Kingwendu kuwa Mheshimiwa Mbunge

maatope

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2013
Posts
1,422
Reaction score
957


Msaani maarufu wa Maigizo Nchini aitwaye Rashid Mwinshehe maarufu Kama "Kingwendu", amesema anajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ambacho amedai Kuwa anaona Kinapendwa na Watanzania wengi bila ya Kutaja Jina la Chama hicho wala Jimbo atakalogombea.

Wataalamu wa Masuala ya Kisiasa Nchini, wameitafsiri Kauli hiyo ya Kingwendu Kwa Mitazamo tofauti, huku Wengi Kati yao Wakisema Kuwa Upinzani Una Nguvu Kubwa hivi sasa hapa Nchini, hivyo Sio ajabu Kwamba yawezekana Msanii huyu amevutiwa na Kuamua Kujiunga na Chama fulani Cha Upinzani Ili aendeshe harakati za Ukombozi wa Taifa hili.

Akizungumza na Mwandishi wa Tanzania Daima, Kingwendu alisema, "Ninajiandaa Kugombea Ubunge 2015 Kupitia Chama ninachoona Kinapendwa na Watanzania wengi Kwenye Jimbo ambalo ntalitaja hapo baadae Wakati Utakapofika, Bado ninafanya Mazungumzo na Washauri wangu wa Karibu Kuhusiana na Swala, nadhani ntaliweka Wazi muda Ukifika..."Zaidi nawatakia Watanzania Kila la Kheri Katika harakati hizi".


Kila la kheri Ngwendulile kwani wao waweze wana nini na wewe ushindwe una nini? heno heno
 
Nimecheka sana! Huyu akigombea jimbo la watu wenye stress anapata!
 
Mmekosa picha muafaka ya kuambatisha na hiyo habari ?..coz hiyo picha haifanani ra ujumbe.
 
He he he kuna nini mjengoni kila mtu anakimbilia
 
Duh!muheshimiwa kingwendu huku muheshimiwa kigangwala watamchanganya muheshimiwa speaker.
 
Ntakua Nachekaaa tuuu akiwa bungeni...
hapa zenji tulikuwa na mwakilishi wa aina hiyo marehemu Fadau,huyo ilikuwa mwisho wa shida ikifika zamu yake kuchangia hoja baraza la wa wakilishi!
 
He he he kuna nini mjengoni kila mtu anakimbilia

Ukiachana na unono wa salary, kuna kitu inaitwa KAMATI....we acha tu, yaani mnaandika tu proposal kwa madame, mnapewa fungu a.k.a Fuba then mnazunguka nchi moja baada ya nyingine kama Pilot wa KLM....ila kama wewe ni SHE unaweza kukatizwa a.k.a kupigishwa U turn na chairman anytime....me mwenyewe naangalia upenyo ukipatikana tu naanza mchakato...

Pambana Kingwendu baba, Kasungura ni kadogo na usipokaa front row huambulii hata kucha zake.
 
Biashara ya siasa inalipa sana...ngoja nitafute mtaji nami niwekeze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…