Elections 2010 Kinana: Siwezi Kutamka "Asiye Sikia La Mkuu Kwenye Vyombo Vya Habari.....

Elections 2010 Kinana: Siwezi Kutamka "Asiye Sikia La Mkuu Kwenye Vyombo Vya Habari.....

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
10,827
Reaction score
4,176
Namfananisha Kinana na Waziri wa Ulinzi wa Iraq enzi za anguko la utawala wa Saddam Husein. Jamaa (muhammad Saeed al sahhaf) alikuwa anakanusha kila kitu kuhusu kuzidiwa na Wamarekani. Hata Wamarekani walipoingia Baghdad jamaa alikuwa ngangari kukanusha kuwa "hakuna kitu kama hicho, na kama wameingia basi makaburi yao yatakuwa hapahapa Baghdad". Ikafika mahali Baghdad ikatekwa, jamaa akasepa.

Jana Kinana alikuwa akihojiwa na chombo kimoja cha habari cha kimataifa. Akaona amepata wasaa wa kujenga hoja isikike nchi nzima. Kwamba JK na mama yake walitukanwa "matusi makubwa ya nguoni ambayo ni aibu kuyatamka kwenye vyombo vya habari labda unitafute baadaye kwenye simu nitakwambia".

Nilipofuatilia matusi yenyewe sikuamnini: Ati mbunge wa Temeke ametamka "Asiyefunzwa na Mamaye Atafunzwa na Ulimwengu" dhidi ya JK. Haya matusi? Vipi kauli ya Jk kuwa Watanzania waliokusanyika Mwembe Yanga wakati wa mkutano wa Dr. Slaa "ni majuha?".

Nimemkubali kinana kuwa ni mtaalamu wa propaganda, lakini mwaka huu mjomba umefulia.
 
Did you mean muhammad Saeed al sahhaf, the information minister?
 
Nasikia maneno yalikuwa zaidi ya hayo ya asiyefunzwa na mamake, fuatilia ukweli.
 
Kinana hana tofauti na ...they are no where in Baghdad, wakati vifaru vya US vinakatiza mtaani Baghdad...sijui ndo mafunzo ya kijeshi unafiki mpaka mwisho ...kwi kwi kwiiiiiiii
 
Back
Top Bottom