Kingamuzi cha Cannal plus

Kingamuzi cha Cannal plus

Ziyech04

Member
Joined
Jun 24, 2021
Posts
10
Reaction score
7
Wadau kwa anaefahamu nawezaje kupata kingamuzi cha cannal hapa Tz na gharama zake za malipo huwa ni shi ngap
 
masafi na Ziyech04 mimi mtaa ninaoishi kuna jamaa anadeal na hizo ishu na kusupply huduma ya tv cable.

Nikahama ule mtaa (mkoa) so ikanibidi nimtafute kumuuliza kama naweza pata king'amuzi cha canal akajibu ving'amuzi vipo, vipya kwenye boksi, gharama ni 150K (kinakuja na kifurushi cha mwezi) na malipo ni 45K kwa mwezi.

Nikamuuliza nitalipaje na kinakua subscribed nchi za kifaransa? Akajibu haina shida pesa hua anatumiwa yeye za wote wenye ving'amuzi hivyo na walio chini yake yeye anaforward kwa jamaa yake yuko Burundi.

Akanielezea pia ya kwamba anakuuzia decoder pekee na hiyo decoder inatumia ungo wowote wa Startimes au dstv. Nikamuuliza nainstall vipi akajibu kwamba ni maelezo ya kawaida mfunga ving'amuzi yeyote anaweza kuinstall.

So far hicho ndicho ninaweza waambia. Ila sitatoa mawasiliano yake kivyovyote vile ili yasije maswala ya kuanzishiana nyuzi za utapeli.
 
Back
Top Bottom