Mikopo Consultant
JF-Expert Member
- Oct 28, 2024
- 529
- 1,150
Baada ya madudu mengi kutokea ndani ya mifumo ya kiutawala kwa miaka 5 iliyopita ambapo CCM ilitawala yenyewe, pamoja na misuguano ya ndani ya chama, imepelekea CCM kuona umuhimu fulani walau wa kuwa na uwakilishi mdogo wa wapinzani wenye nguvu ili kufunika kombe na kuendelea kuwahadaa wananchi na jumuiya ya kimataifa.
Kwa maana hiyo, CCM wanaichukulia CHADEMA kama mtaji muhimu wa kisiasa ili waondokane na ile aibu ya kutawala peke yao kupitia uharamia wa chaguzi. Na hapa wanawahitaji CHADEMA tuu, kwa sababu hivo vyama vingine havina ushawishi kwa watanzania (walau visiwani wanajua ACT hawana shida, washakubali michezo yao)
Hivyo, hoja ya 'No reforms, no election' inawaumiza na kuwatesa sana CCM kwasababu wanaona kabisa kuna hatari ya kuwakosa CHADEMA kwenye ballot kitu ambacho wanahisi kitakuwa kimewaharibia sana mipango yao.
Nilivyoona clip ya CPA Makalla akitaka kabisa kulia machozi kuwaomba CHADEMA washiriki uchaguzi, nikathibitisha kwamba, hii no reforms, no election ni mechi ambayo Tundu Lissu amekabia juu kabisa na amewashika vilivyo CCM kwenye koo.
Chopa zikianza kuruka huku na huko kuipigania agenda ya 'no reforms, no election', nina wasiwasi Mh. CPA Makalla na Babu Wasira watamfuata Lissu kwa magoti, wakiwa wamechoka kabisa na kukaukiwa makoo.
Hofu yangu kubwa ni CCM kufanya hata uhuni wa kufanikisha wanachadema feki kuomba kuchukua fomu za kugombea ubunge kwa ticket ya CHADEMA. (Kama iliwezekana kwa wabunge 19, hata hapa inaweza kuwezekana) Hapa muwe macho CHADEMA.