King Majuto ajipanga kufanya filamu mpya pamoja na Wema na Diamond

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689




Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto amesema hivi kariburi alimshawishi Wema Sepetu azungumze na mpenzi wake Diamond Platnumz ili wafanye kazi ya pamoja.


Mzee Majuto ambaye ni mshindi wa Tuzo za Watu 2014 ya filamu inayopenda, ameiambia Bongo5 kuwa amemwachia kazi hiyo Wema ili azungumzee na mzee (Diamond).

"Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwambia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja," amesema Majuto. "Mimi, Wema na Diamond, hata Diamond ninaweza kuzungumza naye sema nimeanza na Wema kwanza, akikubali mtasikia tu."

Kwa upande mwingine Majuto amesema ili acheze filamu anahitaji kulipwa shilingi milioni 3.

"Umri unaenda sasa biashara za nisaidie nisaide hakuna, kama unanitaka ili tufanye kazi unatakiwa uandae milioni 3."
 
mzee wangu anatafuna tufani tartiibu....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…