masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,207
- 13,839
Nimemwona katika luninga, ITV , na kumsoma vizuri Katibu Mkuu wa CCM, juu ya rasimu mpya ya katiba na msimamo wake kichama.
Naona Kinana anajaribu kutembea katika mto wenye mawe ya utelezi, asipoangalia ataanguka yeye pamoja na chama-CCM.
Nafikiri CCM bado haijajijua kuwa iko katika awamu ya mpito kisiasa, na suala la uendeshaji wa serikali zilzomo hauwezi kuwa na muono wa miaka 50 iliyopita.
Kilichonipa wasiwasi, na mimi ni mwana CCM, ni hii nukuu ya gazeti la Nipashe, kama ilivyo katika magazeti mengi
Noashe leo 7/6/2013 uk4;
"Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakiungi mkono rasimu ya katiba mpya iliyozinduliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jumatatu wiki hii kwa asili mia mia moja.
Chama hicho kimesema wiki ijayo kitatoa msimamo wake kuhusu rasimu hiyo iliyoandaliwa na tume hiyo iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.
Kauli hiyo ya chama tawala ilitolewa jana jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu wake, bdulrahman Kinana, baada ya kuulizwa na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa chamachake juu ya rasimu mpya"
Sasa hapo ndio naona Chama kinataka kuingiza doubt juu ya kazi nzuri iliyofanywa na Kamati ile ya kisomi ya Jaji Warioba.
Kamatti ile ilikuwa na wasomi wengi na hata makada wa vyama tofauti, na nilipendezwa na msimao wao wa utaifa kwanza.
Kinana naona ana fanya attempt ya kuingiza siasa za kichama katika maoni yaliyokusanywa nchi nzima na yanayoelekea kuwa yamewakuna wengi.
Kama CCM itafanya mabadiliko makubwa katika rasimu hiyo, basi wengi tutajiuliza ni kwa manufaa ya nani na kwa ridhaa ya nani.
Hili tutajiuliza maana walioulizwa kutoa maoni yao wakati wa utayarishaji wa rasimu hiyo ni watanzania wote bila kujali itikadi za kichama.
Na dio maana nasema, hala hala Kinana, usijelikoroga, mawe hayo anayaojaribu kutembea juu yake yana utelezi mwingi.
Na asijekuta chama na yeye mwenyewe wanabebwa na maji yanayokwenda kasi ya mabadiliko ya kihistoria