Kinga za malaria zipo nyingi sana zinazotolewa kwenye hospitali zetu, labda uwe 'specific' we unaongelea kinga wa aina gani na ni nchi gani umeona.
Kuna program ya kutoa vyandarua kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga kwa 'Hati Punguzo' kujikinga na malaria, kuna dawa za SP zinatolewa kwa kina mama wajawazito hata kama hawaumwi malaria (IPTp) katika miezi 3 -4 na 6 -7 ya mimba kwa ajili ya kujikinga na malaria, kuna utafiti unaendelea Mtwara sasa juu ya huduma kama hiyo ya SP kwa kina mama wajawazito kwa watoto wachanga (IPTi), kuna tafiti zinaendelea Bagamayo juu ya chanjo ya kuzuia malaria, Kuna elimu ya afya inatolewa mahospitalini jinsi ya kujikinga na malaria etc..
We unataka/unaongelea ipi?