Kinywaji cha ulanzi: Tufumbue Fumbo la maajabu

MAMESHO

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2011
Posts
1,432
Reaction score
1,738
Habari za leo wakuu. Wanyalukolo nimewafikia na wote mkaao nyanda za juu kusini.

Wengi mnafahamu kuhusu kinywaji cha ulanzi. Kinywaji hiki huzalishwa kutoka katika aina ya mmea wa ulanzi ambao pia upo maeneo mengi ya nchi hii na barani Afrika. Nina maswali yafutayo ambayo sina majibu.

1. Ni kwa nini upatikane tu ukanda wa juu wa kusini mwa Tanzania? Inamaana tukiotesha mianzi aina hiyo sehemu tofauti hatuwezi kugema tukapata? Africa nzima hakuna sehemu yenye ulanzi isipokuwa huko.

2. Ulanzi unaanza kuwa juice halafu unabadilika kuwa pombe pasipo kuongezwa kitu chochote. Hii inatokeaje? Maana pombe za kienyeji huwa inaongezwa hamira ili kuchachua. Huu haongezwi kitu nini huwa kinatokea?

3.Ni maeneo mangapi yana uwezo wa kuzalisha ulanzi na unazalishwa kwa kiasi gani kwa mwaka?

4.Je kuna teknolojia ya kukuza uzalishaji wa zao hili ambayo inatumika?

Nitangulize shukrani. Ikiwa kuna msaada wa kupata majibu ya maswali haya nashukuru.

Ikiwa kuna wataamu wa mimea na watafiti nitafurahi kujifunza kutoka kwenu.
 
1. Unapatikana maeneo ya kanda ya juu kusini kwa kuwa kuna baridi na udogo wake uko half tifu tifu, ambapo mianzi inastawi kwa wingi

2. Ulanzi sio Juice, ni pombe halisi ya kienyeji, ila ule utamu wake ambapo ukiwa umetoka kugemwa, ndo unafanya iwe km juice, maana ukinywa hata huo muda unalewa km kawaida, na unapendwa na rika zote toka watoto hadi wazee.

3. Maeneo ni haya, Njombe, Iringa na Ruvuma, kuhusu uzalishaji wake kwa wastani siwezi fahamu, maana haijawahi fanyika utafiti.

4. Kwa kupitia vifaa vya kiwandani sidhani km iko hiyo teknolojia, ila kwa njia ya kuenyeji na asili iko na inafanywa na wahusika wenyewe kwa kiwango wakitakacho.

Ulanzi ni mtamuu sanaaa, had mate yamejaa mdomoni kuutamani
[emoji39][emoji39][emoji39]

Woiiiiih
 
Utafikiri ulifanya thesis ya ulanzi😂 hizo point umeshuka kama upo kwenye presentation
 
1. Unapatikana maeneo ya kanda ya juu kusini kwa kuwa kuna baridi na udogo wake uko half tifu tifu, ambapo mianzi inastawi kwa wingi

2. Ulanzi sio Juice, ni pombe halisi ya kienyeji, ila ule utamu wake ambapo ukiwa umetoka kugemwa, ndo unafanya iwe km juice, maana ukinywa hata huo muda unalewa km kawaida, na unapendwa na rika zote toka watoto hadi wazee.

3. Maeneo ni haya, Njombe, Iringa na Ruvuma, kuhusu uzalishaji wake kwa wastani siwezi fahamu, maana haijawahi fanyika utafiti.

4. Kwa kupitia vifaa vya kiwandani sidhani km iko hiyo teknolojia, ila kwa njia ya kuenyeji na asili iko na inafanywa na wahusika wenyewe kwa kiwango wakitakacho.

Ulanzi ni mtamuu sanaaa, had mate yamejaa mdomoni kuutamani
[emoji39][emoji39][emoji39]

Woiiiiih
Nimekunywa na naupenda sana. Kuna wajasiriamali wamenza kuuweka kwenye chupa lakini wanaweka maji sana hauwi wa kiwango. Ila ule local aisee. Uko poa sana. Kama kuna ambao wanapack OG niambieni nikanunue
 
Uko wapii? Ili nikupelekee chimboo hilo ukapate ulanzi OG.
 
Mkuu nenda iringa au songea utaweza kupata majibu ya maswali yako,
Ulanzi ule mtamu siyo juice,unakunywa unausikilizia utamu lakini unalewesha kama kawaida
Ule konki huwa tunauita mkangafu,
Ulanzi unagemwa kwa mianzi fulani hiv maalum ambayo ikiwa bado michanga(midogo) urefu hata wa meta 1 hivi,unakata kwa juu then unategesha mbeta basi hapo unapata kinywaji chako
 
Habari za leo wakuu. Wanyalukolo nimewafikia na wote mkaao nyanda za juu kusini.

Wengi mnafahamu kuhusu kinywaji cha ulanzi. Kinywaji hiki huzalishwa kutoka katika aina ya mmea wa ulanzi ambao pia upo maeneo mengi ya nchi hii na barani Afrika. Nina maswali yafutayo ambayo sina majibu.

1. Ni kwa nini upatikane tu ukanda wa juu wa kusini mwa Tanzania? Inamaana tukiotesha mianzi aina hiyo sehemu tofauti hatuwezi kugema tukapata? Africa nzima hakuna sehemu yenye ulanzi isipokuwa huko.

2. Ulanzi unaanza kuwa juice halafu unabadilika kuwa pombe pasipo kuongezwa kitu chochote. Hii inatokeaje? Maana pombe za kienyeji huwa inaongezwa hamira ili kuchachua. Huu haongezwi kitu nini huwa kinatokea?

3.Ni maeneo mangapi yana uwezo wa kuzalisha ulanzi na unazalishwa kwa kiasi gani kwa mwaka?

4.Je kuna teknolojia ya kukuza uzalishaji wa zao hili ambayo inatumika?

Nitangulize shukrani. Ikiwa kuna msaada wa kupata majibu ya maswali haya nashukuru.

Ikiwa kuna wataamu wa mimea na watafiti nitafurahi kujifunza kutoka kwenu.
Bamboo wine wanaita wazungu Nadhani ingefaa kutafuta namna ya kuhifadhi na kuiweka kwenye chupa ikapatika mwaka mzima whole country

Nadhani inaweza kua idea nzuri ya uwekezaji
 
Mkuu nenda iringa au songea utaweza kupata majibu ya maswali yako,
Ulanzi ule mtamu siyo juice,unakunywa unausikilizia utamu lakini unalewesha kama kawaida
Ule konki huwa tunauita mkangafu,
Ulanzi unagemwa kwa mianzi fulani hiv maalum ambayo ikiwa bado michanga(midogo) urefu hata wa meta 1 hivi,unakata kwa juu then unategesha mbeta basi hapo unapata kinywaji chako
Mkuu watu hawawahi kuwaza kuukusanya kutoka kwenye hayo maeneo kisha wakauweka sawa ukaingia sokoni ukiwa na lebel ?

Ukiwa kwenye mtindo huu wa vinywaji vikali kama wine zingine ?
 
2.Process ni fermentation,inatokea hata bila kuweka hamira.Hamira(yeast) huweka as catalyst
 
Habari za leo wakuu. Wanyalukolo nimewafikia na wote mkaao nyanda za juu kusini.

Wengi mnafahamu kuhusu kinywaji cha ulanzi. Kinywaji hiki huzalishwa kutoka katika aina ya mmea wa ulanzi ambao pia upo maeneo mengi ya nchi hii na barani Afrika. Nina maswali yafutayo ambayo sina majibu.

1. Ni kwa nini upatikane tu ukanda wa juu wa kusini mwa Tanzania? Inamaana tukiotesha mianzi aina hiyo sehemu tofauti hatuwezi kugema tukapata? Africa nzima hakuna sehemu yenye ulanzi isipokuwa huko.

2. Ulanzi unaanza kuwa juice halafu unabadilika kuwa pombe pasipo kuongezwa kitu chochote. Hii inatokeaje? Maana pombe za kienyeji huwa inaongezwa hamira ili kuchachua. Huu haongezwi kitu nini huwa kinatokea?

3.Ni maeneo mangapi yana uwezo wa kuzalisha ulanzi na unazalishwa kwa kiasi gani kwa mwaka?

4.Je kuna teknolojia ya kukuza uzalishaji wa zao hili ambayo inatumika?

Nitangulize shukrani. Ikiwa kuna msaada wa kupata majibu ya maswali haya nashukuru.

Ikiwa kuna wataamu wa mimea na watafiti nitafurahi kujifunza kutoka kwenu.
Mnyalukolo; Kamwene. Ndaulyi muyetu:
1. Aina hiyo ya mianzi a.k.a vitindi inaweza kusitawi maeneo yote yenye hali ya hewa na mazingira yanayofanana na yale ya nyanda za juu kusini. Kwa mfano Kilimanjaro, Arusha na Lushoto. Changamoto iliyopo ni Watu hawajajaribu kuistawisha tu na pengine ile Teknolojia ya kugema hawaijui.
2.Ni kweli Ulanzi huanza kama juice lakini kuna wale nzi wadogo wenye macho mekundu(Drosophila) kwa kihehe wanaitwa "mbulagasogo" wanapenda sana kufyonza pale palipokatwa na pia panapotundikwa ile mbeta na hata ndani ya mbeta zenyewe. "Mate" ya nzi hawa yanaichachusha (ferment)haraka sana hiyo juice na kuifanya iwe pombe(Alcohol). Kwa wagemaji ulanzi (na hata pombe iitwayo Tembo kutoka kwenye matunda ya nazi) wanajua kwamba hiyo juice sio rahisi uikute bado ni juice asubuhi wanapokwenda kukusanya- nzi watakuwa weshafanya yao. Ladha ya hiyo "juice/pombe" asubuhi inakuwa tamu sana lakini inalewesha na kadri muda utakavyoenda inazidi kuchachuka (alcohol concentration inaongezeka) na kupoteza utamu na inakuwa kali wenyewe wanaita "mkangafu". Lakini pia muda ukizidi mno inageuka na kuwa "vinegar" wenyewe wanaita mdindifu. Kwa hiyo ulanzi kama juice bila ya hao mbulagasogo haitageuka kuwa pombe.
Ila jamani Ulanzi mwe mwe mweee Yinoga bee.
Namba 3 na 4 watachangia wenzangu.
 
Mkuu kwa hiyo wakati wa kugema ulanzi (sap)utatoka ukiwa na kiwango cha pombe(alcohol)moja kwa moja? Aisee? Nilidhani ukikaa muda ndiyo unakuwa na kilevi.
 
Mnyalukolo; Kamwene. Ndaulyi muyetu:
1. Aina hiyo ya mianzi a.k.a vitindi inaweza kusitawi maeneo yote yenye hali ya hewa na mazingira yanayofanana na yale ya nyanda za juu kusini. Kwa mfano Kilimanjaro, Arusha na Lushoto. Changamoto iliyopo ni Watu hawajajaribu kuistawisha tu na pengine ile Teknolojia ya kugema hawaijui.
2.Ni kweli Ulanzi huanza kama juice lakini kuna wale nzi wadogo wenye macho mekundu(Drosophila) kwa kihehe wanaitwa "mbulagasogo" wanapenda sana kufyonza pale palipokatwa na pia panapotundikwa ile mbeta na hata ndani ya mbeta zenyewe. "Mate" ya nzi hawa yanaichachusha (ferment)haraka sana hiyo juice na kuifanya iwe pombe(Alcohol). Kwa wagemaji ulanzi (na hata pombe iitwayo Tembo kutoka kwenye matunda ya nazi) wanajua kwamba hiyo juice sio rahisi uikute bado ni juice asubuhi wanapokwenda kukusanya- nzi watakuwa weshafanya yao. Ladha ya hiyo "juice/pombe" asubuhi inakuwa tamu sana lakini inalewesha na kadri muda utakavyoenda inazidi kuchachuka (alcohol concentration inaongezeka) na kupoteza utamu na inakuwa kali wenyewe wanaita "mkangafu". Lakini pia muda ukizidi mno inageuka na kuwa "vinegar" wenyewe wanaita mdindifu. Kwa hiyo ulanzi kama juice bila ya hao mbulagasogo haitageuka kuwa pombe.
Ila jamani Ulanzi mwe mwe mweee Yinoga bee.
Namba 3 na 4 watachangia wenzangu.
Mkuu nakushukuru sana. Sikuwahi kudhani kuwa wale wadudu kumbe wana kazi yao pale.
 
Ulansi bee
 
Back
Top Bottom