SoC04 Kinachotuhusu sisi, bila ya kwetu sisi

SoC04 Kinachotuhusu sisi, bila ya kwetu sisi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Mamshungulii

Senior Member
Joined
May 3, 2023
Posts
175
Reaction score
88
Kuifikia Tanzania tunayoitaka ambayo itakuwa kwaajili ya wanajamii wote ,tunahitaji mbinu mbadala ambayo itaunganisha watu wote husika na itahusianisha huduma mbadala kwa makundi husika ya jamii kwa kuzingatia hitaji husika na mbinu iliyounganishwa na shirikishi.

Dhumuni la kuandika hili andiko ni kuangalia huduma mbalimbali kwa watu wenye ulemavu nchini mwetu, umakini mdogo hufanyika katika chaguzi za vifaa tiba na vifaa saidizi.Kwa maelfu ya watu masikini wenye ulemavu, kukosekana kwa vifaa-tiba nafuu ,visaidizi husika kulingana na muhitaji,na vifaa-saidizi kunaleteleza vizuizi katika muingiliano kijamii hii inajumuisha namna ya uendaji shule,ufanyaji-kazi ,namna ya kujimudu kujifanyia baadhi ya vitu vya msingi pasipo utegemezi.

20240527_223358-BlendCollage.jpg


Ni kweli kwamba masuala ya kijamii ni muhimu sana, na bado hayajashughulikiwa ipaswavyo katika maeneo ya mijini na vijijini. Kwamfano ,upatikanaji wa vitimwendo ni wa kuzingatia kwa wenye navyo lakini asilimia kubwa sana ya wenye uhitaji hawana na wengine walivyonavyo haviwakidhi mahitaji yao au havina vigezo au ni duni kulingana na mahitaji yao.

Mwanajamii katika mambo ya ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii huangalia mahitaji ya watu kulingana na utaalamu wake na kama watu wa fani zingine wanatambua mahitaji ya watu kulingana na utaalamu wao.Anapokutana na mlemavu katika makazi duni mijini au vijijini,inatafakarisha sana kuhusu uendelevu au udumavu wa huyo mlemavu;huanza kujaribu kutaka kutumia”mbinu unganishi” ikiwa ni pamoja na kumpatia vifaa-saidizi,namna ya kufika shule na ushiriki katika mambo ya jamii.Lakini ni muhimu kukumbuka kwamba
MTOTO HUYO NA MAMILIONI YA WATOTO WENGINE MAHITAJI YAO YA MSINGI NI AFYA NA UHAI WAO KILA SIKU UNAPASWA KUPEWA KIPAUMBELE ZAIDI.

KWA WATOTO WENGI, TISHIO KUBWA KWA USTAWI WAO NI NJAA.muhimu zaidi kwa mtoto yeyote, awe mlemavu au la, ni kukidhi mahitaji yake ya kimsingi ya chakula,malazi, na huduma muhimu za afya.

20240528_185148.jpg

Kiutendaji mara nyingi jamii hujikuta wakati wa kusaidia hupuuzia au kubeza mapungufu ya kiuchumi ya kifamilia sababu hiyo hujikuta inatumia pesa nyingi kununua vifaa-saidizi vingine visivyo rafiki au kulipia shule za gharama sana kufikia kumuona mtoto anakufa kwa magonjwa yasiyotibiwa ya kuambukizwa …...au anakufa kwasababu ya njaa.

Hebu tuangazie kisa cha kweli cha Mama huyu ambaye hadi sasa bado hajapata furaha ya kuwa Mtanzania yeye anaweza kusadifu watanzania wengi ambao hawajui hata nini maana ya maendeleo, na ukiwaelezea huzani umewatukana na kutoa machozi.Anasema.

“Unajua mimi ni mkazi wa Kijiji cha Selesele kata ya Lugeye ,kitongoSima,Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.miaka 4 iliyopita nilishuhudia Mume wangu akichomwa moto na wananchi wakisema kwamba ni mchawi ,wakati huo sikujua kwamba nilikuwa mjamzito na baada ya miezi 7 nikabahatika kujifungua mtoto huyu mlemavu.Huyu ni mwanangu wa 7 na nimemzaa akiwa hivi mlemavu wa kichwa kikubwa ,hakai,hatembei,haoni ,kila kitu hapohapo ,mwaka huu mvua imenyesha sana na baadhi ya vyumba tulivyokuwa navyo vyote vimebomoka na hiki chumba unachokiona lilikuwa ni jiko letu imetubidi sisi sote tuhamie humu pia vitu vyote viliungua na vingine Kwenda na mafuriko.Watoto wangu wengine wote wamefukuzwa kwa kukosa sare za shule,yule mwingine mkubwa yeye akienda shule nani atanisaidia kumuangalia huyu mdogo wao mlemavu na kulima ?yule mwingine kiziwi mdogo wangu uliyesema umempatia visaidizi vya kusikia ili umpeleke ajiunge shule ya kata,amefariki jana sababu ya kuharisha na njaa ,wanasema sisi ni familia ya kichawi,mimi na wanangu ,tulimzika pale alale karibu na wazazi wetu”... Nyamaza usilie

Umasikini na ulemavu huwaweka watu hasahasa watoto katika hatari zaidi ya moja, na zote lazima zishughulikiwe.Watu ambao wana uhitaji kwasababu zozote zile wanahitaji kujiunga katika mapambano ya kupata haki sawa na ushiriki kamili katika jamii yenye haki na inayojali zaidi.

Kwa hiyo,tunapofikiri kuhusu “teknolojia saidizi’’,ni muhimu kuzingatia sio tu teknolojia ngumu za misaada ya vifaa-saidizi,lakini pia ipo haja kuzingatia teknolojia laini ya Mawazo na hatua ambayo inaweza kuwafanya walemavu waendelee kuishi, teknolojia rafiki na inayoendana na mazingira yao ili kukidhi mahitaji yao kuwawezesha zaidi kujiamulia wenyewe bila utegemezi.

Tunahitaji teknolojia laini za kiubunifu. Hizi ni pamoja na shughuli na mbinu ambazo walemavu wanaweza kutetea haki zao, kujumuika katika jamii, na kujifunza ujuzi ili kupata riziki na kuwaepusha kuishi kama mnyama zizini.


HATUA ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA ILI KUONDOKANA NA HASARA ZA KIJAMII ZINAZOTOKANA NA UMASIKINI NA ULEMAVU.

20240527_214742-BlendCollage.jpg

Kuna ile kaulimbiu inayosema”kinachotuhusu sisi bila ya kwetu sisi”ni msemo ambao unawasilisha wazo kwamba hakuna sera wala sheria inayopaswa kuamuliwa na mwakilishi yeyote bila ushiriki kamili (wa makundi mbalimbali) walioathiriwa na sera au sheria husika.

Katika usasa kimtazamo tunazungumzia uhusika kitaifa, kabila fulani, watu wenye ulemavu, au makundi mengine mara nyingi yanatengwa na fursa za kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Suluhu ni bora zaidi wakati zinalenga watu wanaoathirika na masuala husika, watunga sera wanahitaji zaidi kutoka kwa watu walioathiriwa moja kwa moja na maswala yanayopaswa kushughulikiwa.

Ni kweli kuna baadhi ya harakati zinafanyika nchini kwa upande wa watu wenye ulemavu wakitaka kuwa na maamuzi katika mambo yanayoathiri Maisha yao wakisisitiza haki za kijamii na nafasi sawa katika mambo kama vile upatikanaji, elimu, ajira na burudani. Wanahitaji sauti itakayowangoza katika utungaji wa sera na sheria hasa zinazowaathiri.


Leo hii yakufanyiwa na watu ni mengi, haitoshi kufanya kufanyika kwa kushirikiana….maelekezo mengi yenye mamlaka na yasiyokuwa ya kibunifu, kutokushirikishwa katika utatuzi wa tatizo. Wenye uhitaji kugeuzwa kama vitu, badala ya kufanyiwa kazi kwa kuzingatia jinsi alivyo/walivyo na mahitaji yake kipekee na matakwa yao wenyewe mara nyingi huachwa hasa watoto katika mlolongo wa matatuzi bila kushirikishwa kulingana na matakwa yao.

20240527_213429-BlendCollage.jpg


Kuna hitaji la dharura la vifaa vya mafunzo na kozi ili kuweka mkazo mdogo katika kufuata maagizo sanifu, na msisitizo zaidi katika mtazamo wa uchunguzi, wa kutatua matatizo ambapo mtu mlemavu na wanafamilia wanajumuishwa na kusikilizwa kama sawa.

Kote Tanzania unaona watoto wadogo kwenye viti mwendo vya wakubwa, na wakubwa wembamba katika vitimwendo vikubwa, vipana, vizito ambavyo hawawezi kujongea kwa urahisi.

20240527_205822-BlendCollage.jpg

Tunachohitaji ni mawasiliano yanayojali na kuzingatia umuhimu wa kila mtu. Kwasasa tupo kwenye utandawazi wafanya maamuzi, wamiliki wa maamuzi wote wanaweza kuwasiliana kwa haraka sana dunia nzima kupitia akilibandia. Kwa hakika ambao hawana teknolojia ya sasa wana hatihati kuachwa nyuma.

Kiuhalisia sehemu kubwa kibinadamu imeachwa nyuma. Leo kuna sehemu nyingi hawafikishiwi rasilimali zinazofaa kwa wakati. Kuzingatia kielelezo cha maendeleo cha kimataifa kwa kuzingatia kuutangaza UCHOYO badala ya UHITAJI kumefanya watu kujilimbikizia mali na kuukatili utu. Na kukosekana uwiano kati ya masikini na Tajiri. TUBADILIKE

TUNAPOSONGA MBELE KWA KUKIMBIA, TUSISAHAU WATAMBAAO, ILI TUFIKE SALAMA KWA FURAHA NA TABASAMU KWENYE TANZANIA TUNAYOITAKA.


20240527_222249-BlendCollage.jpg

 

Attachments

  • 20240527_221347-BlendCollage.jpg
    20240527_221347-BlendCollage.jpg
    226.9 KB · Views: 4
  • 20240528_135515-BlendCollage.jpg
    20240528_135515-BlendCollage.jpg
    389.3 KB · Views: 3
  • 20240527_222936-BlendCollage.jpg
    20240527_222936-BlendCollage.jpg
    186.9 KB · Views: 2
  • 20240527_223358-BlendCollage.jpg
    20240527_223358-BlendCollage.jpg
    200.8 KB · Views: 2
Upvote 0
Back
Top Bottom