Kinana Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Wilaya ya Hai

Kinana Mgeni Rasmi Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Wilaya ya Hai

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Ndugu Abdulrhamn Omar Kinana anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Hai ambao Mbunge wa Jimbo la Hai, Saashisha Mafuwe atawasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kuanzia Oktoba 2020 - 2023.

Mkutano wa CCM Wilaya ya Hai utafanyika tarehe 05 Novemba, 2023 katika Ukumbi wa Dream Park na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali.

Viongozi watakaohudhuria ni pamoja na; Dkt. Doto Biteko, Waziri wa Madini; Mhe Dr. Godwin Mollel, Naibu Waziri Afya; Mhe. Idd Kassim, Mbunge wa Msalala; Mhe. Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga; Mhe. Ng'wasi Kamani, Mbunge Viti Maalum; Mhe. Festo Sanga, Mbunge wa Makete; Mhe. Asia Halamga, Mbunge Viti Maalum; Mhe. Prescus Tarimo, Mbunge Moshi Vijijini.

WhatsApp Image 2023-08-29 at 16.09.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-08-29 at 16.09.39(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-08-29 at 16.09.39(2).jpeg
 
Back
Top Bottom