Kingolwira Morogoro

kwa speed ya treni inawezekana, lakini bahati mbaya tatizo letu watz speed sio kigezo wala tatizo... usimamizi wake ndio utaashangaa na wala hautaamini macho yako...
rejea mradi wa mwendokasi.
Sahihi kabisaa hao hao Trc ni mwaka 2013 na 2015 waliletewa vichwa vipya kabisa vya treni kutoka marekani katika kampuni ya Electromotive Diesel (EMD) ni vya kisasa kabisa ila kavitazame leo.

Pia serekali yetu ilinunua mabehewa mapya ya abiria toka Korea kusini bila shaka 2015 ambayo Leo hii wanayatumia katika treni yao wanaiita deluxe yatazame leo hii yalivyo.

Yani huwa inaniumiza na kunisikitisha sana huwa kutunza hatuwezi kabisa ni kuharibu tu.

Rejea pia reli ya TAZARA ilikuwa na system za kisasa kabisa katika kuongozea treni nyakati hizo ila leo pia angalia kama Kuna hata signaling light moja inafanya kazi tunachojua ni kuharibu haribu tu na kurudishana nyuma.

INAUDHI SANA hivi vichwa sijui vina tatizo gani.
 
Nampenda mama yetu ila sina Imani naye sababu hana muelekeo
 


Serikali Inasema Mpaka Mwezi Wa Nne 2022 Ndiyo Treni Itaanza Safari Kwa Majaribio Dar Es Salaam ~Morogoro

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…