Kinana ndiye aliye karibu zaidi na Urais. Je, ndiye namba 1 ajaye?

Kinana ndiye aliye karibu zaidi na Urais. Je, ndiye namba 1 ajaye?

Tafakari yetu

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2021
Posts
1,505
Reaction score
4,427
Kila nikimtazama na kumtathmini Kanali Kinana namuona karibu zaidi na Urais kuliko mwanasiasa yeyote yule kwa sasa kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Kinana ni mpatanishi kiasili na hata Neno la Mungu kwenye Biblia linasema 'Heri walio wapatanishi maana hao watairithi nchi". Kama Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano amefanikisha pakubwa sana upatanisho wa kisiasa nchini.

2. Kinana ni mwanasiasa wa siku zote asiyechuja kwenye ulingo wa siasa. Toka nikiwa mdogo sana mpaka sasa namsikia siasani na uongozini.

3. Kinana amefika mahali asipoweza kushuka wala kushushwa labda kwa mipango ya Mungu na anaweza kupanda zaidi ya hapo. Alipanda kutoka ukatibu mkuu, umakamu Mwenyekiti na namuona akipanda kwenye uenyekiti

4. Kwa sifa na uwezo alionao naona ni msimamizi mzuri wa falsafa ya 4R za Rais Samia ambazo ni Reconciliation, Resilience, Reforms and Rebuilding na anafaa kuzipokea na kuziendeleza.

5. Kwa sifa ya kiungozi Kanali Kinana ni kama Mwalimu kwenye kujenga misingi ya muda mrefu. Baada ya kupatikana kwa katiba mpya, msingi itatakiwa kuwekwa na ni Kanali Kinana namuona hapo.

6. Kinana yupo kwenye kiwango cha juu cha umaarufu wa kisaisa na kwa sasa ukiachana na Rais Samia hakuna mwanasiasa mwingine aliyekaribia kiwango cha Kinana.

Kama una jicho la tathmini, naamini unamuona Kanali Kinana akiwa karibu zaidi na Urais kwa sasa
 
Ukigeuka kushoto unakutana na jizi la msoga, ukigeuka kulia unakutana na jangili la meno ya tembo.

Ukipiga jicho kwa mbele unaona maushungi yanapepea.

Tutakimbilia wapi? Maskini tembo wetu!!!
 
Back
Top Bottom