Kinyume na kifungu cha 47 (a); jaji warioba kupewa dak 60 tu kuwasilisha rasimu ya katiba Bungeni!

Twilumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2010
Posts
12,576
Reaction score
14,522
Wakuu nimeikuta hii kwenye facebook page ya bwana Julius Mtatiro, nimeona tuilete kama nilivyoikuta

Julius S. Mtatiro

KUMPA JAJI WARIOBA DAKIKA 60 ILI AWASILISHE RASIMU YA KATIBA NI JAMBO LISILO HAKI, NI KINYUME KABISA NA KANUNI ZA
BUNGE TULIZOPITISHA NA NI KULIBURUZA BUNGE MAALUM LA KATIBA

Kanuni ya 47(a) ya bunge maalum la katiba inaeleza kuwa "Mwenyekiti(wa bunge maalum la katiba) baada ya kushauriana na
Mwenyekiti wa Tume(ya mabadiliko ya katiba) watapanga muda unaofaa kwa ajili ya Mwenyekiti wa Tume(ya mabadiliko ya katiba)
kuwasilisha Rasimu ya Katiba katika Bunge Maalum"

Jambo la ajabu ni kuwa, jana jumamosi, mhe. Samweli Sitta(namheshimu sana) ametangaza kuwa, siku ya kesho jumatatu jioni
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ATAWASILISHA RASIMU KWA MUDA USIOZIDI DAKIKA 60.
Taarifa za uhakika tulizonazo ni kuwa, mwenyekiti wetu wa Bunge Maalum(Mhe. Samwel Sitta) hajawasiliana na Mwenyekiti wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba ili kupanga muda kama kanuni inavyoelekeza.

Ikumbukwe kuwa, tume ya mabadiliko ya katiba imefanya kazi kubwa sana kwa miezi zaidi ya 20. Kazi hiyo inahitimishwa kesho
jumatatu tarehe 17 Machi 2014 saa 10.00 jioni ambapo Jaji Joseph Sinde Warioba ataiwasilisha rasimu na kuielezea ndani ya bunge
maalum.

Ikiwa Jaji Warioba anapewa dakika 60 tu kuelezea kwa kina rasimu SURA 17, IBARA 271 na KURASA 148. Jambo hili haliwezekani na
halikubaliki hata kidogo. Kwa maoni yangu, Kazi iliyofanywa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa miezi 20 haiwezi kuwasilishwa
bungeni kwa dakika 60 au saa moja.

Bunge maalum la katiba limetumia wiki tatu kutengeneza kanuni, linatumia siku 3 kwa wajumbe kuapa, ETI BUNGE HILO HILO HALINA
SAA 5 au DKK 300 kwa ajili ya KUMSIKILIZA JAJI WARIOBA! Binafsi napata wasiwasi mkubwa sana ikiwa tutakwenda mbele namna hii.
Nchi ya Ghana ilipokuwa katika hatua hii, bunge lao la katiba lilitenga siku mbili (2) kwa ajili ya kuisikiliza tume ya katiba ikiwasilisha
rasimu ya katiba, sie hatuna hata siku moja kwa ajili hiyo? Mungu wangu, nchi hii tuna matatizo gani?

Mhe. Samwel Sitta ameaminiwa na wajumbe wengi wa Bunge Maalum nikiwemo mimi, na nadhani watanzania wengi wana imani naye
katika kusimamia suala hili, ASIANZE KUJISAHAU NA KUFANYA VITENDO AMBAVYO VITAFANYA TUTILIE MASHAKA NIA YAKE.
Kiongozi mzuri ni yule anayetenda kulingana na makubaliano na anayetenda kwa nia safi ambayo inaaminiwa na anawaongoza kuwa
nia hiyo kweli ni safi.

Hoja kubwa aliyoitumia katika kufanya uamuzi huo ni kwamba, KWA TARATIBU ZA MABUNGE, HOJA YOYOTE HUWASILISHWA TU BILA
UFAFANUZI. Mimi sikubaliani na mtizamo huu. Najua anarejea utamaduni na utaratibu wa mabunge ya kawaida ya kupitisha sera,
sheria, bajeti n.k. Na huwa tunaona mawaziri wanavyoweka hoja zao mezani bila ufafanuzi mkubwa kisha hujadiliwa.

Utaratibu wa mabunge ya kawaida ni tofauti kabisa na bunge maalum la kujadili na kurekebisha na kupitisha katiba. Bunge lolote la
katiba linahitaji muda wa kutosha kuisikiliza tume iliyoandaa rasimu ya katiba, kwa sababu uwasilishaji wa rasimu ya katiba ni mpana
kuliko kuwasilisha hoja ya bunge la kawaida.

Nasema tena, jambo hili halikubaliki na litatufanya tuanze kutoaminiana mapema sana. Nadhani tume ya jaji Warioba inastahili muda
wa zaidi ya saa 4 au walau nusu siku, ili kuwasilisha ufafanuzi wa rasimu husika.

Wabunge wengi wa CCM wana hofu kubwa na Jaji Warioba, na kuna baadhi yao hadi wanasema ingewezekana ni bora angeileta tu
bungeni na kuikabidhi kisha akaondoka zake(wanasema waziwazi). Hofu hii inatokana na mapendekezo mengi mazuri ambayo
wanadhani yataathiri MITIZAMO YA CCM.

Ushauri wangu wa BURE kwa wajumbe kutoka CCM ni kwamba, KATAA NENO USIKATAE WITO. Ni muhimu wakawa wavumilivu na
kumsikiliza Jaji Warioba kwa muda wa kutosha na kisha baada ya hapo wajipange kutimiza azma yao ya kupinga mapendekezo ya
tume ya jaji huyu. Ni vema Jaji Warioba asikilizwe ana wito gani, kwa ufasaha mkubwa, kisha kama CCM wanaweza wakatae
anayosema, hakuna haja ya KUMTENGEA SAA MOJA ILI AKOSE MUDA WA KUTOSHA KUONGEA na wajumbe wa bunge maalum na
watanzania wote kwa ujumla.

Mzee wangu Samwel Sitta asijiamini sana katika uamuzi huu, asianze kuburuzwa na Machungu ya CCM dhidi ya WARIOBA na TUME
yake, asikubali KUBURUZWA wala KUTUMIKA kwani atawavunja moyo wananchi na wajumbe wengi wenye nia njema.
Ni vema kabisa na kwa nia njema jambo hili likatizamwa upya, binafsi nimelifikisha rasmi kwa uongozi wa bunge.
Na nimeona pia nishirikiane nanyi watanzania wenzangu kulitafakari.

Julius Sunday Mtatiro,
Mjumbe - Bunge Maalum la Katiba.

SOURCE; PAGE YA MTATIRO YA FACEBOOK!
 
Mmmh! kazi kweli kweliiiii..... ngoja tusubiri kesho tuone.
 
Uamuzi wowote usiofaa utakuwa na madhira makubwa kwa Sitta na kile kinachodaiwa kuusaka kwake Urais.
 
^^
Kanuni nazo zimetoa mamlaka sana kwa Mwenyekiti,, kila jambo zito linaishia busara za Mwenyekiti.. Uhuru huo walioumpa utatumika kugeuka vifungu vingi.
Time will tell
^^
 
Magamba hata wale walio soma wamegeuka viraza wana buruzwa na wasio kwenda vidato akina mangula
 
...i 100% concur with Mtatiro....kwanza nasikitika sana kuskia eti anaanza Jaji Warioba kuwakilisha rasimu...badala ya kuanza na hotuba ya ufunguzi ya JK kama sheria waliyotunga wenyewe juzi inavyowataka.....this itself tells you kwamba wanachozungumza ccm na wanachofanya ni tofauti na wao wanaona hamna shida....maana wamezoea unafiki wa kusema na kupanga wasiyofanya...inasikitisha sana hii...haswa ukizingatia Sitta kaaminiwa na makundi yote kwenye bunge la katiba....

...Wanampa mda mchache Warioba maana hawajiamini...wanadhani akipewa mda mwingi atawa influence watu wabadili misimamo waliyowekeana kwa nguvu kwenye vikao vyao vya chama....huu ni upuuzi mkubwa....Maamuzi ya Sitta kwa kuanzia yanatoa taswira ya yatakayojiri bungeni....wamepanga kuihujumu rasimu ya katiba....yetu macho na masikio...watanzania si majuha....wanaona na wanatafakari......
 
Back
Top Bottom