Kinana atoboa siri ya mchakato wa maridhiano

Kinana atoboa siri ya mchakato wa maridhiano

comte

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2011
Posts
9,019
Reaction score
6,825


Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amewataka vyama vya upinzani nchini kuwa waungwana na wenye shukrani kwani Rais Samia amefanya mambo mengi mazuri hivyo anastahili kuheshimiwa.

Akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Tabora, Kinana amesema;"Walikuwa hawajapokea ruzuku yao tulipo Kutana na Rais na wao, wakasema sasa tunaona tumeelewana tunaomba ruzuku yetu tuichukue na mtupe ruzuku yetu tangu uchaguzi ulipomalizika, Rais akasema sawa andikeni barua, wameandika ruzuku yao wakalipwa lakini matokeo yake unaambiwa Rais huyu hana maana Dooh!!"

" Nimekupa hela zako sina maana , nimekufungulia mikutano akili za matope, lakini Rais ni binadamu inataka moyo wa uvumilivu sana mtu kuweza kuvumilia mambo yote haya, ukiangalia mamlaka aliyonayo Rais lakini akasema hapana nimewasikia nitaendelea na kazi yangu Watanzania ni waungwana wataelewa jambo hili vizuri zaidi ya wanavyolieleza wao wapinzani"

KinanaKinana ameendelea kuwasihi upinzani kuacha kejeli dharau na matusi kwani havisaidi kuletea maendeleo"Niwasihi matusi kejeli ,dharau , kupuuza hakusaidi sana... Sisi tumekaa nao tumewaheshimu , tumewasikiliza, kikao cha mwisho na wao tulifanya mwezi Juni hakuna agenda hata moja imetoka CCM zote zimetoka kwao na nyingi tumezifanyia kazi, walikuwa na wanachama wao walikuwa na kesi nyingi tu zote zimefuatiliwa kwa utaratibu husika nyingi zimefutwa zimebaki mbili tu na hizo mbili ni kwa sababu zinahusika na mauaji huwezi zifuta haraka haraka....

Basi jamani yote haya hayafai? haya stahili kushukuriwa? haya stahili Rais kuheshimiwa?""Tumefungua mikutano kujakusemwa , kusakamwa na kuzalilishwa, tumetoa ruzuku walioomba kusafiria kupata fursa yakutusema na kututukana, watu walikuwa wamefungwa wameachiliwa atusemi tumewafanyia hisani lakini tumekuwa waungwana, Rais amekuwa muungwana sana" Alisisitiza Kinana

Aidha Kinana amesema kuwa Watanzania wanapaswa kuimarisha umoja na mshikamano na kutokutumika vibaya uhuru waliopewa."Watanzania tuimarishe umoja na mshikamano ,tupokee kwa mikono miwili utaratibu huu wa maridhiano ambao Rais ameuridhia kwa kupenda kuleta amani na umoja katika nchi yetu, tusiutumie vibaya, usifikiri kwa kutukana, kwa kukejeli, kwa kuonyesha dharau hoja yako itakubalika kwa haraka hoja yako itatupiliwa mbali, peleka hoja yako kistaarabu itakubalika " _Alisema Kinana

Pamoja na yote Kinana amewasihi wapinzani kuwa waungwana na wajenge hoja kwa kujibu hoja na sio kujenge hoja kwa dharau.
 
Naona kesi ya ugaidi inampleka tena Gaidi Mbowe andeleee kujibu mashtaka yake maana alionekana ana kesi ya kujibu
Who cares!!!

Yusuphu alitokea Gerezani akaapishwa Uwaziri mkuu!!

Kama hutojali, amini Freeman Aikael Mbowe ndiye PM ajaye wa NYIKANI!!!
 
Mzee #Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”[emoji848][emoji848][emoji27][emoji27][emoji3596]

MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA.

Suala la Mishahara ya Wabunge analoliongea @HecheJohn linaumiza roho sana.

Mwalimu wa Tanzania mwenye TGTS D1 mwenye mshahara take home 531,000 kwa mwezi, akifanya kazi kwa miaka 38 atalipwa shilingi 242,136,000 (milioni 242).

MBUNGE wa Tanzania kwa mwaka mmoja analipwa shilingi 240,300,000 (milioni 240 bila posho za kamati).

Yani mwalimu wa Tanzania mwenye degree analazimika kufanya kazi kwa miaka 38 ili aweze kupata malipo anayopewa mbunge wake (ANAYETAKIWA KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA TU) kwa mwaka mmoja tu. Ndio uzalendo huu?????? @SuluhuSamia

YANI IPO HIVI,
Mbunge anayelala tu bungeni @bunge_tz analipwa;

Posho za vikao kwa mwaka ni sh. 42,300,000 (milioni 42.3)
Mshahara na marupurupu kila mwezi 16,500,000 × miezi 12 = 198,000,000 (milioni 198).
Jumla kwa mwaka mmoja ni sh. 240,300,000 (milioni 240, hii haihusishi posho za kamati za kudumu).

Kwa miaka mitano, mbunge wa Tanzania analipwa 1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUCHANGANUE MALIPO YA MBUNGE VIZURI.

Sitting Allowance - 220,000
Per Diem - 250,000
Jumla kila siku mbunge analipwa 470,000/= (haijalishi ameongea au lah).
Mshahara na marupurupu kwa mwezi - 16,500,000/=

Mshahara wa mbunge kwa mwaka mmoja ni shilingi 198,000,000 (milioni 198).
Mshahara wa mbunge kwa miaka mitano ni shilingi 990,000,000 (milioni 990).
Bado kila baada ya miaka mitano huyu mbunge analipwa kiinua mgongo milioni Mia mbili (200,000,000).

Vikao vya Bunge

Kikao cha Januari 31 - Feb 10 = siku 11
Kikao cha bajeti April 4 - June 30 = siku za vikao 59
Mkutano wa tisa wa bunge mwaka 2022 Nov 1-11 = siku 10
Mkutano wa nane kuanzia Sept 13-23 = siku 10
Jumla ya siku za vikao vya bunge ni siku 90.

Siku 90 za vikao × 470,000 = 42,300,000
42,300,000 za vikao × miaka 5 = 211,500,000

JUMLA KWA MIAKA MITANO
1,201,500,000 (Bilioni moja na milioni 200) bila kuhusisha posho za kamati.

TUANGALIE MSHAHARA WA MWALIMU KWA MIAKA MITANO

Mwl. mwenye TGTS D1 mshahara wake basic ni shilingi 771,000 kwa mwezi, ukitoa makato, take home ya mwalimu huyu no shilingi 531,000.

Mshahara wa huyu mwalimu kwa mwaka 531,000 × miezi 12 = 6,372,000 mara miaka mitano = 31,860,000 (huu ni mshahara wa Mia I miwili wa mbunge).

Kwa miaka 38 mwalimu analipwa 6,372,000 * 38 = 242,136,000 (sawa na mshahara wa mwaka mmoja wa mbunge).

Huyu mwalimu akidai nyongeza ya mshahara anaambiwa "KUWA MZALENDO." Kama sio wizi huu ni nini????

Wakati mbunge wa Tanzania anaogelea kwenye bwawa la utajiri wa kodi za walala hoi, mtoto wa mtanzania maskini anashindwa kujengewa hata choo cha tundu kwenye shule yake; hata dawati la shilingi elfu 50 tu limeshindikana; hata kitabu cha elfu kumi tu imeshindikana.

IFIKE MAHALI TUACHE HUU UFALA WA KUENDELEA KUFUMBIA MACHO UDHALIMU WAKATI TUNAOUMIA NI SISI NA WATOTO WETU. MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA PALE WATU WA CHINI TUTAKAPOSIMAMA KUPINGA UDHALIMU.
 
Mzee #Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”[emoji848][emoji848][emoji27][emoji27][emoji3596]

MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA...
Pole mwalimu..ualimu ni wito!..utapata thawabu mbinguni!!
 
Mzee #Kinana anasema “wabunge wetu wanalipwa pesa kidogo sana”[emoji848][emoji848][emoji27][emoji27][emoji3596]

MISHAHARA YA WABUNGE NI WIZI NA UNYANG'ANYI WA HALI YA JUU KABISA TANZANIA...
Mwalimu achana na ualimu njoo kwenye siasa ugombee nawe uwe mbunge ulipwe zaidi ya unacholipwa sasa.
 
chadema wameshindwa kuishi kwa ustarabu nchini
Lakni nyinyi hamwezi ishi bila ya kutumia nguvu ya dola.
JamiiForums-84020155.jpg
 
Kinana aache kutisha watu nchi hii ya Tanzania aache watu waongee aache vitisho hata Samia ataondoka na wanakuja maraisi wengine
 
Naona kesi ya ugaidi inampleka tena Gaidi Mbowe andeleee kujibu mashtaka yake maana alionekana ana kesi ya kujibu
Huwa nawaelewa sana wazungu waliowekeza hapa nchini, maana wanajua wangekubali kutumia mahakama hizi za kishenzi, wangeishia kupoteza kila mashitaka. Ogopa mahakama zinazopewa maagizo na viongozi wa kisiasa walioko madarakani.
 
Back
Top Bottom