Shaadya Salum
Member
- Jan 24, 2024
- 13
- 6
Wewe ni kiongozi. Unaona watu unaowaongoza wanalalamikia uvunjifu wa katiba, kanuni, miongozo, na taratibu ambazo wewe kiongozi kwa viapo vyako na ahadi yako kwa CCM uliahidi kuvilinda, kuvitetea, na kuvihifadhi.
Mheshimiwa Rais anasisitiza haki, lakini wewe husikii; umeweka pamba masikioni. Viongozi wa dini wanahubiri haki, lakini wewe husikii. Viongozi wa kitaifa wanahubiri haki, lakini wewe husikii. Umekuwa nunda.
Ujue wewe, hata ukitamka neno Mwenyezi Mungu, unajitamkisha tu kutuzuga. Wewe ni tapeli. Upo unasubiri kumaliza tu maisha ya kidunia ili uende zako kuishi motoni. Ndiyo maana hujali vilio vya mafukara. Ndiyo maana ukiona mtu anaandika ukweli, roho yako chafu inakereka.
Bado muda unao, Badilika, Acha kujisahaulisha kwa utamu wa fedha za kuwadhulumu mafukara wanazostahili. Kumbuka daima kuwa moto wa jahanam kuni zake ni watu na mawe. Na inavyoonekana, usipobadilika na kuacha kufuru, utakuwa mmoja wa kuni za jahanam.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Pia soma: