Kinana anatekeleza Ilani ya CCM kwa nguvu zote!

Kinana anatekeleza Ilani ya CCM kwa nguvu zote!

gwamaka aswile

Senior Member
Joined
Mar 26, 2015
Posts
186
Reaction score
106
:dance:
Ndugu Mhariri, awali ya yote napenda kuipongeza serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kazi nzuri inayofanya kuhakikisha nchi yetu inakuwa na amani na wanachi wanapata maendeleo.
Nasema hivyo kwa sababu hivi sasa nchi yetu inamaendeleo katika nyanja mbalimbali, mfano barabara, shule, hospitali na nk.
Yote hayo ni mambo yanayofanywa na serikali ya CCM licha ya kwamba kuna changamoto kadhaa ambazo serikali inakumbana nazo lakini kadiri siku zinavyokwenda naamini mambo yatakuwa safi.
Hata hivyo, nashangazwa na baadhi ya watu hasa viongozi wa siasa kutoka kambi ya upinzani ambao wanabeza kila kitu kinachofanywa na serikali ya CCM.
Mfano hai ni pale wanapomshambulia Katibu Mkuu wa CCM, Abdurhaman Kinana ambaye hivi sasa yupo katika ziara nchi nzima kukagua miradi ya maendeleo na kusema anawahadaa wanachi ili waichague CCM katika uchaguzi mkuu ujao.
Napingana na watu hao na kusema katibu mkuu huyo anafanya hivyo kutekeleza Ilani ya chama chake kuhakikisha Watanzania wanapata maendeleo na hivyo ndivyo chama hicho kimekuwa kikifanya tangu kuanzishwa kwake 1977.
Napenda kuwaasa wananchi kutosikia maneno ya watu hao wachache ambao hawana jipya zaidi ya kupinga mazuri yanayofanywa na CCM, kwa kuwa wana masikio na wana macho wanaona mambo mazuri yaliyofanywa na yanayoendelea kufanywa na serikali ya CCM.
Kwa kuwa wanayaona nawaomba wasihadaike ikifika Oktoba waichague CCM ili iendelee kuliongoza taifa letu.
 
Duu kweli hawanjamaa ndo maana ni wazee wa kijani mi nawafuatilia kwa makini nione mwisho wao!
 
Duu kweli hawanjamaa ndo maana ni wazee wa kijani mi nawafuatilia kwa makini nione mwisho wao!
Hawa wazee wa kijani wanajiamini na wamejipanga vizuri. Hebu tuone na wengine watajipanga labda miaka ijayo. Sisi tunasubiri kujiandikisha ili tuipigie kura Katiba Inayopendekezwa. Sijui wewe umeshajiandikisha au unasubiri awamu hii inayoanza Ruvuma, Lindi na Mtwara!!
 
Back
Top Bottom