Kinachosababisha macho kuonekana mekundu unapopiga picha usiku.

Kinachosababisha macho kuonekana mekundu unapopiga picha usiku.

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
xRed-Eye.jpg.pagespeed.ic.fE9IIZ3rfv.jpg


Wengi wamekuwa wakishangaa ni kwa nini macho huonekana mekundu kwenye picha pindi wanapopiga picha hususani nyakati za usiku kwa kutumia kamera yenye mwanga(flash).

Wakati wa giza mboni ya jicho hutanuka sana kuruhusu mwanga mwingi kuingia ndani ya jicho, kitendo hiki hufanya mishipa mingi ya damu kwenye jicho kutanuka na hivyo damu nyingi kusukumwa kwenye mboni ya jicho.

Unapopiga picha kwa kamera yenye flash, mwanga huu wa flash ya kamera huwa unakuwa na spidi kubwa sana kuliko uwezo wa mboni ya jicho kusinyaa, hivyo asilimia kubwa ya mwanga huu huakisiwa kwenye mboni ya jicho ilijoyaa damu kwa wakati huo.

Kitendo hiki hufanya jicho kuonekana jekundu, kutokana na wingi wa damu inayokuwa iko kwenye mboni ya jicho kwa wakati huo.

Kifupi wekundu ule unaouona ni mchanganyiko wa reflection ya mwanga wa kamera na damu inayokuwa kwenye mishipa ya mboni ya jicho kwa wakati huo.

=======

Maelezo kwa kina.

Mwanga huingia ndani ya jicho kupitia cornea. Baada ya hapo mwanga hufanyiwa utambuzi na retina na taswira hupelekwa moja kwa moja kwenye ubongo kupitia optic nerve. Kiasi cha mwanga kinachoingia kwenye retina hudhibitiwa na pupil. Wakati wa mchana sababu kuna mwanga mkali, pupil husinyaa na kuruhusu mwanga kidogo kuingia ndani ya jicho.

Wakati wa giza, pupil hutanuka kuruhusu mwanga wa kutosha kuingia. Katikati ya retina na sclera (sehemu nyeupe ya jicho) kuna kiwambo chenye tishu zinazoitwa Choroid. Safu hii husambaza damu, virutubisho na oksijeni katika maeneno ya nje ya retina. Choroid ina mishipa mingi sana ya fahamu.

Mwanga wa flash ya camera unapotoka, pupil huwa haipati muda wa kutosha kusinyaa, hivyo basi kiasi kikubwa cha mwanga huakisiwa (reflected) na fundus (sehemu ya mbele ya jicho). Kutokana na choroid kuwa na mishipa mingi ya damu, hivyo basi mwanga unaochukuliwa na lensi ya kamera huonekana mwekundu. Mtu akiangalia picha yake ataona macho yake yanaonekana mekundu.

Kutokana na angle ambayo mwanga huingia kwenye jicho ni sawa na engo (angle) ambayo mwanga huakisiwa kutoka nje, na jinsi flash inavyokuwa karibu na lensi ya kamera ndivyo kunavyokuwa na uwezekano mkubwa wa mwanga ulioakisiwa kuonekana na lensi.

Sababu nyingine inawezekana kuwa ni kiasi cha melanin kwenye kiwambo nyuma ya retina na umri wa mtu anayepigwa picha. Watu weupe (light skinned people) wenye macho yenye rangi ya blue huwa wanakuwa na kiasi kidogo cha melanin kwenye fundus zao hivyo basi uwezekano wa macho yao kuonekana mekundu ni mkubwa kuliko watu weusi (dark skinned people) ambao wengi wao huwa na macho yenye rangi ya kahawia (brown).

Watoto wadogo pia wakipiga picha na kamera yenye flash kuna uwezekano mkubwa kwenye picha akaoneka ana macho mekundu, hii inatokana na ukweli kuwa pupils za macho ya watoto hutanuka kwa haraka kuliko za wakubwa hata kwenye mwanga mdogo sana.
 
Nini kifanyike ili ukipiga picha usiku macho yasiwe mekundu
 
Nakumbuka tuliwai piga picha ya pamoja na wazungu mida ya usiku, sisi weusi macho yalikuwa mekundu na wao wakatoka vizuri tu..nahisi rangi ya ngozi ndo tatizo lenyewe
 
Maelezo yako yanaeleweka.
Nadhani hata mnyama simba akipigwa picha Usiku ndicho kinachosbabisha macho yake kuwaka.sasa basi embu nieleweshe.

Yakwake hayana mishipa ya damu??sababu huwa ni meupee kabisa.au kama umeishawahi kumtesa mbwa gizani akalia muda mrefu utaona macho yakimeremeta.
 
je nini husababisha wanyama ikifika usiku macho yao yanang'aa kama taa za gari
 
Nakumbuka tuliwai piga picha ya pamoja na wazungu mida ya usiku, sisi weusi macho yalikuwa mekundu na wao wakatoka vizuri tu..nahisi rangi ya ngozi ndo tatizo lenyewe
Hahahaha itabidi jamaa akufafanulie vzr tena. Kwann wazungu hayakutoka mekundu.
 
Kwani hii huwa inatokea mara zote tu ukipiga picha!!
 
Back
Top Bottom