Kinachowaponza watawala ni kuongoza kwa mazoea

Kinachowaponza watawala ni kuongoza kwa mazoea

Mchokoo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
1,181
Reaction score
1,579
Eti, mbona lile walisema wee lakini bado tulifanya yetu na hakuna kilichotokea? Achana nao, kwa maana kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji.

Halafu, mbona Magu alipokuwa anamua lake hakuna aliyefurukuta?

Hatukatai, ila tambueni nyakati zinabadilika, vilevile watu wanabadilika. Yaani watanzania wa leo siyo wale wa jana.

Hivi suala la bandari hamuoni kama limeshatugawa vipande vipande?

Wengi tunajiuliza; ni ubora gani uliomo ndani yake, ambao wenzetu mnaona ni aheri tuparanganyike kuliko kuukosa huo?
 
Kushindwa kusoma alama za nyakati ndio kinaenda kuwaondoa ccm madarakani bila katiba mpya wala tume huru ya uchaguzi,hawa watu bado wanawaza kianalogia wakati dunia iko kidigital,wameshindwa kusoma alama za nyakati bado wanatumia mbinu za miaka ya 1960.

Nfano nchi zenye bandari ikiwepo Dubai Durbun walishahama kutoka kwenye mifumo ya kutoza ushuru bandarini kabla ya biashara kufanyika free ports wanatumia mifumo shirikishi ili kuongeza idadi kubwa ya wafanyabiashara na wanunuzi kukutana kukuza uchumi kupitia bandari huko kwetu wanawaza kuuza kabisa.
 
Utaonaje ubora wa mkataba wakati ulishazoea kuiba pale Bandarini?
 
CCM hawaogopi wananchi kwasababu hawapo madarakani kwa ridhaa ya wananchi,unless Kuna badiliko lolote kwenye tabia za waTZ CCM hawaogopi chochote
 
Na wew utauonaje ubovu wa Mkataba wakati umezaliwa na kukuzwa ndani ya wanufaika wa upigajia wa rasilimali za Taifa.
Sio kila nayetetea ubovu wa mikataba ni mnufaika,kipindi cha magu kuna watu walifurahi sana kuona watu wenye uwezo wa kiuchumi kurudi nyuma wakifikiri mtu akiwa na uwezo anajidai au analinga,kuna watu wanafurahi kuona watu wakiwa masikini wakutupwa ndani ya nchi tajiri wao ndio furaha yao. Mfano mchawi anawezo wa kuingia bank kuiba pesa kichawi lakini kilasiku kusumbua watu kuwakalia kama vigoda kesho akiamka hata mbuni hana.
 
Sio kila nayetetea ubovu wa mikataba ni mnufaika,kipindi cha magu kumawatu walifurahi sana kuona watu wenye uwezo wa kiuchumi kurudi nyuma wakifikiri mtu akiwa na uwezo anajidai au analinga,kuna watu wanafurahi kuona watu wakiwa masikini wakutupwa ndani ya nchi tajiri wao ndio furaha yao.
Ubaya au uzuri wa kitu huonekani machoni au ndani ya fikra za mtu. Kwa upande wako Mkataba unauona hauna shida, yaweza kuwa umeusoma ukauelewa au umesikiasikia tu kama wengine wanavyousikia, na kuna wengine wanakubwa tu kwa ushabiki. Forecasting Forecasting Forecasting.
 
Chambua mkataba kifungu kwa kifungu acha kucheza na maneno eti wizi bandarini wakati kila tasisi zimejaa wizi mbona msizibinafsishe.
 
Chambua mkataba kifungu kwa kifungu acha kucheza na maneno eti wizi bandarini wakati kila tasisi zimejaa wizi mbona msizibinafsishe.
Kijana.., Think Big. Naona kama hujielewi, mim sijazungumzia Wizi Bandarini.
 
Utaonaje ubora wa mkataba wakati ulishazoea kuiba pale Bandarini?
Wakati tunaletewa mradi wa bomba la gas, porojo ilikuwa ni mabadiliko ya tabia hivyo umeme wa maji sio wa kuaminika. Kisha kundi hilo lililotuimbisha wimbo ule wa umeme wa gas na athari za mabadiliko ya tabia nchi kuhusu umeme wa maji, likawa ndio kinara wa kusifia bwawa la umeme la SG!
 
Huoni matunda ya Umeme wa Gesi kwenye miradi ya Kinyerezi na viwanda vya Dar?

Unadhani usingekuwepo huu mradi na mito hii inavyokauka hali yetu ingekuwaje?
 
Kwa huu mkataba Mbarawa amewaingiza Cha kike.
Utabiri wa shehe Yahya utatimia kwa Mara ya nne.
1. Alisema rais ajaye atatokea Pwani. JK
2. Atafuatiwa na atakaye toka bara na atakaa muda mfupi.
3. Ajaye Ni mwana mama.
4. Atakabidhi madaraka kwa upinzani............DP w oyee.
 
Back
Top Bottom