Elections 2010 Kinana: Chadema ni chama cha kibepari na kimwinyi

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Posts
10,266
Reaction score
8,085
…..Kwa upande mwingine, Kinana amedai kuwa Chadema ni chama chenye Katiba inayolinda siasa za kimwinyi na kibebari, na si siasa za kijamaa kama ambavyo DK. Slaa amekuwa akiitumia kutoa ahadi zake jukwaani.
Chadema kinaamini katika mrengo wa kulia, chama kinachoamini siasa na sera za kibepari na utakumbuka wakati kinaanzishwa waanzislishi wake walikuwa wanapinga sera za siasa za ujamaa, wakitetea sera za ubepari………..

My take to Kinana:
Kinana, ikiwa chadema ni chama cha kibepari, ninashangaa kuona kuwa ni chadema hiyo hiyo inayowapinga mabepari, mafisadi na wanyonyaji wakubwa wa nchi hii ambao wote ni wana ccm. Ni bora ya chadema ambayo imeweka wazi kufuata sera ya kibepari lakini bado inataka mgawanyio matumizi sahihi ya rasilimali za taifa.

Kwa sasa hata mwendawazimu hawezi kusema CCM si chama cha kibepari. Ni ajabu kwa graduate wa Havard kutamka maneno kama haya. Fanya utafiti wa mabepari wote na mafisadi wote wa nchi hii.

Unataka kusema watu hawa ni wanachama wa chadema, chama cha kibepari na kimwinyi?
Kinana, J. Kikwete, Salma Kikwete, Rostam Aziz, Andrew Chenge, Edward Lowasa, Nimrod Mkono Jeetu Patel Beno Ndulu, Idrisa Rashid the list goes on…
Niajabu unaona makalio sugu ya nyani na unasahau kuwa makalio ya ccm ni makaa ya moto yanayowachoma na kuwateketeza wananchi kila siku.

Kinana you are a disgrace to Havard University.
 
Mabepari hawawezi toa elimu na afya bure.
Alafu mabepari kwao ufisadi ni sehemu ya maisha.
Sasa mbona yote hayo ni kinyume na CHADEMA
 
Utopian politics!
Ukisikia MUFILISI wa kisiasa ndio kama hivi....Amegundua kuwa huwezi kuzipaka matope siasa za CHADEMA katika mambo ya ukweli, kwahiyo sasa zinaanzishwa hadithi za kitoto!...huh!
 
mi hicho nakiona kama kifo cha mfamaji tu.
 
Wakati huu ni muafaka sana wa kusikia kauli ambazo hata mtoto mdogo ambaye ufahamu wake bado ni mdogo atajua tu kuwa anayetamka hajui asemacho,kachanganyikiwa au ana msongo wa mawazo hivyo kushindwa kutawala muenendo mzima wa anayoyasema.
Siasa ya ujamaa ilikufa siku nyingi ndani ya CCM na imebaki katika makaratasi tu na katika kumbukumbu,tufike mahali sasa tuanze kuchunguza matamshi ya hawa wanasiasa maana wanapotosha jamii wakati ukweli upo wazi kwa kila mtanzania mwenye akili timamu.
 
Mabepari hawawezi toa elimu na afya bure.
Alafu mabepari kwao ufisadi ni sehemu ya maisha.
Sasa mbona yote hayo ni kinyume na CHADEMA

Afadhali kama CHADEMA wanaojipinga kama unvyodani lakini wanaahidi kutoa elimu na afya bure, kuliko CCM ambayo ni ya kijamaa lakini itenda kibepari.
 
[FONT=Times New Roman said:
Kinana you are a disgrace to Havard University.[/FONT]

Nimeipenda hii zaidi. Hivi huyu msomarl alisoma Havard ya ukweli au magumashi? Lately amekuwa akifanya vitu vya ajabu kweli kweli maskini natamani Havard wangechukua hiyo degree yao maana anaidhalilisha sana. Yaani bila aibu kweli anasema Chadema ni chama cha mabepari wakati yeye mwenyewe ni bepari nambari one? Ile meli yake iliyobeba nyara zetu kuzipeleka China imeishia wapi? Please mzee usitukumbushe machungu yetu. Na hiyo family ya kikwete inavyotumia rasilimali zetu kwa mambo binafsi sio ubepari huo? Hii nchi mmeifanya yenu na mnaweza kufanya lolote kweli. No no no please mwogopeni Mungu kama mnaamini maana kwa mwenendo I doubt kama mnaamini kuwa kuna higher power otherwise msingewaonea maskini wa Tanzania kwa style hii.
 
Yeye asema kuwa chadema ni mabepari. Sisi hiyo haituhusu. Tutaichagua chadema. Mungu tusaidie. Ccm mtabaki wenyewe mkilalama.
 
nilifikiri peke yangu nalifahamu hili.. kumbe muheshimiwa kinana naye anajuwa!.. uniform zao zinaeleza story nzima! chadema ni chama cha aina gani...
 
Kinana what a joke is, mbona hakuthubutu kusema CCM ni chama cha kijamaa, siku hizi CCM wanaona aibu hata kutaja neno ujamaa.
 
Hivi cha cha kibepari kinaweza kutoa elimu na afya bure, Chama cha kibepari hivi kinaweza kuficha ufisadi uliofanywa na serikali ya CCM. Mimi nachukulia hayo maneno kama mtu anayetapatapa
 
Kinana mwenyewe ni bepari na huyo si ndio kampuni ya meli ambayo yeye ni mdau ilishikwa na mali ya magendo na Kinanan huyu huyu si ndio nyapara wa mwana mfalme yule wa kiarabu anayemiliki Loliondo sasa nani bepari,kwanza cha kujiuliza huo utajiri alionao kinana aliupataje si kama rushwa na kushirikiana na mabepari aache hizo asije tuletea madhara kwenye nchi yetu,kwani wao wanaweza kukimbilia kwingine na wakapokewa kama wana wapotevu wanaorudi nyumbani,Kinana hana uchungu hata chembe na nchi hii kwani si anajua mambo ambayo watu wa Loliondo wanafanyiwa na rafiki yake mwarabu
 
Me nadhani kama ni ubepari basi huu wa chadema utakuwa mzuri kulingana na ilani yao ya uchaguzi, sasa Kinana anayeuponda ubepari wakati chama chake kinauishi ubepari tena negative capitalism and imperialism inayokandamiza watu masikini huku gap kati ya tajiri na masikini ikizidi kuongezeka na wakizidi kulindana si bora huu ubepari wa chadema utakaowajali masikini kwa kuwahudumia matakwa yao? Naamini kuwa akili ni nywele na huyu mwenzetu hana. Nadhani anaongea kisiasa zaidi ya kiutendaji na utekelezaji!
 
Huyu Msomali ni idiot.

Hawakilish Watanzania halisi,bali Wasomali na Al shabab politics
 
Katika Ujamaa njia kuu za uchumi (ie mabenki, viwanda, makampuni, etc)humilikiwa na umma (si watu binafsi)! Sasa huyu msomali atuambie CRDB, NBC, TANGOLD, MWANANCHI GOLD, DEEP GREEN FINANCE, MEREMETA, RICHMONDULI, DOWANS, etc vinamilikiwa na nani? Kinana is becoming 2nd Makamba!
 

Source na habari kamili ni hii hapa http://www.raiamwema.co.tz/news.php?d=2584 hicho ni kipande kidogo ulichoamua kuweka hapa...nitapigia mstari baadhi ya hoja ulizoziwacha. Whats your intake now ?

...Kinana ajibu mapigo
Mwandishi Wetu Septemba 22, 2010


KINYUME cha utamaduni wake wa muda mrefu wakati wa kampeni, Chama Cha Mapinduzi (CCM) sasa kinajibu kila hoja anayotoa mgombea Urais kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa, Raia Mwema imethibitisha.

Kwa muda mrefu sasa CCM kimekuwa chama chenye uhafidhina katika baadhi ya taratibu ambazo zimegeuzwa utamaduni, lakini sasa kinapata kazi ya ziada kujibu hoja za Dk. Slaa ambaye dhahiri anakisumbua.

Huko nyuma CCM imekuwa ikijibu hoja za wagombea urais wa Upinzani kupitia kwa wapiga debe wake lakini safari hii, imekuwa ikitumia viongozi wake rasmi kwa kazi hiyo, akiwamo Mwenyekiti wa Kampeni wa chama hicho, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

Hoja za karibuni ambazo CCM imezijibu rasmi ni pamoja na ile ambayo Dk. Slaa anasema ni kutaka kupunguza mishahara ya wabunge na mshahara wa Rais; kutangaza mpango wa kujenga reli kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam.
Katika kujibu hoja hizo, Kinana ameliambia Raia Mwema katika mahojiano na gazeti hili kuwa hoja ya kukata mishahara wabunge na Rais, haitawezesha kupata fungu kubwa la kutatua matatizo ya wananchi.

Katika mahojiano hayo yaliyochapishwa kwenye gazeti hili, Kinana anasema kama wabunge watakatwa asilimia 15 ya mishahara yao kwa idadi yao zitapatikana Sh milioni 225 ambazo hazitasaidia sana malengo ya kuinua huduma za wafanyakazi kama Dk.Slaa anavyodai.

"Sh 750,000 mara watu 300 ni unapata Sh. milioni 200 na zaidi, ni fedha ndogo sana, sijui unawezaje kuboresha mishahara ya wafanyakazi au mazingira yao kwa fedha hizo. Kwa hiyo, ni kuchukua vitu vidogo vidogo ambavyo masikio mwa wananchi vinaleta raha lakini havina tija.

"Amesema nakata mshahara wa Rais kwa asilimia 20, mimi nilifikiri anaondoa kabisa mshahara wa Rais labda angeeleweka vizuri zaidi. Rais yeyote duniani, hasa Rais wa Tanzania hana mshahara, Rais anaishi kwa marupurupu zaidi kuliko mshahara.

" Sasa anasema ataondoa asilimia 20 ya mshahara wa Rais, tuchukue kwa mfano, Rais analipwa Sh milioni 10 ina maana ataondoa Sh milioni mbili tu kwa mwezi, kwa mwaka ni Sh milioni 24. Huu ni udanganyifu," alisema.

Katika hatua nyingine, Kinana alimkingia kifua Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ambaye naye alishambuliwa na Dk. Slaa kwamba ana matumizi ya anasa.

"Anasema Spika wa Bunge anajilipa marupurupu makubwa pamoja na kujenga ofisi yake kama Mbunge wa Urambo.

"Jambo moja ambalo Watanzania hawajui na ningependa walijue ni kwamba mara baada ya haya yote yanayofanyika bungeni, mishahara anayosema mikubwa, kujenga ofisi za wabunge na kuanzisha Mfuko wa Jimbo haya ni mapendekezo ambayo yameletwa na kukubaliwa na Dk. Slaa mwenyewe.

"Kwa nini? Spika wa Bunge aliunda Tume ya watu saba kuangalia uendeshaji wa Bunge pamoja na maslahi ya wabunge, Dk. Slaa alikuwamo.

"Hiyo kamati ilikuwa na watu saba, CCM watano na wawili kutoka Kambi ya Upinzani Bungeni, ambaye ni Dk. Slaa na Hamadi Rashid Mohamed. Wamezunguka nchi mbalimbali duniani kuangalia wabunge wana maslahi gani, wana uwezo
kiasi gani, wanahuduma kiasi gani na marupurupu kiasi gani.

"Sasa Dk. Slaa na wenzake ndio waliopitisha mapendekezo haya ambayo analalamikia. Alikuwamo kwenye mapendekezo hayo yaliyopitishwa bungeni kwa ushawishi wake.

"Haiwezekani akubali hayo mapendekezo halafu arudi kwa wananchi kuwaambia kwamba hiki kinacholipwa kwa wabunge ni kibaya," alisema Kinana na kuongeza:

"Na alikuwa anapokea mshahara na hata siku moja sijasikia akikataa mshahara au kuchukua na kupeleka kwenye NGO fulani inayosaidia watu masikini. Sasa huko ni kuhadaa watu."

Akizungumzia ahadi ya Dk. Slaa kujenga reli na kununua treni yenye kasi, alisema haiwezekani kujenga na kupata treni yenye uwezo wa kutembea kwa saa tatu kati ya Mwanza na Dare es Salaam.

"Kuna treni inaitwa bullet train ya Japan ambayo kwa mwendo huu anaosema Dk. Slaa itachukua karibu saa 10.

"Kuna treni ya Kifaransa inaitwa TGV, yaani treni inayokwenda kasi sana kuliko nchi yoyote za Ulaya na kwa hesabu nilizopiga (kutoka Dar-Mwanza) inachukua zaidi ya saa sita lakini yeye amesema saa tatu. Huku ni kuhadaa watu, unajua unapokaa majukwaani si vizuri kudanganya watu na ndiyo maana nasema Kikwete (Jakaya, mgombea Urais kwa CCM) atapa kura nyingi," alisema.

Kwa upande mwingine, Kinana amedai kuwa CHADEMA ni chama chenye Katiba inayolinda siasa za kimwinyi na kibepari, na si siasa za ujamaa kama ambavyo Dk. Slaa amekuwa akiitumia kutoa ahadi zake jukwaani.

"CHADEMA kinaamini katika mrengo wa kulia, chama kinachoamini siasa na sera za kibepari na utakumbuka wakati kinaanzishwa CHADEMA na waasisi wake walikuwa wakipinga sera za siasa za ujamaa, wakitetea sera za ubepari.
"Walikuwa wakipinga serikali kumiliki mashirika ya umma au kampuni, wakisema si sawa, ni vizuri kuyaweka kwenye mikono ya watu binafsi, kutoa huduma za afya na elimu bure serikali isifanye hivyo.

"Hata ukiangalia Katiba yao ndivyo inavyosema. Inazungumza juu ya siasa za kuendeleza watu binafsi na si wananchi kwa ujumla. Sasa kauli anazotoa Dk. Slaa hadharani hazifanani na maudhui ya kimsingi yaliyoko kwenye Katiba ya CHADEMA.

"Wako karibu zaidi na vyama vya Republican (Marekani), Conservative (Uingereza) na vyama vya kimwinyi vya Uholanzi, Ujerumani na Australia, kwa hiyo wasidanganye wananchi," alisema.
 
Chama cha Kibepari ni kile kinachotumia mabango makubwa ya biashara katika kampeni. Ni kile kinachotumia mabailioni kwenye kampeni wakati wanafunzi wanakaa chini. Ni kile ambacho serikali yake inatumia magari ya milioni 200 wakati wazazi wanalala mzungu wa pili na nne kwenye wodi zao. Hivi katika dunia ya leo kuna ujamaa kweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…