa kama MAHARAGE YA MBEYA , MAJI MARA MOJA , Watu wanajipigia tu watakavyo !
Ni aibu kubwa sana kwa uongozi wa Yanga kumtegemea Manji kulipa hadi mishahara ya viongozi wake .
Ukweli ambao watu wengi wanaujua lakini wanaunyamazia ni kwamba timu za Simba na Yanga hazina mipango yoyote ya Maendeleo wala hazina vyanzo vyovyote vya kupata hela na zinadaiwa kila kona ya nchi , vihela vyote vya milangoni vinaliwa na wajinga wachache sana wanaojifanya wana akili kupita kiasi .
Hata hii Simba yetu akiondoka Mohamed Dewji tu , wachezaji watakunywa chai kavu , au Mmesahau chapati za Kaduguda ?
......Itaendelea .....