Elections 2010 Kinana amechanganyikiwa au ni kiziwi/kipofu?

Dark City

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2008
Posts
16,253
Reaction score
11,626
Kinana amesema kupitia BBC kuwa mwaka huu CCM imetumia gharma kidogo kuliko miaka yote? Mhhh... haya bwana hawa jamaa naona hata vichwa hawana tena.

Sikiliza hapa kuanzia dak ya 55.00
BBC Swahili - Mwanzo

Dondoo:


Mwandishi: Mbona ahadi zenu nyingi sana?
Kinana: ahadi siyo nyingi, ila zinaonekana nyingi kwa sababu ndizo wananchi wanataka kuzisikia
Mwandishi: Kwanini CCM mnamwandama slaa?
Kinana: Ndiye anayeongoza kura za maoni, pia anaongoza kupiga kelele zisizo na msingi na amepeleka kesi nyingi kwa msajili na mahakamani zisizo na maana.
Mwandishi: Mbona anapokelewa sana na wananchi?
Kinana: Hakuna mtu anayepokelewa zaidi ya JK? Hata hivyo mbona Mrema alipokelewa na watu wengi zaidi?
Mwandishi: CCM imetumia gharama kubwa mwaka huu, kwa nini?
Kinana: Atakayeweza kueleza gharama za CCM ni Msajili. Hata hivyo mwaka huu CCM imetumia gharama kidogo kuliko miaka yote....


.......Nimechoka na hawa watu..
 
Anaweza kuwa sahihi 2005 haikuwa mchezo...EPA,DEEPGREEN,MEREMETA etc etc
 
Hivi bado huwa unamsikiliza Kinana????

Mkuu nilikuwa nasikiliza BBC ndo nikakutana na vioja. Halafu ukimsikiliza vizuri, utangundua kuwa ana wasi wasi hadi anakuwa kama anatetemeka!

Mhhh, kuishi kwingi ni kuona mengi!!! Labda nitamwona hata Rais wangu mupya!!
 
Kila nikifuatilia mahojiano na huyu mzee nagundua kweli kwamba huyu mzee hana busara, ni jazba tu na emotions!
 
Hapa ndipo watakapopigiwa bao. Maana Kikwete ndiye mrema wa leo.
 

Hiyo sentensi ni ya kuchanganyikiwa...sasa nani zaidi...Mrema AU Kikwete?....1995 Kikwete mwenyewe kimoyo alimuunga mkono Mrema baada ya yheye kukosa CCM
 
Mkuu nilikuwa nasikiliza BBC ndo nikakutana na vioja. Halafu ukimsikiliza vizuri, utangundua kuwa ana wasi wasi hadi anakuwa kama anatetemeka!

Mhhh, kuishi kwingi ni kuona mengi!!! Labda nimwona hata Rais wangu mupya!!

Itakuwa ni raha iliyoje! Nchi nzima italipuka kwa furaha kwa mafisadi kuondolewa madarakani.
 
Hiyo sentensi ni ya kuchanganyikiwa...sasa nani zaidi...Mrema AU Kikwete?....1995 Kikwete mwenyewe kimoyo alimuunga mkono Mrema baada ya yheye kukosa CCM

Huyu Kinana nadhani anatamani kampeni zingeisha leo basi tu mambo yaishe. Kwa jinsi anavyoongea...inaonesha amejichokea!

Ila amenishangaza kwamba ahadi siyo nyingi, ila zinaonekana nyingi kwa sababu ndizo wananchi wanataka kuzisikia. Ya kweli hayo?
 
Mirungi imemchanganya huyo msomali anaona duble duble,Dr wa ukweli anawapeleka mchaka mchaka
 
Huyu ni mwizi na mhujumu uchumi kwa muda mrefu sana....ameshiriki kwa asilimia mia moja kuua JKT kama ambavyo ameua sana wanyama katika mapori ya nchi yetu...ana wasiwasi Dr Slaa akiingia itakula kwake...time will tell,tutafukua hata makaburi yao, wewe subiri tu haki haipotei..
 

Kuna wadogo zake wasomali wamekamatwa huko mtwara walikuwa wanavizia kuteka meli inasemekana wawili ni watoto wa mama yake mdogo.Na yeye ndiyo anawapa silaha za kutumia si alikuwa mwanajeshi anajua wapi pa kupata silaha.Mradi wa utekaji meli ni wa kinana na mwenzake wa PARADISE HOTEL
 
Hiyo sentensi ni ya kuchanganyikiwa...sasa nani zaidi...Mrema AU Kikwete?....1995 Kikwete mwenyewe kimoyo alimuunga mkono Mrema baada ya yheye kukosa CCM

Huenda kuna kaurafiki ka siri kati ya JK na Mrema, si ajabu baada ya JK kutemwa na Mkapa kwenye kura za maoni 2005, alikuwa na bifu na si ajabu alimpigia chapuo Mrema. May be this time Mrema is paying back!! Siasa ni mchezo mgumu kweli jamani lol
 

Weweeeee,
lete habari tuwamanye hawa wevi wa njii yetu.

ila chama alichomo ndo dira yake,na wala haiwapi shida kuishi na mwivi huyu!
 
Hapa ndipo watakapopigiwa bao. Maana Kikwete ndiye mrema wa leo.
Jamani wacheni kujfariji hali siyo nzuri. Sasa plot yote karibu imeishajulikana kama 80%. Kwanza REDET na Synovate wanalainisha mazingira kwa tafiti feki. Pili lawama za watu kuvunja amani na utulivu. Tatu vyombo vya ulinzi na usalama kutoa vitisho. Nne Tume ya Uchaguzi kutoweka wazi Daftari la Wapiga kura mapema ili lihakikiwe. Baada ya hapo CCM imeanza majigambo ya ushindi wa kishindo kwa kutumia matokeo ya hizo tafiti feki. Siku ya uchaguzi inavyokaribia ndivyo tutakavyoanza kutangaziwa masharti ya kisifanyike hiki au kile siku hiyo. Yote ikilenga kubana wapiga kura wasijue na kutetea matokeo ya uchaguzi halali. Je, tunayo majibu ya changamoto hizo? Kama hatuna twendeni tukalale CCM imeishapeta.
 
Kinana anatetea ugali wake sasa, kilichobaki ni porojo tu. Katika watu niliokuwa nawaheshimu ccm mmojawapo ni kinana, lakini sasa ni miongoni mwa watu ninaowaona wa hovyo ndani ya ccm pamoja na makamba. Kazi kuongea pumba tu na mambo yasiyokuwa na utafiti wowote.
 

kwa nn huyu kimama asirudi kwao somalia awapelekee hizo busara zake...!

kwa nn asiongelee meno ya tembo yaliokamatwa kwenye meli yake..!
 
Kinana hivi sasa ni mzigo kwenye kampeni ya Jk na wala siyo vinginevyo. Hii siyo 1995 huu ni mwaka wa 2010. Tofauti ni kubwa mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…