Komeo Lachuma
JF-Expert Member
- Oct 31, 2014
- 7,926
- 17,030
Chama ni mchezaji mzuri sana wala nisiwe mnafiq.... Ni bonge la mchezaji yaani huyu bwana kama unataka kujifunza kucheza mpira si vizuri kumwangalia. Anaweza kukudanganya ukaona mpira ni mchezo rahisi sana. Ukaamini hata wewe unaweza enda cheza kama anavyocheza.
Chama si mchezaji wa kumwamini anapokuwa na mpira ni mwongo sana... Anaweza kukudanganya kuwa anapiga ukaamini anapiga kumbe hapigi. Halaafu anaweza kukuaminisha kuwa hapigi kisha anapiga. Namchukia kwa sababu hiyo ya uongo. Si mkweli anapokuwa uwanjani. Binafsi huwa siwezi unafiq.
Napenda niseme nililo nalo moyoni. Kama ambavyo niliwahi sema sikuwahi mpenda manara akiwa simba siwezi mpenda sasa akiwa kwetu yanga. Siwezi...Kwa nini niwe mnafiq? Mi siwezi.Huyu ni uchafu ambao watu wametoa chooni sisi tumechukua kuja kuleta sebuleni. Anyway siyo issue.
Jambo moja ambalo silipendi kwa chama. Sipendi chama kuchezea simba. Hili nalisema tu kwa uwazi huyu angekuwa yanga angekuwa mbali sana. Tungempamba na kumpambanua.
Angekuwa ndiye wimbo wa taifa kwenye vyombo vya habari n.K ila naona simba kama hawampi hadhi yake anayostahili. Nachukia hapo tu. Natamani sana angekuwa jangwani. Chama, chama, chama babaaaaaa... Chama. Huyu jamaa huyu.
Jana niliona mambo aliyoyafanya itoshe kusema ni bonge la mchezaji... Kiukweli jamaa ana vitu vingi mguuni anakosa tu nguvu na kasi. Ila akili anayo sana. Jamaa anatumia akili kucheza mpira na anafanya mpira uonekane ni kitu rahisi sana. Ila nachojiuliza kwa nini aendelee kuchezea simba?
Angekuja kuungana nasi jangwani akutane na mzee wa kutupia magoli Mayeleee Kitu. Mwaka huu tunaanza kuwaliza watu kuanzia tarehe 13/08. Kilio kinaanzia hapo.... Watu watalia sana.. Watalia na kuendelea kulia mpaka mwisho wa msimu.