Humble African
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 4,781
- 14,415
Kwa nchi ya Egypt kama kuna Farao alieitikisa Misri akiwa hai na na kuendeleza ubabe hata akiwa mfu kaburini basi alikuwa ni mtoto mdogo aliejitwalia ufalme akiwa na miaka tisa tu kutoka kwa baba yake aliefariki then ufalme kuhamishiwa kwa mtoto wake mdogo kabisa wa kiume aliezaliwa mwaka 1325 kabla ya yesu kuzaliwa na kuzikwa mwaka 1334 aliefahamika awali kama Tutankhaten huku neno Aten likiwa na maana "the living face of sun God" Mungu ambae baba yake alikuwa akimuabudu ambapo baada ya baba yake kufariki alibadilisha jina na kuitwa tutankhamun huku neno Amun likiwa na maana "the living face of all God" na hii ni baada ya yeye kubadilisha namna ya kuabudu katika utawala wake huo ikiwemo hata kuabudu kulikopelekea na majina kubadilishwa nchini Misri kuanza kuishia na neno "Amun" ikiwa na maana "the living face of all God". Mfano "Tuta nkh Amun"
Na kwa vile aliunyaka uking akiwa na umri mdogo magenerals na washauri wake walimsaidia sana kuiongoza Misri ambayo ilikuwa himaya yenye uthabiti na ubora wa hali ya juu sana kivita, kiutawala, kidini n.k kipindi hicho ilikuwa Misri iliyoteka sehemu ya Nubia empire iliyokuwa na akiba ya dhahabu kibao walizoiba na kujiwekea Kama hazina nchini mwao Misri isitoshe hata sehemu za Mediterranean walifanikiwa kuziteka na kuzitawala. Iliwatisha wananchi kuona mtoto wa miaka tisa anaongoza taifa kubwa kama Misri kwa wakati huo Misri ikiwa yenye ushawishi Duniani ila Jenerali mkakamavu Aye alimsaidia King Tut kuiweka himaya sawa na imara bila kutetereka.
Katika kile kipindi wafalme walioana Dada na kaka ili kulinda ule ufalme usitoke nje ya koo yao hivyo hata wazazi wa king Tut walikuwa kaka na Dada kitu kilichopelekea awe na matatizo makubwa ya kiuumbaji yakifahamika kama genetical disorder ambapo alikuwa na mguu moja uliopooza, meno yasiyo na formula, hips pana kama za kike, e.t.c hakudumu muda mrefu kwenye utawala maana alitawala kwa miaka 9 pekee na baadae akafariki na sababu za kifo chake hazikufahamika wazi wazi ingawaje kuna nadharia zinasema alikufa kwa ajali ya kunagushwa na farasi wengine wanasema alikufa Kwa maralia... Ingawaje kuna kovu kichwani mwake ambalo wataalamu wa 3D Scanning wanadai alilipata baada ya kuwa ameshafariki.
Kifo chake ilikuwa mshtuko mkubwa kwa Misri maana hakuna alietegemea kama King atakufa katika umle mdogo kama ule na kwa vile hakukuwa na maandalizi yeyote muhimu juu ya kifo chake ikiwemo kuandaa kaburi lake mfalme kama inavyojulikana kipindi cha zamani watu wenye nafasi na pesa kwenye jamii walikuwa wanaandaa makaburi yao mapema kabla hawajafa ili wakifa wakazikwe humo na makaburi yalikuwa ni miamba wanachimba chini yanakuwa na vyumba vikubwa zaidi hata ya 10 na kimoja ndio kinakuwa kaburi vingine wanaweka Mali na vitu vyake atakavyoambatana navyo huko anakoenda kwenye after life kwa mujibu wa imani zao waliamini atahitaji hivyo vitu huko kwenye maisha ya baadae...mfano Yesu alipofariki kuna tajiri alijitolea kuuzika mwili wa yesu kwenye kaburi lake mwenyewe alilotakiwa kuzikwa yeye kutokana na udharula wa kifo cha Yesu. Kwa ishu ya king Tut bahati mbaya hakuandaliwa kaburi lake maana alifariki ghafla hivyo akaamriwa jamaa mmoja aliekuwa official atoe kaburi lake ili kingTut akapumzishwe.. Maana moyo ulikuwa umeanza kuharibika na kwa mujibu wa imani za Wamisiri wa kale waliamini moyo ndio kiungo muhimu sana kwa binadamu kwenda nacho kwenye after-life maana ndicho anachotumia kufikiria na kureasoan mambo na kuchakata taarifa.. ubongo kwao ulikuwa kiungo cha kawaida sana hawakuamini kama binadamu anafikiria kwa kutumia kichwa.
Ifahamike kwamba huyu mfalme mtoto alikufa kipindi ambacho Misri ilikuwa kwenye ubora wake na ilikuwa na mali nyingi sana ilizoiba Duniani kama dhahabu, almasi n.k hivyo king Tut alivyokufa akazikwa kwenye hilo kaburi huku vyumba viwili chini ya huo Mwamba wa kaburi kukijazwa Mali zisizo kifani zikiwemo kiti chake cha ufalme cha dhahabu tupu, mask yenye sura yake ya kifalme ya dhahabu, jeneza lake alilolazwamo lilikuwa la dhahabu, fimbo zake za ulemavu zaidi ya 130 zilikuwa nyingi za dhahabu, sandals zilizokuwa na sura ya maadui zake kwenye soli kama ishara ya kuwakanyaga, nyoka wake wa dhahabu na masanduku makubwa ya dhahabu tupu na Mali zingine kibao za kufuru..!
Lakini kanuni ya wafalme wa Misri ya kale walikuwa wakifa wanazikwa kwenye mapyramid makubwa na kukaushwa ili miili yao isioze ndio maana hata Firauni hadi Leo bado mwili wake upo Duniani...King Tut nae alipitia katika mchakato huu unaoitwa Mummy Kwa kiingereza na Mumiani kwa kiswahili... Je Mumian ni nani?
Mumiani (Mummy)
Mumiani ni maiti ya binadamu au mnyama ambaye ngozi na viungo vyake vimehifadhiwa kwa kutiwa dawa ya kutoozesha. Mumiani hufungwa kwa bendeji kutoka kichwani hadi vidole vya miguu na kuwekwa kwenye majeneza ya jiwe hekaluni au piramidi. Kama ni mafarao, kabla ya kuzikwa, wao hufungwa kwa uchawi na mganga mkuu ili kuondoa au kulaani yeyote anayemsumbua farao katika usingizi wake wa milele. Wakati kaburi la farao ambalo limepovurugwa (mara nyingi na wanaakiolojia na wezi wa makaburi) linaweza kuamsha mumiani ambayo haiwezi kupumzishwa mpaka laana ivunjwe, kwa kawaida kwa kusoma maandishi yaliyochongwa upande wa jeneza la jiwe au kuta za kaburi, au hata hati ya kukunja yaliyo na kivunja-laana. Wasiposimamishwa, mumiani watatembea Duniani milele, wakiweka laana kwa yeyote ambaye apitie njia yao, na kuwageuza kuwa wanasesere wa vuudu au vifaa vingine vidogo..Hao ndio Mumiani jinsi walivyo.
Sasa miongoni mwa vitu vilivyomfanya Mumiani king Tut awe maarufu ni kungunduliwa na kwa eneo kaburi lake lilipokuwa kwenye eneo la valley of Kings baada ya miaka 3400 kuwa imepita huku mwili wake ukiwa bado Katika hali hali nzuri ya kutambulika kirahisi bila uharibufu mkubwa. Iligharimu safari ngumu ya miaka zaidi ya 3000 kwa "tomb raiders" wale kule Misri kulisaka kaburi la King Tut ili wabomoe na kuiba mali zilizomo ndani ya kaburi...walihenya kutafuta kaburi la Dogo huyu kwa udi na uvumba ili waibe Mali kwa miaka na miaka bila mafanikio..sababu ya kulikosa inaelezwa ilikuwa ni viapo na makafara makali yaliyopigwa kwenye lile kaburi la King vilivyoaminika kulipoteza kimazingara ili lisionekane kwa macho ya kawaida na pia kwa vile hakuzikwa kwenye makaburi official ya wafalme hivyo Haikuwa rahisi kumpata maana alizikwa kwenye kaburi la mtu wa kawaida tu.
Na pia licha ya corridor ya yale makaburi kuandikwa maandishi yenye biti kali na la kutisha la uchawi mkuu na laana kuu kwa atakaethubutu kumsumbua mfalme Mumiani King Tut Katika usingizi wake wa milele bado wazungu hawakuogopa wala kutaka kushindwa kumsakua King Tut...nanukuu kakipande haka kanasema;
"Curse be those who disturb the rest of a Pharaoh. They that shall break the seal of this tomb shall meet death by a disease that no doctor can diagnose”. Ilisomeka hivi kwenye upande mbili za korido la kuelekea kwenye jeneza la alikolala King Tut.
Wazungu sio wa kushindwa kirahisi rahisi mwaka 1922 mwanaikokolojia Howard Carter na Lord Carnarvon waligundua hili kaburi lililotafutwa kwa miaka zaidi ya 3000 na wakadharau biti zote na kuanza kazi mara moja ya kuingia kwenye chumba alikolala King Tut. Howard akiwa mtaalamu wa ikolojia(Archeology) na Lord Carnarvon aliekuwa anafadhili mradi mzima na akiwa msaka fedha anaetaka kukwapua hazina za king Tut tofauti na Howard yeye alikuwa na dhamiri ya dhati ya kutafiti maisha ya King na kuifahamisha Dunia juu ya historia adhimu ya "Boy King" huyu Tut.
Hapa ndipo sekeseke lilipoanzia na kumfanya king Tut awe mashuhuri na kaburi lake kuogopwa Duniani na kutoa funzo kwa wale vichwa ngumu wasio sikia sambamba na wezi wenye tamaa mbaya ya mali wasizozijua chanzo chake. Na hatimae kuhasisiwa kwa muvi na vitabu vikielezea scenario inayoitwa "The curse of king Tut" kwa kiswahili "laana ya mfalme Tut "
Mapema tu baada ya kuvunja kaburi na kuzama ndani kuanza utafiti mwaka 1922 swahiba wa karibu alie fadhili mradi mzima tajiri sana Muingereza huyu Lord Carnarvon alifungua dimba la kukumbwa na laana Kali ya King Tut kwa mbwa wake aliekuwa England kuuwawa kwa kung'atwa na nyoka aina ya Cobra ambae kiutawala wa kifarao alikuwa ndio ishara ya ulinzi wa Mali zote za kifalme kiroho na kimwili..habari zilipofika Misri watu wakajua kazi imeanza na laana ya ile kaburi imeanza kazi sababu cobra ndio kafungua dimba la kazi.
Then miezi saba tu baadae Lord Carnarvon mhusika mkuu mwenyewe, kadhia ya laana ya king Tut ikamkumba akiwa bado Misri akang'atwa na mbu shavuni na ghafla umeme kukatika mtaa mzima na kuachiwa kidonda ambacho King Tut pia alikuwa nacho pale pale shavuni alipong'atwa Carnarvon wakati wa uhai wake king Tut, imagine mbu akung'ate upate pneumonia (Limonia) na pia yule mbu alikuwa na sumu aina arsenic.. Sumu ambayo a.k.a yake ni king poison Kwa sababu Kings wengi maarufu Duniani waliitumia kujiua nayo, hivyo ishara mbili kuu kubwa zikajitokeza kuashiria kazi ya laana ya kaburi la King Tut imeanza rasmi.. Kwa matukio haya mawili, Mbwa kipenzi wa Carnarvon kung'atwa na cobra kisha kufariki na mbu kupachika sumu ya arsenic kwenye mwili wa lord Carnarvon na kumsabishia kifo. Kuliashiria kazi ilianza rasmi.
Baada ya hapo mdogo wake na mdhamini mkuu wa show Carnarvon akifahamika kama Audrey Herbert aliefariki kifo cha maajabu bila ya kuwa na tatizo kubwa la kiafya bali punde baada ya kaka yake kufungua lile kaburi la King Tut akapata upofu..madaktari wakahisi labda ni meno yale yaliyoanza kuoza kwa kasi ndio yamemsababishia hayo yote wakayang'oa yote akawa kibogoyo then baadae na yeye damu yake ikakutwa ina sumu kimaajabu ajabu tu..akachukua round akafariki na yeye miezi mitano baada ya kaka yake kwa mateso makali. Taharuki ikazidi kupanda Duniani magazeti makubwa Duniani yakaripoti tukio la "king Tut curse"
Aaron amber huyu yeye ni mtaalamu wa masuala ya Misri ambae yeye hakufanya hii kazi moja kwa moja ila yeye alikuwa ana kazi ya kuandika tukio zima kwenye kitabu chake kilichoitwa "Egyptian book of the dead" hivyo alikuwa na urafiki na watu takrbini wote walioshiriki tukio zima la kubomoa kaburi la king Tut na zaidi alikuwa best friend wa Lord Carnarvon ambae ndie alikuwa financier na yeye aliekufa kimaajabu tu. Baada ya nyumba yake kuwaka moto akajikuta anang'ang'ana kukiokoa kitabu kile alichokuwa amekaribia kukimaliza kukiandika lakini yeye na kitabu wakawaka moto hadi wakiwa majivu. Maajabu haya!
Sir Bruce Ingham, kitu cha kufurahisha ni kwamba huyu jamaa hakuhusika moja kwa moja na kumsumbua King Tut huko kaburini kwake.. Yeye "aliambukizwa" tu hii laana na rafiki yake Howard Carter ambae alimpa zawadi ya "bracelet" urembo wa kuvaa mkononi alioutoa huko kaburini kwa king Tut ukiwa umeandikwa kwa kimisri cha kale "Curse be to those who move my body" ikimaanisha "laana iwe juu ya wote watakougusa mwili wangu." Siku chache baada ya Bruce kupokea ile zawadi nyumba yake iliungua yote na walipojaribu kujenga tena ikapitiwa na mafuriko na kuua.
Hugh Evelyn White alikuwa mwanaikolojia ambae yeye kazi yake ilikuwa ni director mkuu wa wale wachimbaji wa lile kaburi kwa njia ya excavation..yeye hakuweza kumudu uzito wa ile laana ya kifo na alikuwa anasema kwa miaka mingi kuna sauti ilikuwa inamuijia kichwani ikimuamuru ajiue mwenyewe haraka...hakusita akatekeleza maagizo kwa kujinyonga na kufariki. Akiacha kipande cha Ujumbe kikisema "I have succumbed to a curse which forces me to disappear" ukisema nimefwonzwa na laana ambayo inanilazimu kupotea" ni kipindi hicho hicho team nzima ya excavations unity iliparaganyika wakapukutika kama majani ya mti mkavu wakati wa kiangazi. Hadi mwaka kuanzia mwaka 1922 hadi 1929 team ilipukutika na aliefanikiwa kutoboa hadi 1930 alikuwa Howard Carter mwenyewe tu.
Howard Carter huyu alikuwa starring wa hii Muvi ndie aliekuwa mtafiti na mgunduzi mkuu wa kaburi la King Tut mwenye akili, ujanja na uzoefu wa haya masuala haya ya kifarao, laana zao na namna ya kuhandle Mali zao. jamaa hakudharau suala la makafara na kuwaona waganga na wachawi wakuu wampe mafusho ili apunguze nguvu ya yale malaana, kimsimgi hii Haikuwa kazi yake ya kwanza anayajua yanayotekeaga wale mafirauni wa kifarao wakitibuliwa wanatibuka kweli ila Lord Carnarvon yeye aliongozwa na tamaa ya Mali ya kutaka ubwete wa kuchukua hazina za mafarao akajua atapitia mzigo kwa ubua tu...hakujua msako wa hawa mafarao.... Kwa upande wa Carter hakuwahi kupata magonjwa ya kushtukiza wala majanga ya moto wa mafuriko wala ndugu zake kukumbwa na magumu ya laana ya King Tut.. Maana yeye alijua kuchanga karata zake vizuri na namna ya kuzipoza hizi roho Korofi za laana na Hakuwa na lengo la kuiba Mali za mafarao bali haliipenda kwa dhati historia na ustaarabu wa Misri ya kale na alitaka Dunia nzima ione kilichojiri Misri hivyo hii ilimfanya asie adui mkubwa na mhanga wa laana. Ilimtokea kuna kipindi alikuja mtu ambae ni wa kimaajabu ambae hakumuona wala kumkariri akagonga mlango kisha akampa kipande cha karatasi na kutoweka kimazingara kipande kikiwa na Maandishi yanayosomeka " May your spirit live, may you spend milion of years, you who love Thebes, sitting with your face to the north wind, your eyes beholding happiness " tokea mwaka 1922 hadi mwaka 1939 akiwa na miaka 64 ndio akafariki kwa cancer ya kawaida isiyo na chembe ya laana ndani yake. Na hayo maandishi ya kwenye kikaratasi yamewekwa kwenye kaburi lake alimozikwa Howard Carter.
Naam, Mafarao wana mengi sana ya kuzungumzia ikiwemo ishu ya Firauni ambayo inachanganya watu huku wengine wakiamini Mungu alimfanya Farao asioze hili vizazi vyote vimshuhudie na wengine wanaamini alikaushwa kwa njia ya Mumian(mummy) kama utamaduni wa Misri unavyoelekeza...Mimi sijui? Ninachofahamu Misri ina mengi sana ya kuzungumziwa ya kusisimua na kufundisha.
kwa Leo yangu ni hayo. Enjoy!
Kisses and hugs! [emoji176]