SoC02 Kinachosababisha kutokuwa na Utawala Bora baadhi ya nchi nyingi

Stories of Change - 2022 Competition

Padone EPM

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2020
Posts
604
Reaction score
882
Habari,

Wana Jamvii leo naona tujikite kuangazia visababishi vya kutokuwa na Utawala Bora katika Nchi za Afrika. Kwanza kabisa Utawala bora ni dhana inayosimama katika msingi mkuu wa ujumuishaji na ushirikishwaji wa viongozi na wananchi katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.Ili Nchi au Taifa kuendeshwa katika misingi Bora lazima iwe na Utawala Bora unaohusisha viongozi wajibikaji na wazalendo na Nchi zao.

Endapo kutakuwa na Utawala Bora kunaweza kusababisha matumizi mazuri ya Dola, Maendeleo endelevu, Huduma Bora za kijamii,Amani na utulivu na pia kutatua migogoro mbalimbali.Bila kusahau endapo kutakuwa hakuna Utawala Bora Rushwa,ufujaji wa Mali za Umma, na migogoro mingi hutokea.zifuatazo ni sababu zinazopelekea kutokuwa na Utawala Bora:-

SABABU ZA KUTOKUWA NA UTAWALA BORA.

i)Kupeana Madaraka wao kwa wao.

-Hakika kutokana na Uendeshaji wa serikalii mbalimbali Nchi nyingi hususani Afrika wamejikita katika kuteua au kuwapa nyadhifa kubwa katika uongozi watu wao wa karibu na hiyo inaleta Radha mbaya ya uongozi endapo ikatokea ubadhirifu wowote hawawezi kushughurikiana kwasababu wote ni wamoja.

ii) Kutozingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi husika
-Kumekuwa na mazoea ya ukiukwaji wa Sheria Kanuni na Taratibu zilizowekwa Ili kusimamia haki na usawa kwa Wote hivyo basi inapoteza maana halisi ya Utawala Bora na inapelekea kutokuwa na Utawala Bora nchini.

iii) Kushamiri kwa Vitendo vya Rushwa
-Kama inavofahamika kuwa Rushwa ni Adui wa haki hivyo basi kukishamiri vitendo vya Rushwa ndani ya Utawala wa kitu Fulani au Nchi kunapelekea kutokuwa na Utawala Bora.

iv) Kutokuwepo kwa uwazi katika Uendeshaji wa shughuli za Umma
-Misingi ya Utawala Bora inahusisha uwazi juu ya Uendeshaji na maamuzi yoyote yatolewayo na serikalii husika chini ya Utawala wake kama hakuna huwazi basi hakuna Utawala Bora.

v) Kutowajibika kwa Viongozi
-Viongozi wengii katika Nchi nyingi Afrika hawawajibiki katika kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kupelekea kutokuwa na Utawala Bora.Viongozi wengi wamejikita katika maslahi binafsi na kusahau kutatua shida za wananchi.

vi) Kuvunja misingi ya Haki na usawa katika kuendesha shughuli za Umma. Hii inaleta maana mbaya kwa Utawala mbovu kwakuwa inakiuka misingi ya Utawala Bora Moja kwa Moja kwa maana inanyonya haki na usawa baina ya uongozi na watawaliwa.

Hivyo basi Ili kujenga na kuhakikisha Utawala Bora unafuatwa ipasavyo yafuatayo yanaweza kuleta tija na kuwepo kwa Utawala Bora,:-

1. Demokrasia
- kuhakikisha kuna kuwepo na demokrasia huru na inayoweza kujiendesha yenyewe bila kuingiliwa katika kujenga uongozi uliobora na dhabiti.Demokrasia ni mfumo wa uendashaji wa uongozi unashirikisha pande zote katika utoaaji wa maamuzi hivyo basi kuwepo na demokrasia katika upatikanaji wa viongozi mbalimbali wa serikali na sio kufanya teuzi za ndugu au watu wa kundi Moja wenye hisia sawa au linganifu.

2. Kuwepo kwa Utawala wa Sheria
- Kuwepo na Utawala wa Sheria pia ufuatwe bila kukiuka kipengele chochote hii itasaidia kuwepo kwa Utawala Bora. Pindi kiongozi anapokosea aweze kuwa chini ya Sheria na awajibishwe bila kuangalia Cheo chake.sheria rafiki zitungwe kwa kujadiliwa na pande zote mbili uongozi na wananchi na piah ziwekewe mfumo wa usimamizi madhubuti.

3. Ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi
- Hii Moja kwa moja inatoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao binafsi na pia kushiriki Moja kwa moja kwenye maamuzi na hiyo ndo maana halisi ya Utawala Bora. Endapo kuna tatizo linalowasibu wananchi na viongozi wanataka kulifanyia utatuzi inapaswa wakae kwa pamoja kujadili ni mbinu zipi za kutatua ki urahisi zaidi bila kuwa na malamiko pande zote.

4. Kudhibiti Vitendo vya Rushwa.
- Hii itasaidia Haki kupatikana kwa usawa kwa mwenye nacho na asiyenacho na kuonesha maana halisi ya Utawala Bora.kwa maana Rushwa ikiwepo itapindisha haki endapo mwenye nacho akitoa Rushwa kufanya haki iwe yake ko Vitendo hivo vikithibitiwa vitasaidia sana kuwepo kwa Utawala Bora unaosimamia misingi imara.

5. Kuboresha utoaji wa huduma za Umma.
-Hii itasaidia sana katika uongozi Ili kuonesha uongozi uliobora na wenye kujali wananchi kwa wakati bila kubagua. Katika utoaji wa huduma za kijamii serikali au viongozi wanatakiwa kuhakikisha wameboresha mifumo ya kuwafikia wananchi kwa wakati bila kuwa na ubadhirifu wowote katika Kila ngazi kwanzia ngazi ya Raisi adi balozi wa nyumba Kumi.

6.Uhuru wa vyombo Vya kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
-Nchi nyingi Afrika mahakama ndo chombo kikuu Cha kusimamia na kufafanua Sheria mbalimbali zilizowekwa lakini Ili kuhakikisha zinafanya kazi ipasavyo bila kuingiliwa na Muhimili wowote inatakiwa kiwe huru kufanya kazi yake. Pia chombo hiki kikiwa huru kinaweza mwajibisha Kiongozi yoyote aliekiuka Sheria hizo bila kuogopa Cheo chake au wadhifa alionao serikalini.

7. Vyombo Vya habari kuwa huru.
-Hii inasaidia sana kwa maana serikali au viongozi hawawezi kufika Moja kwa Moja kwa wananchi hivo basi kupitia vyombo Vya habari kutoa ukweli au kutangaza Yale yote yanayoendelea viongozi wanaweza pata taarifa na kutatua matatizo hayo haraka sana.

8. Uzalendo na uadilifu na Nchi.
- Hii inasaidia sana kuhakikisha Utawala Bora unafuatwa kwakuwa tutaweka tamaa zetu pembeni na kujikita kwa maslahi makuu ya Taifa ikiwemo kuchagua viongozi walio sahihi na pia kutunza rasilimali za Nchi bila kuzitumia vibaya.kwasababu kama kiongozi ni mzalendo atahakikisha anasimamia rasilimali za Nchi kwa wivu mkubwa dhidi ya watu wabaya.

Mwisho kabisa Ili kuhakikisha misingi ya Utawala Bora inafuatwa bila Kuvunjwa ni lazima tuwe wazalendo kwanza na Nchi zetu na tusifikilie maslahi Binafsi bali mustakabali wa Nchi kiujumla kwaajiri ya sasa na vizazi vya badae.Uzalendo Daima mbele Nakupenda Tanzania.

IMG_20220726_112301_564.jpg
 
Upvote 4
Habari,

Wana Jamvii leo naona tujikite kuangazia visababishi vya kutokuwa na Utawala Bora katika Nchi za Afrika. Kwanza kabisa Utawala bora ni dhana inayosimama katika msingi mkuu wa ujumuishaji na ushirikishwaji wa viongozi na wananchi katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.Ili Nchi au Taifa kuendeshwa katika misingi Bora lazima iwe na Utawala Bora unaohusisha viongozi wajibikaji na wazalendo na Nchi zao.

Endapo kutakuwa na Utawala Bora kunaweza kusababisha matumizi mazuri ya Dola, Maendeleo endelevu, Huduma Bora za kijamii,Amani na utulivu na pia kutatua migogoro mbalimbali.Bila kusahau endapo kutakuwa hakuna Utawala Bora Rushwa,ufujaji wa Mali za Umma, na migogoro mingi hutokea.zifuatazo ni sababu zinazopelekea kutokuwa na Utawala Bora:-

SABABU ZA KUTOKUWA NA UTAWALA BORA.

i)Kupeana Madaraka wao kwa wao.

-Hakika kutokana na Uendeshaji wa serikalii mbalimbali Nchi nyingi hususani Afrika wamejikita katika kuteua au kuwapa nyadhifa kubwa katika uongozi watu wao wa karibu na hiyo inaleta Radha mbaya ya uongozi endapo ikatokea ubadhirifu wowote hawawezi kushughurikiana kwasababu wote ni wamoja.

ii) Kutozingatia Sheria,Kanuni na Taratibu za Nchi husika.
-Kumekuwa na mazoea ya ukiukwaji wa Sheria Kanuni na Taratibu zilizowekwa Ili kusimamia haki na usawa kwa Wote hivyo basi inapoteza maana halisi ya Utawala Bora na inapelekea kutokuwa na Utawala Bora nchini.

iii)Kushamiri kwa Vitendo vya Rushwa.
-Kama inavofahamika kuwa Rushwa ni Adui wa haki hivyo basi kukishamiri vitendo vya Rushwa ndani ya Utawala wa kitu Fulani au Nchi kunapelekea kutokuwa na Utawala Bora.

iv)Kutokuwepo kwa uwazi katika Uendeshaji wa shughuli za Umma.
-Misingi ya Utawala Bora inahusisha uwazi juu ya Uendeshaji na maamuzi yoyote yatolewayo na serikalii husika chini ya Utawala wake kama hakuna huwazi basi hakuna Utawala Bora.

v)Kutowajibika kwa Viongozi.
-Viongozi wengii katika Nchi nyingi Afrika hawawajibiki katika kutatua matatizo ya wananchi kwa wakati na kupelekea kutokuwa na Utawala Bora.Viongozi wengi wamejikita katika maslahi binafsi na kusahau kutatua shida za wananchi.

vi) Kuvunja misingi ya Haki na usawa katika kuendesha shughuli za Umma. Hii inaleta maana mbaya kwa Utawala mbovu kwakuwa inakiuka misingi ya Utawala Bora Moja kwa Moja kwa maana inanyonya haki na usawa baina ya uongozi na watawaliwa.

Hivyo basi Ili kujenga na kuhakikisha Utawala Bora unafuatwa ipasavyo yafuatayo yanaweza kuleta tija na kuwepo kwa Utawala Bora,:-

1. Demokrasia.
- kuhakikisha kuna kuwepo na demokrasia huru na inayoweza kujiendesha yenyewe bila kuingiliwa katika kujenga uongozi uliobora na dhabiti.Demokrasia ni mfumo wa uendashaji wa uongozi unashirikisha pande zote katika utoaaji wa maamuzi hivyo basi kuwepo na demokrasia katika upatikanaji wa viongozi mbalimbali wa serikali na sio kufanya teuzi za ndugu au watu wa kundi Moja wenye hisia sawa au linganifu.

2. Kuwepo kwa Utawala wa Sheria.
- Kuwepo na Utawala wa Sheria pia ufuatwe bila kukiuka kipengele chochote hii itasaidia kuwepo kwa Utawala Bora. Pindi kiongozi anapokosea aweze kuwa chini ya Sheria na awajibishwe bila kuangalia Cheo chake.sheria rafiki zitungwe kwa kujadiliwa na pande zote mbili uongozi na wananchi na piah ziwekewe mfumo wa usimamizi madhubuti.

3. Ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi.
- Hii Moja kwa moja inatoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao binafsi na pia kushiriki Moja kwa moja kwenye maamuzi na hiyo ndo maana halisi ya Utawala Bora. Endapo kuna tatizo linalowasibu wananchi na viongozi wanataka kulifanyia utatuzi inapaswa wakae kwa pamoja kujadili ni mbinu zipi za kutatua ki urahisi zaidi bila kuwa na malamiko pande zote.

4. Kudhibiti Vitendo vya Rushwa.
- Hii itasaidia Haki kupatikana kwa usawa kwa mwenye nacho na asiyenacho na kuonesha maana halisi ya Utawala Bora.kwa maana Rushwa ikiwepo itapindisha haki endapo mwenye nacho akitoa Rushwa kufanya haki iwe yake ko Vitendo hivo vikithibitiwa vitasaidia sana kuwepo kwa Utawala Bora unaosimamia misingi imara.

5. Kuboresha utoaji wa huduma za Umma.
-Hii itasaidia sana katika uongozi Ili kuonesha uongozi uliobora na wenye kujali wananchi kwa wakati bila kubagua. Katika utoaji wa huduma za kijamii serikali au viongozi wanatakiwa kuhakikisha wameboresha mifumo ya kuwafikia wananchi kwa wakati bila kuwa na ubadhirifu wowote katika Kila ngazi kwanzia ngazi ya Raisi adi balozi wa nyumba Kumi.

6.Uhuru wa vyombo Vya kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa.
-Nchi nyingi Afrika mahakama ndo chombo kikuu Cha kusimamia na kufafanua Sheria mbalimbali zilizowekwa lakini Ili kuhakikisha zinafanya kazi ipasavyo bila kuingiliwa na Muhimili wowote inatakiwa kiwe huru kufanya kazi yake. Pia chombo hiki kikiwa huru kinaweza mwajibisha Kiongozi yoyote aliekiuka Sheria hizo bila kuogopa Cheo chake au wadhifa alionao serikalini.

7. Vyombo Vya habari kuwa huru.
-Hii inasaidia sana kwa maana serikali au viongozi hawawezi kufika Moja kwa Moja kwa wananchi hivo basi kupitia vyombo Vya habari kutoa ukweli au kutangaza Yale yote yanayoendelea viongozi wanaweza pata taarifa na kutatua matatizo hayo haraka sana.

8. Uzalendo na uadilifu na Nchi.
- Hii inasaidia sana kuhakikisha Utawala Bora unafuatwa kwakuwa tutaweka tamaa zetu pembeni na kujikita kwa maslahi makuu ya Taifa ikiwemo kuchagua viongozi walio sahihi na pia kutunza rasilimali za Nchi bila kuzitumia vibaya.kwasababu kama kiongozi ni mzalendo atahakikisha anasimamia rasilimali za Nchi kwa wivu mkubwa dhidi ya watu wabaya.

Mwisho kabisa Ili kuhakikisha misingi ya Utawala Bora inafuatwa bila Kuvunjwa ni lazima tuwe wazalendo kwanza na Nchi zetu na tusifikilie maslahi Binafsi bali mustakabali wa Nchi kiujumla kwaajiri ya sasa na vizazi vya badae.Uzalendo Daima mbele Nakupenda Tanzania.

View attachment 2304347
Hongera
 
Back
Top Bottom