Elections 2010 Kinana: Wapinzani hawana jipya

Dopas

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2010
Posts
1,151
Reaction score
392
MWENYEKITI wa kampeni ya mgombea urais wa CCM, Abdulrahman Kinana juzi alisema kwamba wapinzani hawana jipya.

Alitoa kauli hiyo wakati akimnadi kwa wananchi wa Arusha mgombea ubunge wa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.

Alisema,Dk Batilda ni ‘lulu’ kwa wananchi wa jimbo hilo na hivyo wanapaswa kumpa kura zote ili awe Mbunge.

Kinana alisema,wapinzani wanazungumzia tatizo la ufisadi na ubadhirifu ambayo yameshashughulikiwa na serikali ya CCM na wao wanayarudia tu.

Kinana alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mgombea huyo wa CCM na kuwasihi wananchi wa Arusha kutofanya kosa kuiachia lulu na hazina hiyo.

Alisema, kuna watu watapita huko na kule kueleza ubaya wa mgombea wa CCM lakini nyie msidanganyike kwa maneno yao kwani kila kukicha wanazua mapya yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

“Wapinzani hawana jipya kwa sasa wasikilizeni na muwaache hapo hapo wala msiwafikirie kwani mtaumiza vichwa bure,” alisema.

Dk. Buriani aliwaomba wananchi wa Arusha wamchague yeye awe Mbunge wa jimbo la Arusha kwa sababu wana uhakika wa kuweka Jiji la Arusha katika hadhi ya kimataifa zaidi.
 
Ana kesi ya kujibu kama hiyo juu ni kweli na hali yake yaweza kuwa mbaya saana.

Ngoja USA na Uganda wapate habari. Museven atakuja ambembe sasa hivi.
 
Ni kweli wapinzani hawana jipya? Hata tukianza tu na huyu Kinana, ikithibitika kweli kuwa yupo ndani ya mianya ya ufisadi kweli tutasema wapinzani hawana jipya? Ikithibitika kuwa JK anazunguka na Helkopta inayotumia mafuta ya walipa kodi wananchi maskini wa Tanzania, wanaoambulia mlo moja kwa siku kwa bahati kweli wapinzani hawana jipya? Ikithibitika kuwa mabango, tshirts, kanga, na kofia za CCM zimetoka nje ya nchi zikikwapua mabilioni ya pesa kodi ya walalahoi ya wa Tanzania maskini, kweli wapinzani hawana jipya?
 
Kauli zingine zinajieleza mojakwa moja huda shida ya kufikiri saa.
Wapinzani kuzungumzia tatizo la ufisadi wa ccm hakuna shida kabisa kwanza wapizani ndo waliibua hilo hivo huyo.
Ki ukweli ni kwamba wanajaribu kutudisha ktk zama zile ambazo mtu haruhusiwi kusema ukweli hasa kuhusu serikali kuu.

Watanzania umefika wakati wa kuwa na uwezo wa kuwaeleza wananchi ukweli wa mambo hata kama yalifanywa na serikali fisadi!

CCM wanadai kwa kauli za wagombea wa upizani juu ya ccm, ati huenda kampeni zikiisha hawataongelesha (watakuwa maadui) wacha iwe hivo kwani upinzani nia yao ni njema kabisa.

Itafikia wakati ambapo kampeni zetu zitakuwa ni za kuambizana ukweli tupu " ccm wamefanya jambo gani linalowapa jeuri ya kutamka kuwa upinzani hawana jipya?

Hongereni upinzani (CHADEMA) kwa kuishughulisha ccm.....

UPIZANI.....WENYE UWEZO WA KUANGALIA NDANI NA NJE YA BOKSI...
 
Wapinzani hawana jipya

MWENYEKITI wa kampeni ya mgombea urais wa CCM, Abdulrahman Kinana juzi alisema kwamba wapinzani hawana jipya.

Alitoa kauli hiyo wakati akimnadi kwa wananchi wa Arusha mgombea ubunge wa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.

Alisema,Dk Batilda ni ‘lulu’ kwa wananchi wa jimbo hilo na hivyo wanapaswa kumpa kura zote ili awe Mbunge.

Kinana alisema,wapinzani wanazungumzia tatizo la ufisadi na ubadhirifu ambayo yameshashughulikiwa na serikali ya CCM na wao wanayarudia tu.

Kinana alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya mgombea huyo wa CCM na kuwasihi wananchi wa Arusha kutofanya kosa kuiachia lulu na hazina hiyo.

Alisema, kuna watu watapita huko na kule kueleza ubaya wa mgombea wa CCM lakini nyie msidanganyike kwa maneno yao kwani kila kukicha wanazua mapya yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

“Wapinzani hawana jipya kwa sasa wasikilizeni na muwaache hapo hapo wala msiwafikirie kwani mtaumiza vichwa bure,” alisema.

Dk. Buriani aliwaomba wananchi wa Arusha wamchague yeye awe Mbunge wa jimbo la Arusha kwa sababu wana uhakika wa kuweka Jiji la Arusha katika hadhi ya kimataifa zaidi.

Source:Habari Leo.
 
Watu mnaweka post heading za kuvutiiiia lakini ukiingia ndani, unakuta habari yenyewe hata haina mashiko.
 
Ni kama TV shows za msimu.Kinana usiumie kichwaaaa.Mbona wananchi tunajua.Wafa maji wanatapatapa.Viva CCM.
 
Hao wanajua kuwa KINANA KICHWA CHA CCM ndio maana wanaleta mashambulizi Binafsi.Kinana msomi wa Harvard sio kama Mbowe Form Four au mgombea mwenza wa Chadema Said Mzee MSOMI WA Darasa la saba.na muimba kwaya bwana Slaa.
 
[QUOTE=Padri;1065635]Hao wanajua kuwa KINANA KICHWA CHA CCM ndio maana wanaleta mashambulizi Binafsi.Kinana msomi wa Harvard sio kama Mbowe Form Four au mgombea mwenza wa Chadema Said Mzee MSOMI WA Darasa la saba.na muimba kwaya bwana Slaa.[/QUOTE]

Padri kweli Mbowe Form 4??????
 
Usipoteze muda wako ku-post ujinga.

Watumiaji wa JF siyo mazuzu!!!
 
Mpuuzi wewe!
 
Hao wanajua kuwa KINANA KICHWA CHA CCM ndio maana wanaleta mashambulizi Binafsi.Kinana msomi wa Harvard sio kama Mbowe Form Four au mgombea mwenza wa Chadema Said Mzee MSOMI WA Darasa la saba.na muimba kwaya bwana Slaa.

Voyeur!
 
Na kina maji marefu,elimu ya NGUMBARO na waganga wa kienyeji
 
nimetaka kushangaa iweje tumefika mchana Kinana hajatajwa wala hajaanzishiwa thread

nadhani ikifika jionikutakuwa na threads kama 5 tofauti za Kinana na kesho itakuwepo nyingine
 
nimetaka kushangaa iweje tumefika mchana Kinana hajatajwa wala hajaanzishiwa thread

nadhani ikifika jionikutakuwa na threads kama 5 tofauti za Kinana na kesho itakuwepo nyingine

Hii thread ina facts.Na hata zikipatikana posts nyingine zenye facts ni muhimu kuwekwa hapa.Hata kama ni mia per day zitawekwa.
 
we Kinana tulia usipende kuropoka we si umehojiwa juzi juzi hapa ukasema CCM isimaumiwe sana tunawachanganya wananchi au umesahau..Kama huyo Buriani ni lulu umefuata nini arusha kumpigia kamapeni ..kaaa chini uone watakachomfanya na hiyo lulu unayomuita .....hahaa Meneja wa kamapeni za rais unaenda kumpigia debe mbunge kweli maji yako shingoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…