Kesi ya ugaidi dhidi ya Mbowe imeweka wazi jinsi ndani ya Polisi kulivyo na magenge ya uharamia, ambayo kazi yale ni kuteka, kutesa na kubambikia watu kesi.
Hata kabla ya kukamilika kwa kesi hii, na hukumu kutolewa, kuna mambo kadhaa yaliyo dhahiri:
1) Ndani ya jeshi la polisi, kama ilivyokuwa kule Zambia, kuna polisi walio wema ambao hawakubaliani na matendo maovu ya wakubwa zao dhidi ya raia wasio na kosa.
2) Ndani ya jeshi la Polisi, kuna genge la ugaidi ambalo kazi yake ni kuteka, kutesa na kubambikia watu kesi ili kuitisha jamii isiwe huru katika kukosoa, kutetea na kudai mambo wanayoamini kuwa ni haki yao. Kundi hili, kimsingi, ni genge la maharamia ndani ya Jeshi la Polisi, ambalo lipo ndani ya jeshi la polisi kwa lengo la kutumika na wanasiasa kufanya uhalifu dhidi ya ubinadamu. Genge hili kwa kiasi kikubwa linajumuisha baadhi ya makamanda wa polisi katika ngazi mbalimbali, na lipo karibu na watawala na chama tawala. Genge hili linatumika kuzima zinazoitwa chokochoko dhidi ya watawala.
3) Watawala wameligeuza jeshi la polisi kuwa kundi la kulinda nafasi zao kwa njia zozote, haramu na za kawaida. Na hapa ndiyo chanzo cha zile kauli za polisi, "maelekezo kutoka juu"
4) Uonevu dhidi ya Mbowe, umekuwa na faida kuliko hasara. Sasa wananchi wengi wametambua kuwa Polisi, kwa kiasi kikubwa, wamekuwa sehemu ya makundi ya kihalifu ambayo raia mwema anastahili kujihadhari nayo kadiri anavyoweza.
5) Uhalifu wa polisi, ni mgumu sana kuukwepa kwa sababu umehalalishwa na mfumo wa utawala. Ni uovu unaolindwa na sheria na watawala.
Tanzania ilipambana kumwondoa mkoloni, lakini baada ya kumwondoa mkoloni, ipo chini ya ukoloni ulio mbaya zaidi wa mtanzania mweusi mwenzie. Wanaotenda uovu siyo kwamba hawajui, bali wanaamini kwa kuwatisha wanaokosoa, wanaodai haki na mifumo ya kudhibi watawala, wao watakuwa huru kutawala milele, watakuwa huru kufanya chochote wakati wowote kwa yeyote na kwa namna yoyote watakayo bila ya kuhojiwa na yeyote. WATANZANIA KWA UMOJA WETU TUKATAE KUTAWALA KAMA PUNDA, LAZIMA TUPATE KATIBA MPYA ILI KIONGOZI APEWE MIPAKA YA MAMLAKA YAKE.
KATIBA MPYA, WAPENDE WASIPENDE, TUIPIGANIE MPAKA TUPATE. Kama wazee wetu, tena nyakati zisizo na tekinolojia waliweza kuushinda ukoloni, kwa nini sisi leo tushindwe kuushinda ugandamizaji wa watanzania wenzetu dhidi yetu?
Mateso ya Mbowe, yapande mbegu na yakawe chachu ya kudai mfumo bora zaidi wa kiutawala.
Pongezi nyingi kwa polisi, hasa wa ngazi ya chini, wanaoudhiwa na kusikitishwa na amri wanazopewa na wakubwa zao ambao ni maharamia. Yale mema wanayowatendea watanzania wenzao wasio na hatia wanapokuwa kwenye serlo za polisi, wasidhani yanapotea, yanaishi, na kuna siku yatazaa matunda; na yale maovubyanayotendwa na polisi maharamia, kuna siku yatapata adhabu istahiliyo.
Mungu uliye mkuu wa haki, tunakuomba uendelee kuuanika uovu wote wa polisi na wanasiasa maharamia, na wakati ukifika, mkono wako ukatende dhidi yao kwa namna istahilivyo na kwa hekima yako.