Kinywa cha mfanyabiashara hakipaswi kutamka maneno haya; bahati, bahati mbaya na bahati nzuri

Economist Jay

Member
Joined
Feb 18, 2016
Posts
42
Reaction score
51
Maneno bahati mbaya na nzuri yamekuwa yakisikika sana katika vinywa vya watu wengi duniani, mtu akifanikiwa kutoka salama katika ajali watu husema kuwa “yaani imekuwa bahati nzuri ametoka salama” na ikitokea labda wakati akitoka ndani ya gari baada ya ajali lakini akaumia mguu utasikia watu wanasema kuwa ‘wakati akitoka ndani ya gari bahati mbaya mguu wake umeteguka.’ Je, kauli hizi zina maana yoyote katika ulimwengu wa biashara?

Kabla sijajibu swali hilo hapo juu, napenda nirejee katika maana ya neno ‘bahati’. Neno bahati maana yake ni tarajio chanya limtokealo mtu katika maisha yake hapa duniani, kinyume na neno hili huitwa mkosi. Waswahili wengi hupenda kulazimisha maneno “bahati mbaya” kuwa neno “mkosi” kitu ambacho siyo sahihi. Hebu tafakari kauli zifuatazo;

John ana bahati, amepata ajali.
John ana bahati mbaya amepata ajali
John ana mkosi, amepata ajali

Ukiangalia sentensi zote hapo utagundua kuwa sentensi ya 1 na ya 2 siyo sahihi kwa sababu huwezi kuwa na bahati alafu ukapata ajali au ukawa na bahati kisha ikawa mbaya. Sentensi ya 3 iko sahihi kwa sababu mkosi huambatana na mabaya, na bahati huambatana na mazuri.

Kutokana na ukweli huo sasa tunaweza kutumia vizuri maneno hayo katika maongezi yetu katika maisha. Pamoja na kwamba kuna neno hili “bahati”, hii haina maana kuwa neno bahati linaweza kutumika kila mahali. Eneo ambalo neno hili halipaswi kutumika ni katika maswala yote yanayohusisha mipango katika kufikia malengo husika.

Sehemu yoyote ambayo kuna neno mipango, neno bahati halina nafasi kabisa, kutokana na kwamba bahati ni kitu cha kusadikika, hutokea lakini hakihusishi utaratibu fulani wa akili katika kupatikana kwake. Neno bahati hutofautiana na neno mkosi katika kutokea kwake, bahati hufariji kwa maana ya kuleta manufaa fulani lakini mkosi huondoa faraja na huleta huzuni.

Je, Maneno bahati, bahati mbaya, na bahati nzuri yana nafasi katika biashara na wafanyabiashara?

Jibu la swali hili liko wazi kabisa maneno hayo yote hayana nafasi katika biashara na kwa mfanyabiashara mwenyewe, kinywa cha mfanyabiashara hakitakiwi kabisa kutamka maneno hayo.

Biashara ni sayansi, inahusisha akili ya mtu kupanga mipango ya biashara ambayo itakufanya uweze kufikia malengo utakayojiwekea. Biashara hufuata njia zote za kisayansi katika kuanzishwa kwake na mavuno yake. Kutokana na maelezo haya unaweza kujiuliza; kwa nini watu huwa wana mipango mizuri kabisa na wanapokwenda kuitekeleza huwa wanaingia hasara?

Jibu la swahi hili pia liko wazi, ukijinasibu kuwa una mipango mizuri ya biashara lakini ulipokwenda kuitekeleza uliingia hasara, maana yake ni kuwa haukuwa na mipango thabiti, hasara huwa ni matokeo ya mipango mibovu ya biashara aliyokuwa nayo mtu.

kabla hujaanza biashara, unapojiandaa ni lazima uangalie na mambo ambayo huenda yakatokea kwa dharura na kusababisha uingie hasara, hivyo ukijiandaa na haya hapo ndipo unaweza kusema mpango wako wa biashara umeuweka vizuri, lolote litakalotokea ili kukukwamisha utakuwa tayari ulishaliwekea tahadhari, na hii ndiyo tunaita mpango madhubuti wa biashara.

Mfano unaweza ukawa umejiandaa kulima pamba, ukaandaa pesa kwa ajili ya kulimia, parizi, uvunaji lakini ukasahau bajeti ya kununua dawa ya kuulia wadudu watakaoshambulia matunda ya pamba shambani. Sasa hapa ukipata hasara usijekuanza kutuhumu kilimo na wadudu, ni lazima ujitafakari na kukubali kuwa hukuwa na mipango mizuri, ingekuwa ni mipango mizuri usingepata hasara.

Wafanyabiashara wengi husingizia kuwa hawana bahati na biashara, lakini ukweli ni kwamba hawana mipango mizuri ya biashara. huwezi kutegemea bahati kitu ambacho hakihusiki katika vitu vinavyohitaji akili ya mtu kuleta mpangilio mzuri wa kumnufaisha.

Biashara yoyote ile haiendeshwi kwa bahati, bali biashara duniani zinaendeshwa kwa mipango makini. Mfanyabiashara anatakiwa kujitahidi sana katika kupangilia vizuri mambo yake yote yanayohusisha biashara fulani.

Harasa ni matokeo ya mipango mibovu, bali faida ni kiashiria kuwa unatumia mipango madhubuti katika biashara.

Mafanikio ni haki yako!
Makala haya na nyengine nzuri utazipata kwenye link hii hapa chini

www.mgejwajr.com

0759708499
 
Asante Kwa bandiko lako.

Lakini nikurekebishe kidogo unaposema kupata hasara katika biashara ni mipango mibovu kiujumla nakukatalia. Hasara Kwenye biashara inachangiwa na vitu vingi Mno. Tatizo Huwa mnaoandika Hizi habari za biashara wengi wenu Huwa sio wafanyabiashara kiuhalisia.
 
"Dada hivyo vitu unavyovisema kwa nini hukuviweka kwenye mpango mwanzo kama vitu vya dharura??

Kwenye bandiko langu kuna maneno yanasomeka hivi

"
kabla hujaanza biashara, unapojiandaa ni lazima uangalie na mambo ambayo huenda yakatokea kwa dharura na kusababisha uingie hasara, hivyo ukijiandaa na haya hapo ndipo unaweza kusema mpango wako wa biashara umeuweka vizuri, lolote litakalotokea ili kukukwamisha utakuwa tayari ulishaliwekea tahadhari, na hii ndiyo tunaita mpango madhubuti wa biashara.
"
 
Thread kama hizi znajenga zipewe kipaumbele
 
Na ndio maana tunaambiwa mfanya biashara au mjasiriamali unatakiwa uzikubali changamoto. Changamoto hazikwepeki Kwenye biashara yoyote Duniani hata hao matajiri wakubwa Duniani wanakumbana nazo. Na wamewaajiri watu wenye talanta tofauti Kwenye shughuli Zao unakuta mwisho wa siku mradi badala ya kuingiza faida Ni hasara tupu.

Mimi naongelea experience sijasomea popote biashara ila ni kitu ninachokifanya Kwa Muda wa miaka zaidi ya 10. Natambua nacho kiandika.
 
Changamoto zipo sana. Na kuna ambazo unaweza predict na kuna zisizo.predictiwa. mara nying watu hupredict zile common kama majanga ya moto, wizi na kadhalika. Ila kuna ambazo sio common na zinapo tokea huwa na impact kubwa sana

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Hapo nakuunga mkono waandishi na wahamasishaji wengi wa mambo ya biashara na ujasiriamali hata biashara hawazijui zinafanyikaje
 
Hapo nakuunga mkono waandishi na wahamasishaji wengi wa mambo ya biashara na ujasiriamali hata biashara hawazijui zinafanyikaje
Biashara tunazifanya, unaona hii ninayofanya tayari ni biashara! Au biashara ni nini Mkuu.
 
Kwa hivyo Mkuu, ikitokea umepata hasara, utasema bahati mbaya mambo hayakwenda sawa? Na je, unaamini kuwa katika biashara kuna kitu kinaitwa bahati?
 
Hapo nakuunga mkono waandishi na wahamasishaji wengi wa mambo ya biashara na ujasiriamali hata biashara hawazijui zinafanyikaje
Ndio kweli kama huyu yeye anauza maneno wakati hajui kila biashara ina changamoto zake
 
Muhubiri : Mlango 9

11 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.
 
John hana bahati, amepata ajali
John ana bahati mbaya amepata ajali
John ana mkosi, amepata ajali
 
Kwanza watu hawajui tu hamnaga bahati mbaya neno BAHATI halinaga ubaya siku zote BAHATI ni nzuri tu.Watafute neno jingine la kuonyesha ubaya.Yaan umepata BAHATI halafu iwe mbaya sidhani
 
Kuna changamoto ambazo zinakuwa ndani ya uwezo lkn zingine sio
Mf. Changamoto waliyoipata wamiliki wa daladala baada ya kuja Mradi wa mabasi mwendo kasi.
 
Labda mi niseme hivi hilo suala la bahati silifahamu vizuri mi binafs naamini kwamba lipo ila sio kwamba ndio ulifanyie ground source hivyo nakubaliana na wewe kua biashara ni ishu ya kisayansi zaidi ingawaje si kila jambo linalotokea sayansi hiyo ya biashara inaweza ku predict na ku prove!
Anyway, nilitaka kugusia kidogo hapo kwenye hasara, kwa uelewa wangu mdogo hasara ni sehemu ya biashara na wakati mwingine hua tunajisahau tunapoifikiria hasara kua ni kitu negative saana kiasi cha kupigwa vita no loss is the part of business! Mfano hai kampuni ya Space X, ya mwanasayansi Elon Musk iliyowekeza katika safari za anga japo amewekeza billions of money kwenye kampuni hiyo lakini kampuni bado inavuna hasara kwanini? kwa stage ya uwekezaji uliopo ni kwamba bado haijaanza kutengeneza faida but in the long run akishaanza kupeleka watu kufanya utalii kwenye sayari ya Mars na kuanza kutengeneza faida mpaka kufidia loss (uwekezaji uliofanyika) it takes time! So wakati mwingine hasara inaweza kupatikana lakini business plan yako lazima ionyeshe ni lini au baada ya muda gani biashara yako itaanza kutengeneza faida! Sijui nineeleweka....
 
Kitu kingne nilichokiona kwa wafanyabiashara wetu ni kua tunafanya biashara kwa mazoea au mi nimezoea kuita tunafanya biashara kitamaduni yaani kizamani tangu alivyokua anafanya babu yako kisha baba na ndo hivyo hivyo na mimi nachofanya kufanya biashara kisayansi, kwa kufanya utafiti, kufanya prediction mambo yakabadilika kila kukicha sikuiz, kuendanana na kasi ya sayansi na teknolojia (hasa digital technology) sasa kwa mtindo huu wa kwetu wa kufanya biashara pasi na kuzingatia mazingira haya yanayotuzunguka ni vigumu kufanya biashara kisayansi!
 
Bahati huwa ipo, na inahusisha mambo ambayo huna uwezo nayo, na yakikutokea yana uwezo wa kukuathiri (positively au negatively), mfano kuuguliwa
 
Mkuu una biashara yoyote ambayo ina mtaji wa milioni moja??
Mfano nafanya biashara ya mafuta ya alizeti kutoka singida kuja Dar, nikapakia lori zina halafu njiani likapata ajali na mafuta yote yakamwagika uniambie mimi nitakuwa sina mkosi, kuwa serious mkuu na kazi za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…