Kinachowauma Simba ni Timu nyingi kutohongeka kwa sasa

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Simba ni kama sikio la kufa tu hata uliwekee Boric Acid ear drops hamna kitu.Simba wamebaki kumpigia promo GSm na kuacha kumpigia Promo boss aliyenunua timu yao mo.

Kwanini Simba wanalia sana na ishu za Udhamini Jibu ni jepesi tu baada ya ligi yetu kukua na wenye pesa zao kuamua kumwaga mpunga timu zinasajili wachezaji wazuri na mabenchi ya Ufundi mazuri na kumwaga mipunga mizuri kwa wachezaji.

Hili limekua gumu kwa Simba kwani wachezaji wengi wamegomea bahasha zao na kukaza viwanja kwa kucheza kwa juhudi kubwa.

Zamani ligi yetu ilikua haina maokoto baadhi ya timu zilikua zinakosa hata fedha za kununua jezi hapo ndipo Simba walikua wanafanya michezo yao michafu kwa kuhonga wachezaji rejea Ishu ya ULIMBOKA huku alikamwata Live akihonga wachezaji wa Timu ya Mtibwa ili waachie magoli.

Rejea ishu ya KABWILI huyu walienda na gia ya kumnunulia gari kipindi kile yanga IPO apeche alolo ili aruhusu magoli uzuri dogo alisema ya moyoni.

Hii ndio baadhi ya michezo michafu ya Simba pia kuna refa mmoja wa Zamani alipokua anahojiwa Azam anasema Simba walimpa mpunga ili awape wachezaji wa Yanga kadi kumbe basi hii ndio michezo yao michafu na wameanza kitambo.

Simba wanapiga kelele ili kuwakatisha tamaa wadhamini wajitoe timu zikose fedha ili waweze kupitisha fedha zao haramu.

Either wanaweza kuwa wanatoa bahasha za khaki mpunga unaliwa na bado wanakaziwa walifanikiwa tu siku ile wanacheza na Tabora Utd kwa hisani ya mdau wao mkubwa aliyeko Tabora.

Ila Mpira wa Tanzania kazi kweli kweli kwa hiyo Simba wanataka wasikaziwe wapate ushindi kirahisi tu kama wanacheza Moro kids.

Waache kelele kwa kushirikiana na wachambuzi wao uchwara na wawekeze kwenye Mpira.
 
Kwahiyo tuseme timu zimgoma kupokea rushwa [emoji3][emoji3][emoji3] hivyo ni mwendo wakupokea vichapo tu ha ha ba
 
Iko siku mtaumbuka tu kwani dunia ina siri basi,kama mayele alivyowaumbua na mijini yenu
 
Tunangoja droo ya klabu bingwa sie jioni ya leo.

Yoyote aliye mbele yetu sisi Simba aje tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…