orturoo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2017
- 2,947
- 4,876
Vimelea kutoka kwa kinyesi cha binadamu na nguo zilizoharibika za Hello Kitty zilipatikana kwenye mifuko ya takataka iliyobebwa na puto za Korea Kaskazini hadi Korea Kusini, maafisa wanasema.
Mamia ya puto za kubebea taka zimetolewa na Pyongyang kuvuka mpaka katika wiki chache zilizopita, kulipiza kisasi kwa kampeni ya vipeperushi iliyotumwa kaskazini na wapinzani wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Kong Un.
Uchambuzi wa baadhi ya vifurushi vya puto uligundua kuwa vilikuwa na udongo ambamo "minyoo " waligunduliwa kuwa ndani. Uwezekano wa maambukizi kutoka kwa vifurushi nimdogo, wizara ya muungano ya Korea Kusini ilisema.
Korea Kaskazini inasema puto hizo ni kulipiza kisasi kwa kampeni ya propaganda inayokosoa utawala huo.
Vitu vilivyobebwa na puto pia vilijumuisha nguo za nchi za "magharibi" zilizokatwa ambazo zilikuwa zimetolewa kutoka Kusini. Nguo hizo zilikuwa na wahusika wa katuni kama vile Mickey Mouse, Winnie the Pooh, na Hello Kitty, kulingana na Reuters, pamoja na soksi na nguo za watoto zilizo na viraka vingi.
Uchafu uliotumwa na Korea Kaskazini pia ulifichua hali mbaya ya kiuchumi ya nchi hiyo, na kuangazia "msimamo wa kihasama dhidi ya Korea Kusini", afisa wa wizara alisema.
Chanzo: BBC
Pia soma
- Korea Kaskazini Yatuma Puto Zenye Taka na Kinyesi Kuvuka Mpaka wa Korea Kusini Kama "Zawadi za Uaminifu"