Kinana: Serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko

Kinana: Serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
914
* Asema Tanzania itashangaza dunia

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimeendeleza msimamo wake wa kupinga muundo wa Serikali tatu kuingizwa katika Katiba mpya, kikisema kuwa muundo huo ni hatari kwa umoja na mshikamano wa taifa.

Chama hicho kimeonya kuhusu muundo huo na kusema kuwa Serikali zaidi ya mbili zinaweza kuvuruga ustawi wa taifa, kwani ni rahisi zaidi nchi kuingia katika machafuko.

Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kinana alisema muundo wa Serikali tatu ni mzigo kwa taifa na kwamba Tanzania itakuwa nchi ya kwanza kuwa na marais watatu, jambo ambalo halipo duniani kote.

"Katiba ni jambo muhimu kwa ustawi wa nchi yetu, lakini katika hili la kuwa na Serikali tatu ni hatari, kwani kwa mujibu wa rasimu yetu ya sasa, inaonyesha kuwa kila Serikali itakuwa na mamlaka kamili.

"Ikiwa kutatokea serikali moja kati ya hizo tatu na moja ikasema sasa inanunua vifaa vya kujilinda, basi ile ya Zanzibar nayo itafanya hivyo na ile ya Muungano pia itafanya hivyo.

"Hata kama kuna vita serikali moja ikasema hatutaki nyingine itasema tunataka, mwishowe mtaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe," alisema Kinana na kuendelea:

"Kwa hali hiyo, ninachotaka kuwaambia ni kuwa Katiba Mpya itaandikwa na maisha yale yale yataendelea. Afrika Kusini, India na Kenya wamebadili katiba zao, lakini hali ya maisha ya wananchi wao iko vilevile," alisema.

Katika mkutano huo, Kinana alisema msimamo wa chama chake kuhusu muundo ni Serikali mbili na kueleza kuwa chama chake kitaheshimu maoni ya Watanzania kuhusu muundo wowote bila shinikizo la kisiasa.

Alisema hatua ya kuwa na wingi wa Serikali kuna hatari ya nchi kuwa na Bunge la Mabwenyenye na Bunge la Makabwela, ambapo alisema kuna hatari ya fedha za walipa kodi kutumika vibaya.

Kinana alionya hatua ya kuwa na ukubwa wa Serikali ambayo itakuwa mzigo kwa Watanzania, ambao wamekuwa wakiendesha kwa kulipa kodi zao.

"Hivi sasa nchi ipo katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya, ninapenda kuwahakikishia Watanzania kuwa CCM itakuwa tayari kupokea maamuzi yoyote yatakayoamuliwa na wananchi.

"…. Na ikiwa mtaamua kuwa ya Serikali mbili, tatu hata tano sawa, lakini kubwa katika hili CCM hatuhitaji mchakato huu ufanyike kwa kuingiliwa kwa shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani au hata taasisi ambazo zimejificha kwa mlango wa nyuma.

"Sisi tulisema wazi tunapenda tuendelee na Serikali mbili, lakini katika hili tambueni kuwa na Serikali nyingi zaidi kuna hatari ya kuingia katika mifarakano na hata vita," alisema Kinana.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa hatua ya baadhi ya watu kupita na kupandikiza chuki kuhusu Katiba Mpya, mawazo yao yanatakiwa kupimwa, kwani watu hao wana lengo la kuvunja badala ya kuimarisha umoja.

"Ni muhimu kuandika Katiba mpya ambayo itasaidia kuweka misingi bora na imara ya uongozi, lakini si kuwa na Katiba yenye utitiri wa kila aina ya Serikali, hili hapana, ila ikiwa mtaamua nyie wananchi wenyewe sisi hatuna pingamizi," alisema.

Mapema Agosti mwaka huu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, aliwataka wanachama wa CCM kujiandaa kisaikolojia na muundo wa Serikali tatu, ikiwa Watanzania wataamua hivyo.

Rais Kikwete alinukuliwa na vyombo vya habari kupitia vikao vya NEC mjini Dodoma, ambapo alisema mwaka 1992, kundi kubwa la wananchi lilipinga kuingia katika mfumo wa vyama vingi, lakini lilisikilizwa na nchi ikaingia kwenye mfumo huo.

Source: Gazeti Mtanzania la leo.

Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
 
Kinana unaongea wewe?Tunaitaka Tanganyika yetu usituletee habari za machafuko hapa kama huitaki Tanganyika wewe na wenzako hamieni Nchi nyingine!
 
Kinana unaongea wewe?Tunaitaka Tanganyika yetu usituletee habari za machafuko hapa kama huitaki Tanganyika wewe na wenzako hamieni Nchi nyingine!

Sema arudi nchi ya asili yake.
Nasikia somalia itazaa nchi ya somali land.
 
Hayao yake, sisi watanganyika tunaitaka tanganyika yetu.
Pia alipaswa awaelezze swasawa wananchi wa shinyanga hatari ya serikali tatu na kwanini na ni nini chanzo cha machafuko baada ya nchi kuingia katika serikali tatu. Wanaccm msije na kauli nyepesi kama hizi, mikutano hii mngekuwa mnaeleza how, why na d the concrete reasons why not serikali tatu.
 
Wasomali siku zote wanawaza fujo na vita. Watuachie watanzania tuchague tanzania tuitakayo. Mia
 
Kinana unaongea wewe?Tunaitaka Tanganyika yetu usituletee habari za machafuko hapa kama huitaki Tanganyika wewe na wenzako hamieni Nchi nyingine!

Mkuu kiukweli hata mi nashangaa sana huu msimamo wa CCM kupinga serikali tatu eti ni hatari na itasababisha machafuko. Hivi haya machafuko yatatoka wapi? Mi nadhani kung'ang'ania serikali mbili wakati wananchi wanataka serikali tatu ndo italeta machafuko maana wanalazimishwa bila kuridhia.
 
Katibu mkuu wa CCM taifa Kinana akihutubia wananchi wa shinyanga vijijini amesema CCM inaendelea na msimamo wake wa serikali mbili na kupinga muundo wa serikali tatu kuingizwa kwenye katiba mpya kwa kuwa, serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko na vile vile eti itashangaza dunia.

Source gazeti Mtanzania la leo.

Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
hawa si wale wananchi mliowatisha miaka ile kwamba vyama vya upinzani vitaleta Vita.
 
Katibu mkuu wa CCM taifa Kinana akihutubia wananchi wa shinyanga vijijini amesema CCM inaendelea na msimamo wake wa serikali mbili na kupinga muundo wa serikali tatu kuingizwa kwenye katiba mpya kwa kuwa, serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko na vile vile eti itashangaza dunia.

Source gazeti Mtanzania la leo.

Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?
Hivi wewe hujui kuwa wanaotaka serikali tatu wanalenga kuvunja Muungano, swali ni je kuvunjika kwa muungano kunaweza kuhatarisha amani kutoweka? Nadhani KINANA ana point
 
Hivi ukiwaangalia machoni au hata wale wasio na uwezo wa kukutana nao basi ukiwaona kwenye picha au gazetini:
1. Jaji Agustino Ramadhani
2. Jaji Joseph Sinde Warioba

na upande mwingine:
Abdulahaman Kinana

Unaweza kuona au kuhisi kati yao ni nani ana moral authority ya kuongelea utawala na mustakabali wa nchi kama Tanzania!?

Hivi kweli huyu katibu hajionei hata aibu kupinga swala lililopendekezwa na Watanzania chini ya uratibu wa hao wawili!?
Na nyie masisiemu mko mnamkenulie tu meno!
 
Kinana unaongea wewe?Tunaitaka Tanganyika yetu usituletee habari za machafuko hapa kama huitaki Tanganyika wewe na wenzako hamieni Nchi nyingine!

Wewe na nani mnataka Tanganyika, si mlisema Kskazini mnataka kujitenga? Nendeni huko kaskazini.
 
Anawasiwasi serikali tatu itaiwia ngumu CCM kutawala daima maana ni uwanja wa ugenini.Kama Zanzibar ina waziri wa fedha kwanini Tanganyika isiwe nae? Wakati ukuta huwezi kupigana nao.
 
Katibu mkuu wa CCM taifa Kinana akihutubia wananchi wa shinyanga vijijini amesema CCM inaendelea na msimamo wake wa serikali mbili na kupinga muundo wa serikali tatu kuingizwa kwenye katiba mpya kwa kuwa, serikali tatu ni hatari, itasababisha machafuko na vile vile eti itashangaza dunia.

Source gazeti Mtanzania la leo.

Je kuna ukweli gani katika kauli hii ya Kinana ambayo pia ndio msimamo wa CCM?

SERIKALI TATU=kusambaratika kwa Muungano?
 
Hivi wewe hujui kuwa wanaotaka serikali tatu wanalenga kuvunja Muungano, swali ni je kuvunjika kwa muungano kunaweza kuhatarisha amani kutoweka? Nadhani KINANA ana point

Sio kila jambo linalosemwa na CCM wewe unaunga mkono. kuna muda mwingine jaribu kufikiria nje ya box. Hivi hizo vurugu zitakujaje hebu fafanua
 
Acha kuongea kama umebanwa na tumbo la kuhara wewe!!...Kama mnaichukia Tanganyika kiasi hiki huku Rasilimali zake mnaendelea kuzifilisi nendeni kwa Mfadhili wenu China hakika kuna maeneo ya kutosha ya kuishi kule kwaajili ya MaCCM yote yanayoichukia Tanganyika.Mtake msitake Tanganyika yetu lazima irudi la sivyo Nchi mtaiona chungu hii.CCM hamjazoea kutikiswa hata kidogo basi sasa mjiandae kwa hilo na kitakachofuatia ni kwa MaCCM kuhudhuria kesi The Hague!!!??
 
Back
Top Bottom