Kindumbwendumbwe cha maisha

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
15,267
Reaction score
29,917
Ilikuwa ni siku moja Kibaha na
mimba ikatungwa sawia.

Mama akaiba redio nikimwona,
asubuhi akasema ni binti.

Picha ikaletwa kimzaha, lakini
hali ikabadilika ghafla
sana.........................


Nilikaa na wale jamaa kwa siku
tatu tu, lakini niliona mambo
ambayo binadamu
anaposimuliwa anaweza
kudhani kwamba kuna dhihaka
anayotakiwa kufanyiwa, yaani
haiwezekani.


Niliondoka Dar Es Salaam siku
ya ijumaa kwenda Tanga.

Nakumbuka ilikuwa ni August
mwaka 1995. Nilikuwa
nakwenda kwa jamaa ambaye
aliniita kwake kwenda
kumsaidia kukagua shughuli
fulani ambazo alitaka
kuzifanya.

Wakati ule nilikuwa
najitegemea, nilikuwa sijaingia
serikalini kiajira.

Nilifika mjini Tanga na kumkuta
mwenyeji wangu na mkewe
wakiwa kituo cha basi
wakinisubiri.

Tulisalimiana na
walisema wamefurahi
kunifahamu nami nilisema
nimefurahi kuwafahamu.

Ilikuwa ni mara yetu ya kwanza
kukutana. Walipewa jina na
mawasiliano yangu na jamaa
yangu mmoja.

Nilifika nao nyumbani kwao na
kukaribishwa vizuri sana.
Walikuwa wakiishi Raskazoni.


Ilikuwa ni nyumba ya kifahari
kwa kweli. Lakini nilibaini
kwamba mama au mke wa yule
mwenyeji wangu ndiye
aliyekuwa na kauli pale
nyumbani.

Kwa kipindi cha saa
moja tu tangu kufika nilipata
picha hiyo bila matatizo.


Wakati wa kula chakula cha
usiku, nilitambulishwa kwa
watu wa nyumba ile. Haikuwa
nyumba ya watu wengi.


Kulikuwa na watoto watatu wa
yule mwenyeji wangu. Mkubwa
alikuwa wa kiume aliyekuwa na
umri kama miaka tisa, wa pili
wa kike na wa tatu wa kike pia.


Halafu kulikuwa na ndugu wa
kiume wa mwanamke, kijana
ambaye alikuwa ndio kwanza
amemaliza kidato cha nne.
Halafu kulikuwa na msichana
wa kumsaidia kazi za ndani au
house girl kama wanavyoitwa.
Hawa wote nilitambulishwa
kwao hapo mezani wakati wa
kula.

Lakini wakati tunakaribia
kumaliza kula msichana
mwingine mwembamba mweusi
alikuja pale mezani na kukaa
kitini, karibu wote tulikuwa
tumeshashiba.

Alianza kujipakulia chakula bila
kusema neno. Ilikuwa inaonesha
kwamba alikuwa ametoka
kufanya kazi kwenye sehemu
yenye maji kwani gauni lake
lilikuwa na majimaji.

Nilijua ni msaidizi wa ndani
pia. Lakini niliona kwamba sio
haki kumtendea vile , yaani
kumwacha afanye kazi wakati
wengine wanakula .

lakini
sikuwa nimeenda pale kwa
sababu ya upelelezi.


Nilianza kazi yangu
iliyonipeleka pale usiku ule.
Nilipewa chumba kilicho karibu
kabisa na sebule, ilikuwa
nifanye kazi ya kupitia mafaili
kadhaa kabla sijaandika tarifa
yangu ya kuwasaidia wale
jamaa kupata walichokuwa
wanahitaji.

Naomba nisiseme ni
kazi gani hasa. Kwa hiyo
nilikuwa nimepania kufanya
kazi hadi usiku mkubwa sana
kama sio alfajiri.

Nilianza kazi
kwenye saa nne, nikimwacha
mwenyeji wangu na familia
yake hapo sebuleni, wakiangalia
televisheni. Ilipofika saa sita
usiku nilihisi kiu.

Niliamua
kuvumilia, lakini kiu ilinizidi na
niliamua kwamba ningekwenda
tu jikoni kutafuta maji ya
kunywa.

Nilitoka chumbani mwangu na
kuelekea jikoni ambako bado
kulikuwa na taa iliyokuwa
ikiwaka.

Nilipofika jikoni
nilishangaa kukuta kukiwa na
mtu. Alikuwa ni yule msichana
ambaye sikutambulishwa kwake.

Alikuwa anamalizia kuosha
vyombo ilikuwa inakimbilia
kwenye saa sita na nusu usiku.

“Pole sana, naomba maji ya
kunywa, samahani.” Yule binti
aliitika kwa kusema “sawa
baba”, huku akiinama kwa
heshima.

Aliniletea chupa ya
maji kutoka kwenye jokofu.
“Hapana, napenda ya moto,
kama yapo” nilimwambia.
Aliitikia kwamba yapo na
kunichukulia chupa mezani
hapo jikoni nilimwangalia na
kugundua kwamba alikuwa
analia.

Kwa kuwa nilishangaa wakati
ule wa kula, na hapa saa sita na
nusu za usiku mtoto wa miaka
14 au 15 anasafisha vyombo na
halafu kule kulia, nilijua
kulikuwa na jambo.

Nilimuuliza
kama analia, na alisema
hapana. Nilimwambia, ni usiku
na anatakiwa kwenda kulala.
Alisema anakwenda kulala.

Nilikuwa na uhakika alikuwa
analia na alikuwa pia
anajitahidi kufuta machozi ili
nisijua.

Kalikuwa ni kasichana
kadogo, kazuri sana pamoja na
kufujwa kule. Kama ningekuwa
kijana bado ni wazi ningeoa
msichana wa aina ile.

Bahati
mbaya zaidi ni kwamba mke
wangu alifariki miaka mitano tu
nyuma na nilikuwa bado na
maumivu. Hisia zile ziliniumiza
zaidi.


Nilirudi kule chumbani nikiwa
nimeanza kuingiwa na
wasiwasi. Lakini sio wasi wasi
tu bali hata huruma.

Kwa nini
awe yule binti, na kwa nini
sikutambulishwa kwake?
Sikupata jibu
Sikupata jibu.

Ile hali ya
kusafisha vyombo hadi saa 6:30
usiku, tena peke yake huku
akilia, ilinikera sana, na
nilijiambia siondoki pale bila
kujua kitu kuhusu binti yule.


8:30 nilisikia kama miguu ya
mtu huko sebuleni, nilihisi
kwamba angekuwa ni yule binti.
Hali hii ilinifanya niwe na hofu
kidogo, kwa sababu mawazo
yangu yalikwenda kwenye
ushirikina hasa kwa kuamini
kwangu kwamba, hapo Tanga
palikuwa na ushirikina sana.

Nilizima taa ya chumbani
mwangu pole polepole na
kuchungulia. Aliyekuwa hapo
sebuleni alikuwa ni mke wa yule
mwenyeji wangu.

Alikuwa
amevaa gauni lake la kulalia na
alikuwa anachukua kitu juu ya
kabati ya sebuleni. Nilivutiwa
kutazama zaidi.

Niliona
akichukua redio fulani ndogo
nzuri sana ambayo hata jioni ile
niliiona na kuitamani.


Bila shaka kwa shughuli za yule
mwenyeji wangu, kuwa na vitu
kama redio ya aina ile
lingekuwa ni jambo la kawaida.

Yule mama aliichukua redio ile
na kuitia kwenye mkoba wake
mkubwa wa kike na aliuweka
mkoba huo kwenye kabati
nyingine ndogo pale sebuleni.

Halafu aligeuza na kurudi
chumbani mwake.
Nilirejea chumbani mwangu
nikijiuliza ni kitu gani hicho.

Nilishindwa kujua yule mama
alitaka kuipeleka wapi ile redio,
na kwa nini aliiweka kwenye
mkoba wake, usiku kama ule.

Sikuweza kupata jibu , bila
shaka hata kama ingekuwa ni
wewe ingekuwia vigumu kupata
jibu.

Niliamua kuendelea na
kazi nyangu.
Kwenye saa kumi kamili usiku
nilisikia mtu huko sebuleni.

Nilifungua amlango wangu wa
chumba na kugundua kwamba
ni yule binti.

Alikuwa anafanya
usafi. Niliwaza. Kulala saa saba
na kuamka sa kumi alifajiri!
Lakini kwa nini iwe ni yeye tu.

Hilo likawa ndilo swali.
Niliamua kulala nikiwa
nimeumia sana.

Kwenye saa 12:30 asubuhi
nilishtushwa na kelele za kilio
cha mtu.

Mtu huyo alikuwa
akipigwa hapo sebuleni. Nilitaka
kurejea kulala, lakini ilikuwa
vigumu kwangu kutokana na
kipigo na kelele hizo.

Niliamua
kufungua mlango wa chumba
changu na kwenda sebuleni.
Yule binti wa usiku na alfajiri
ambaye nilikuwa sijajua jina
lake ndiye aliyekuwa akipigwa.

Alikuwa akipigwa na mke wa
mwenyeji wangu kwa mkanda.
Kutokana na kauli za mama yule
na yule binti mwenyewe ,
ilionekana kuwa alikuwa
akituhumiwa kuiba kitu fulani.
Mwenyeji wangu na wanaye
pamoja na yule house girl
walikuwa wakishuhudia kipigo
kile kama vile wakiangalia
sinema..

“Shangazi mimi sikuiba,siwezi
kuiba, mimi sio mwizi” Yule
binti alikuwa akilia kwa
maumivu na alikuwa amelala
chini akiwa hoi.

Yule mama aliponiona aliacha
kumpiga na aliondoka kwenda
chumbani kwake huku akisema,

“Nikija jioni nikute redio yangu,
ama marehemu mama yako
anilipe”

“Yaani mtoto kila siku wewe tu
ndio kisirani ndani ya nyumba.
Nimeshamwambia mjombako
wewe ni kibwengo na mikosi
haitaisha humu ndani……

Nilijua ni ile redio ambayo yule
mama alikuwa ameiweka
kwenye mkoba wake ambao
bado ulikuwa pale juu kabati
ndogo pale sebuleni.

Nilijua
kwamba, yule binti alikuwa
akipigwa kwa kuonewa kabisa.

Lakini ni mimi tu na yule mama
ndio tuliokuwa tunaujua ukweli
huo, halafu na mungu.

Nilimtazama yule binti pale
chini alipokuwa amelala kwa
maumivu na nilihisi tu machozi
yakinidondoka, Ingawa
nilikuwa sijajua, yule msichana
ni nani pamoja na kwamba
likuwa akimwita yule mama
shangazi, kwangu alionekana
kuwa binti mwenye adabu na
hekima pia.

Baada ya kunywa chai yule mke
wa mwenyeji wangu akiwa
hayupo , nilimuuliza yule
mwenyeji wangu kuhusu yule
binti.

Aliniambi yule binti ni
mtoto wa marehemu dada yake,
ambaye alimzaa na mwanaume
ambaye mama yake alikuwa
anadai kwamba walikutana tu
kwa bahati mbaya na hakujua
kama alipata ujauzito.

Hivyo
hakuwa na anuani yake kamili.
Huyo dada yake alifariki miaka
sita iliyopita akimuacha yule
binti na umri wa miaka minane.
‘Ndio nikamchukua, lakini
kumbe alishaharibika na kwa
kweli anatusumbua sana.

Ni
msichana ambaye hata shule
alikataa, alipomaliza tu la saba.
Na kazi yake ndio hiyo ya wizi,
kama hakuiba redio, simu, saa,
deki basi utapata kesi ya
umalaya.

Kama siyo hivyo basi umbeya
mtupu. Mtaa wote unapata
habari zinazoenda nyumba hii,
basi tu sijui inakuwaje, siju ni
laana kutoka huko kwa upande
wa baba yake…….!

Kesho pia ni Siku Tuombeana mema tuamke Salama

ulale Unono
 
Mtoa mada

ivi wale jamaa wa kijani washakulipa hela yako uliyokuwa unawadai
 
Hadhith nzur i like it!!![emoji7] [emoji7] [emoji7]
 
Daah hadith nzuri tukijaaliwa uzima inshaallah kesho panapomajaaliwa ya Allah utuendelezee hii stor
 

KINDUMBWENDUMBWE CHA
MAISHA!!! SEHEMU YA
MWISHO.....



Nilianza kuipata picha na niliojua
kwamba yule mke wa mwenyeji
wangu hakuwa akitaka yule binti
kuishi nao, kwa sababu zake.

Alikuwa akifanya mambo na
kumsingizia yule binti. Nilijiambia
kwamba siku ya kuondoka pale
ningemambia yule jamaa kuhusu ile
redio.


Lakini ingesaidia chochote?
Kesho yake jumapili nyumba nzima
ilijianda kwenda kanisani,
isipokuwa yule binti ambaye
niliambiwa kwamba anaitwa
Patience.

Huyu aliachwa kwa ajili
yakupika chakula cha familia.
Niliona bila shaka ule ungekuwa
muda mzuri kwangu kuzungumza
na binti yule.

Walipoondoka wote
nilimfuata Patience jikoni na
kumwomba nimsumbue wakati
anapika kwa kuzungumza
naye.Alisema wala simsumbui.

“Nitashukuru maan sina mtu
ninayezungumza naye humu. Wote
wananidharau hadi huyu dada
anayesaidia kazi” Alisema.

Nilimwambia ninaelewa, nimeona
na nilimpa pole. Nilimuuliza kama
ni kweli anaibana ni mbeya na
anafanya tabia chafu za kihuni.

Yule binti alibadiliaka ghafla na
kusema, “Yqaani wameshakwambia
niko hivyo, sasa mimi nimemkosea
nini mjomba na familia yake”
Akianza kulia, nilijisikia vibaya na
kujilaumu kwa kumwambia vile.

“Patience, nisikilize. Hebu
nichukulie mimi kama baba yako.
Naomba utulie unisikilize, kw
sababu siamini hata jambo moja
waliloniambia” Patience aliacha
kulia na kunitazama sana hadi
nikaogopa. “unasemaji?”

Nilijikuta
namuuliza. “hapana” alisema
akijifuta machozi.

Kwa kweli
nilipokuw nikimtizama nilishinda
kujua kama nilikuwa ninampenda,
ninamwogopa, ninamwonea aibu au
ninamfananisha.

Ili mradi tu
nilishindwa kuelewa.

Nilijisikia vibaya kuwa katika hali
hiyo, lakini sikuweza kujizuia.
“samahani, mama na wewe
mlikuwa manishi wapi kabla
hajafariki?

Nilimuuliza.
Alinitazama tena kama awali.

“Tulikuwa tunaishi Arusha” Nilitaka
kujua vitru fulani ili niamue kama
ningeweza kumsaidia kumpata baba
yake.

Lakini nilikuwa naogopa, maswali
mengine huenda yangemkera.
“Mama yako alikwambia baba yako
alikuwa anaitwa nani?” Yule binti
alishika vidole vyake na kuchezesha
miguu kwa muda kabla hajasema,
“kama jina lako” nilijua alikuwa
akinitania au alitaka kutumia
mbinu ili niondoke naye.

Ningeweza hata kufanya hilo kwa
sababu kwa maisha kama yale ni
wazi angeharibikiwa.

“Kwanza wewe unajua jina langu?”
Niliuliza kwa mzaha. “ nalijua, si
nilimsikia mjomba akisema
akimwambia shangazi,

Mr……….akija atatumia chumba cha
kwanza. Alisema na nilianza
kuingiwa na wasi wasi.

Alilotaja ni jina la ukoo, hivyo
niliona niendelee na maswali,
nikijua labda binti yule angekuwa
ni mtoto wa ndugu yangu “Jina la
kwanza na baba yako alikwambia
ni nani?”

Nilimuuliza. “Alinitajia,
nimelisahau, alikuwa akipenda
kutaja hilo la pili” Binti alisema.
Halafu alisema, “ Ninayo picha yake
alipiga na mama, mnafanana naye
kidogo. Ngoja nikaichukue .”
aliondoka na kwenda huko
chumbani kwake.

Alikuwa akilala,
kwenye kijichumba ambacho
nadhani kilikuwa hasa ni stoo
karibu na choo cha jumla cha mle
ndani.
Nilijua ni mzaha mwingine, lakini
nilitaka kumjua huyo mama na
baba yake.

Alirudi baada ya dakika
kumi, bila shaka hiyo picha
ilifichwa mbali sana.

Alinipa picha
hiyo na niliipokea kwa shauku
kubwa. Nilitegemea kumwona
ndugu yangu au mtu yeyote
ninayemfahamu.

Sikumwona yeyote
kati ya hao ninaowafahamu.
Ilikuwa ni picha ya mwanamke
ambaye nilikutana naye kwenye
semina ya maziwa, pale Shirika la


Elimu kibaha mwaka 1981.
“Germana!” Nilinong’ona. Nilihisi
nikiloa jasho mwili mzima na kwa
muda fulani sikujua hasa
nilipokuwa. Nilijikuta nikikaa
kweky kiti hapo jikoni. Ni kama
ndoto, ni ka hadithi, ni ka sinema
fulani.

Nakwambia ukweli sijawahi kuhisi
hali ile maishani na sijui kama
nitakuja kuhisi, maana nashindwa
hata kukueleza

Yule binti alinishika na kunitazama
machoni, “Unamjua mareehemu
mama?” Alniuliza na sikuweza
kumjibu.

Nilitembe na mwanamke
huyu ambaye ndio najua kwamba
ni marehemu, siku moja tu kwenye
semina ile.

Hakuna aliyekumbuka
kuchukua taaarifa kamili za
mwenzake, kwa kuzingatia kwamba
hatukuwa waajiriwa na tulikuwa
ndio tuaanza maisha, vijana
tunaochemka.

Mambo ya semina,
kutenda na kusahau.
“Kumbe Germana alizaa aliza mtoto
mzuri hivi, mtoto wangu. Damu
yangu inateswa na kudhalilishwa
hivi”.

Niliinama na kuanza kulia.
Halafu niliinua kichwa na yule binti
alikuwa akibubujikwa na machozi
pia.
“Mi-mi, mimi ni baba yako
Patience.

Nisamehe, tusa-tusamehe
sana halikuwa kosa letu……
sikuweza kuendelea.

Waliporudi kanisani walishngaa
kukuta tukiwa na Patience kule
chumbani mwangu tukiongea na
kucheka sana.

Yule mke wa
mwenyeji wangu ambaye sasa ni
shemeji yangu alimwita Patience
kwa nguvu na kisirani.

“Umeanza siyo? Unataka
kumvuruga huyo baba wa watu,
kisa?”
“Yaani wewe mtoto nitakuuwa tu,
lazima” Nilimambia Patience akae
kwanza hapo chumbani.

Nilitoka
mimi na kumfuata mke wa jamaa
yangu, “Hapana dada, ni mimi
nilimwita”
halafu nilimwita mwenyeji wangu
aliyekuwa akitokea chumbani
mwake kuja sebuleni.

Alipokuja nilimkabidhi ile picha
niliyopiga na dada yake,
alipoichukuwa aliitizama na
kunitizama, aliitizama tena na
kunitizama.

Halafu alikwenda
kukaa kwenye kochi na kushusha
pumzi kwa nguvu.
“Naomba radhi, mimi ni baba wa
mtoto Patience. Nimeamini
kilichonileta huku Tanga siyo hii
kazi yako bali ni nguvu ya damu
yangu…..Mke wamwenyeji wangu
aliingilia kati.

“Ni kitu gani?”
Niliwasimulia kila kitu.
Sitaki kukuchosha. Hivi sasa
Patience anasubiri kujiunga na
masomo chuo kikuu baada ya
kufaulu vizuri mtihani wake wa
kidato cha sita.

Amechelewa
kusoma, ndiyo, lakini anataka
kusoma na anamudu. Kumbuka
jambo moja, Kila binadamu
unayemtendea jambo baya,
unaitendea damu yako jambo baya
bila kujua.

Kila binadamu
unayemtendea jema, unaitendea
jema damu yako bila kujua.
Sisemi kwa ubaya, lakini yule mke
wa rafiki yangu alifariki mwaka
2001 kwa ugonjwa ambao inadaiwa
kwamba ni ukimwi.

Hali ya uchumi
ya mumewa inatisha sana. Tazama
naye yule mama marehemu aliacha
watoto watatu.

Je huko alipo
atajisikia vipi watoto wake leo
wakitendwa kama alivyokuwa
akimtenda Patience? Kwani
kuwapenda wengine gharama yake
ni kiasi gani?

Je sisi wanaume tuna watoto
wangapi huko nje ambao
hatuwajuiwala kuwatambua? Lakini
ni mara ngapi tunatamani na
kuwafanya watoto hao kuwa
wapenzi wetu?

Hatuoni tunafanya mapenzi na
damu zetu?




*************************MWISHO**
*************************
 
Daaah nouma sana[emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…