Pre GE2025 Kinachokwenda kuinyonga CCM 2024/2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
1. Viongozi waliopo madarakani kujilimbikizia mali na kutumia mali za umma kwa ANASA.

2. Viongozi waliopo madarakani kutosikiliza na kuzifanyia kazi shida za wananchi(kuwachukulia wananchi kama WAJINGA)

3. Viongozi waliopo madarakani kuwalinda MAFISADI na MAJIZI na kuwakandamiza wanaowafichua hao MAJIZI na MAFISADI(Rejea kesi ya MPINA Vs BASHE na SPIKA)

4. Ugawaji wa RASILIMALI za Taifa kwa wageni.

5. Tozo na kodi za ovyo wanazobebeshwa wananchi kila uchao.

6. Wabunge na watumishi waandamizi wa serikali kujiongezea mishahara na marupurupu bila kujali shida za wananchi.

7. Serikali kushindwa kuboresha huduma za jamii(Elimu, Afya, Nishati na miundombinu mingine)
Hayo ni baadhi tu ya mengi yanayokwenda kuinyonga CCM 2024/2025.

Nimejaribu kufanya research kidogo. Nimegundua kwa sasa Watanzania wengi wanajitambua sana ukilinganisha na miaka iliyopita. Zaidi ya Watanzania 7/10 wamechukizwa sana na mambo niliyoyataja hapo juu.
 
Tatizo upinzani nao hawako imara chadema ya 2010 au 15 nchi ingekua Yao mapema
 
Kama tume ya uchaguzi bado iko chini ya mwenyekiti wa ccm, na watu wakaendelea kudanganyika kuwa uchaguzi ndio unatoa viongozi, basi ccm itakaa madarakani sana hata ifanye nini. Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatatupa viongozi sahihi.
 
Wameongeza tozo kwenye umeme kimyakimya alafu chakushangaza tra wanaSema hiyo hela haiko kwenye hesabu zao

Sijui ripoti ya cag inasema ni I juu ya haya mapato
 
Pamoja na kwamba siikubali wala kuipenda sisiem, lakini pia bado sijaona chama ambacho kipo tayari kuchukua madaraka na kuwatumikia waTanzania
 
Kiukwel watanzania tutaishia kulalama tu kuhusu hili jini CCM mnyonya Mali za Tz Kila kukicha .lkn kiukwel wakuitoa CCM hapo ilipo n watanzania wenyewe c mtu yyt yule mwinginee...
 
CCM ni ile ile na madudu yake ni yale yale lakini still kutoka/kutolewa madarakani bado Sana si tuendelee kula tunda kimasikhara tu ndicho tunachoweza.
 
Kama tume ya uchaguzi bado iko chini ya mwenyekiti wa ccm, na watu wakaendelea kudanganyika kuwa uchaguzi ndio unatoa viongozi, basi ccm itakaa madarakani sana hata ifanye nini. Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatatupa viongozi sahihi.
Naunga mkono hoja. Kwa hali ilivyo katika Nchi hii kwa sasa, inahitajika kikosi au watu maalumu kujitoa SADAKA ya kweli na ya pekee ndipo Nchi hii itaingia kwenye mstari wake.

Ilitakiwa ipatikane siku moja tu ya kutangaza UKOMBOZI wa kweli katika Nchi hii.

Siku hiyo ifananishwe na usiku ule wana wa Israel walipokombolewa kutoka mikononi mwa Farao. Usiku ule kulikuwa na VILIO Nchi nzima kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Misri kufa.

Kwa hiyo, hatuhitaji siku mbili au tatu, bali tunahitaji siku moja tu ya kutangaza UKOMBOZI wa kweli kwa kujitoa SADAKA kufanya jambo ambalo kuanzia mtawala wa ngazi ya juu kabisa mpaka yule wa chini kabisa siku hiyo watasalimu amri na kuwapigia magoti Watanzania.
 
Kama tume ya uchaguzi bado iko chini ya mwenyekiti wa ccm, na watu wakaendelea kudanganyika kuwa uchaguzi ndio unatoa viongozi, basi ccm itakaa madarakani sana hata ifanye nini. Machafuko tu ama mapinduzi ya kijeshi ndio yatatupa viongozi sahihi.
KABISA HILI LINAPASWA KUFANYIKA
 
Pamoja na kwamba siikubali wala kuipenda sisiem, lakini pia bado sijaona chama ambacho kipo tayari kuchukua madaraka na kuwatumikia waTanzania
Kiongozi ni mtu, kama ni mbovu lazima na chama kiwe kibovu.Hata Dovutwa anaweza kuongoza vizuri au Hashimu Rungwe, haohao walioko UDP wakawa watendaji wazuri tu.
 
Wapiga kura wengi ni wanasisiemu, wapinzani wengi hawaendi kupiga kura
 
Hivi Gen Z kule Kenya ni chama gani?Hiyo misemo ya kiCCM kuwa Tanzania hakuna chama kilicho tayari kuongoza tumemsikia sana.
Jiulize;Kama hakuna chama kinachoweza kutuongoza,kwa nini CCM inakataa Kuandika Katiba Mpya au kuunda Tume Huru ya Uchaguzi?
Kwanini Sheria za Uchaguzi hazibadilishwi ili tuwe na wagombea binafsi ili tuacheni na vyama dhaifu?
Watanzania wapo tayari tangia 1992,tatizo ni uroho wa Madaraka wa CCM.Tusipindishe maelezo ama Tusihamishe magoli.Hii Nchi ni yetu sote.
Pamoja na kwamba siikubali wala kuipenda sisiem, lakini pia bado sijaona chama ambacho kipo tayari kuchukua madaraka na kuwatumikia waTanzania
 
1. Viongozi waliopo madarakani kujilimbikizia mali na kutumia mali za umma kwa ANASA.

2. Viongozi waliopo madarakani kutosikiliza na kuzifanyia kazi shida za wananchi(kuwachukulia wananchi kama WAJINGA)

3. Viongozi waliopo madarakani kuwalinda MAFISADI na MAJIZI na kuwakandamiza wanaowafichua hao MAJIZI na MAFISADI(Rejea kesi ya MPINA Vs BASHE na SPIKA)

4. Ugawaji wa RASILIMALI za Taifa kwa wageni.

5. Tozo na kodi za ovyo wanazobebeshwa wananchi kila uchao.

6. Wabunge na watumishi waandamizi wa serikali kujiongezea mishahara na marupurupu bila kujali shida za wananchi.

7. Serikali kushindwa kuboresha huduma za jamii(Elimu, Afya, Nishati na miundombinu mingine)
Hayo ni baadhi tu ya mengi yanayokwenda kuinyonga CCM 2024/2025.

Nimejaribu kufanya research kidogo. Nimegundua kwa sasa Watanzania wengi wanajitambua sana ukilinganisha na miaka iliyopita. Zaidi ya Watanzania 7/10 wamechukizwa sana na mambo niliyoyataja hapo juu.
Hivi unawaza nini? kwa tume hii na mfumo uliopo unadhani kuna upinzani watapewa nchi hii ?
 
Back
Top Bottom