Kinamama hoyee! Ewe mama, unataka kuwa Askofu? Ruksa!

Mimi nina majukumu mengine mazito. Ila mifano iko mingi ya maaskofu wanawake
We unazungumzia maaskofu wa kike tu!
Siku hizi tuna wafalme wa kike pia akina zumaridi
 

Ndugu yangu wewe upo sana kutoka kwenye uelewa juu ya ukristo.

Jibu maswali haya machache, kisha nikupeleke darasani taratibu:
1. Masiha Yesu, kabla ya kuondoka Duniani, aliacha kitabu chochote kama mwongozo wa ukristo?

2. Biblia iliandikwa na nani, na aliandikwaje?

3. Nani na lini biblia ilipangwa kwa muundo wa leo au unaokaribiana na huu wa leo?

4. Nini lilikuwa lengo la kuandikwa biblia, na lililengwa kundi gani?
 
Hayo maswali ungewauliza watoto wa Sunday School.
 
Yale Yale ya Eden,

Kwamba itakuwa sawa na Mungu, ukijua mema na mabaya.

Mwanamke ni msaidizi, ni heri kukaa kwa Nafasi yako, kutamani Nafasi ya Mwanaume ni UOVU.

By the way,

Kibiblia, Cheo Cha Askofu ni chini ya Cheo Cha mchungaji.

Mwanamke uwe Askofu kwa wanawake wenzio ukiwafundisha jinsi ya kutunza familia na kutii waume zenu.
 
askofu ananyonyesha baby, bizy home. Ni ngumu kuchanganya baadhi ya vitu
 
Acha upotoshaji
 
Kibiblia, Cheo Cha Askofu ni chini ya Cheo Cha mchungaji.

Mwanamke uwe Askofu kwa wanawake wenzio ukiwafundisha jinsi ya kutunza familia na kutii waume zenu.
Weka vifungu vya ku-support hoja zako. Neno ndio taa yetu
 
Kama ni hivyo basi nami nampendekeza Mh. Dorothy Gwajima.
 
ww n mpinga kristo OVA
 
Weka vifungu vya ku-support hoja zako. Neno ndio taa yetu
Usipotoshe maandiko,

Mstari ulioquote, umeeleza wazi kuwa sifa za mtu huyo ASKOFU, ni shart awe MUME wa mke mmoja.

Ni vyema mwanamke kukaa Katika Nafasi yake.
 
(2 Timothy 2:12)

Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, Bali awe Katika utulivu.
 
Utetezi wako umejikita kwenye mawazo binafsi wala si maandiko. Mi huwa nafatilia posts zako nikajua we ni mtu makini kumbe now najithibitishia kwamba sikuwa sahihi vile nilikuwa nakuchukulia.
Duh, wewe kweli ni Clever505
Kumbe unapenda kila point iwe na maandiko? Safi sana. Ila ujue kuna wengine hawapendi kuona vifungu vifungu kila wakati. Ndio sababu wakati mwingine naweka maelezo tu.

Haya, twende pamoja sasa kwa Maandiko
Katika Waefeso 4:11-13 tunasoma kwamba
Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;

Katika orodha hiyo umeona wadhifa wa Askofu? Hakuna! Katika Andiko lile la mwanzo kabisa, Askofu maana yake mwangalizi(Overseer). Kwa mantiki hiyo, Mtume ni huduma ya juu kuliko ya Askofu. Askofu ni kazi kama ya Administrator. Ndiyo sababu Paulo anaiita kazi njema.

Sasa kama unakubaliana na mimi kwamba Mtume yuko juu ya Askofu, angalia hapa jinsi Paulo anavyosema katika Warumi 16:7 (SRUV)
Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu.

Katika maandiko ya awali kabisa ya Kigiriki, Yunia ni "Ἰουνίαν" (Iounian). Hili ni jina la kike maarufu kabisa Roma. Sasa Paulo anamtaja Yunia kuwa maarufu miongoni mwa mitume. This means, Yunia alikuwa Mtume mwanamke. Kwa mantiki hiyo kama Yunia alikuwa na cheo au huduma hiyo ya juu ya Utume, unashangaa nini nikikuambia kwamba mwanamke anaweza kuwa Askofu, just an Overseer?

Tatizo lililopo ni kwamba katika baadhi ya makanisa, vyeo vya huduma havifuati Biblia. Baadhi ya makanisa wamejitungia vyeo na majina yao wenyewe kama vile Kardinali, Padre, Askofu Mkuu nk. Waliojitungia vyeo ndio hao wanaoona Papa ni mkuu kuliko Askofu. Na wengine wanaona Askofu ni mkuu kuliko Mtume! Na wengine wanaofuata Maandiko wanaona Mtume ni mkuu kuliko Askofu.
Umenipata Clever505 ??
 
(2 Timothy 2:12)

Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, Bali awe Katika utulivu.
Unapotafsiri maandiko unatakiwa kuangalia muktadha, na kujiuliza: nani anaambiwa na kwanini. Ingekuwa mwanamke haruhusiwi kufundisha, Paulo angemkataza pia Prisila(mwanamke) kufundisha. Lakini haikuwa hivyo, Paulo aliwaacha Prisila na Akila Efeso wafanye huduma. Katika Matendo 18 tunasoma kuwa Prisila na Akila walimfundisha Apolo kwa usahihi.
 
Umeamua kurekebisha neno
Kama mpaka Paul aseme ni sheria ya milele ndio ukubaliane nae.
Naomba andiko linalosema kuokoka ni sheria ya milele na sio lilikuwa hitaji la lazima kwa watu wa wakati ule?
 
Tatizo tulilonalo wakristo ni kwamba mtu anapoamua kutetea jambo atajitahidi sana kuungaunga maneno ya Biblia yaendane na anachokitaka. Mada yako Haina Aya maalumu kabisa ya kuitetea ndo naona hapa unajitahidi kuunga maandiko.

Kuna mwamba Fulani ni shoga, huwezi amini ni kwamba anajitahidi kuleta aya za Biblia zimuunge mkono kwenye uovu wake na usipokuwa makini unaingia mkenge kumuamini.

Baadhi ya wakristo wanalazimisha utatu uwepo kwenye Biblia wakati hilo jambo halipo. We pia kwa makusudi kabisa unalazimisha askofu wa kike aruhusiwe. Sasa sio kesi endelea na Imani yako. Ila elewa hilo sio fundisho la Biblia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…