Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Mwaka huu ni mwaka muhimu sana kwetu kama taifa. Ni mwaka ambao taifa letu linaenda kwenye uchaguzi kuchagua viongozi wapya katika taifa letu. Kwahiyo nimeona nisikae bila kuandika kitu chochote. Niongee machache ambayo nadhani yataleta mwanga.
Uchaguzi huu ni muhimu sana kwetu hata kama viongozi ambao tunakwenda kuwachagua oktoba wanajitambua au hawajitambui. Mwelekeo wa taifa letu unategemea sana maamuzi yetu. Kama taifa tunachangamoto nyingi sana ambazo zinahitaji akili za pamoja kuzitatua. Tunahitaji kiongozi ambae ataleta watu wetu pamoja kutatua changamoto hizo. Matatizo hayo yako mengi ya kiuchumi, kijamii na matatizo ya kisiasa.
Na ili nchi yetu iwe imara matatizo haya ya kiuchumi, kijamii na kisiasa lazima yatatuliwe tunahitaji kiongozi imara kuimarisha haya mambo. Tunahitajika kuwa organized zaidi kutatua changamoto zinazotukabili kwa pamoja. Kwakuwa bila kuwa wamoja hili taifa haliwezi kwenda mbele.
Tunahitaji kiongozi ambaye ataamsha hisia za watu kuhusu utaifa na kuhamasisha watu kufanya kazi kwa manufaa ya taifa lakini pia kwa watu binafsi na kwa familia zao. Taifa hili haliwezi kujengwa na viongozi peke yao huku raia wakikaa pembeni kusubiri wawaletee maendeleo. Maendeleo yataletwa na watu. Na kila mtu lazima ashiriki kuleta maendeleo ya nchi yake. Ili tuendelee lazima tulipende taifa letu na tuwe tayari kulitumikia.
Mojawapo ya matatizo ya kijamii ni kuporomoka kwa maadili na kuondoka kwa cohesion katika jamii. Jamii yeyote ili iendelee lazima iungane kwa pamoja ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili. Kwahiyo tunaona hili tatizo kwa ukaribu sana. Tumekuwa taifa la watu wabinafsi na sio watu wenye malengo ya pamoja ya kunyanyua taifa hili na Kumeongezeka rushwa na ufisadi. Hizi ni changamoto ambazo zinahitaji kiongozi hodari na makini kuzitatua. Taifa linapokuwa moja linakuwa na nguvu na hakuna mtu anayeweza kuzuia nguvu hiyo watu kwa pamoja wanapoamua kubadili maisha yao. Watu wetu wamekosa malengo kwa taifa lao pia. Mifumo ya kijamii imeparaganyika watu hawafanyi kazi pamoja kutatua changamoto zinazowakabili. Familia haziko imara, watoto maadili yamepungua. Kwahiyo tunahitaji kiongozi atakayeleta order katika jamii na katika taifa na kujenga mfumo bora wa kijamii utakaowezesha watu kushiriki vyema katika ujenzi wa taifa lao. Kama sisi ni watu huru na sio watawaliwa wa kikundi fulani cha watu ni lazima tufikiri mambo haya na hii ndio demokrasia. Ni lazima tulipende taifa letu na tuwe tayari kushiriki moja kwa moja kulijenga. Ni lazima tujenge jamii ambayo iko huru dhidi ya rushwa na watu ambao wako tayari kutumikiana na sio kutumikiwa. Matatizo ya kijamii lazima yamhusu na kumgusa kila mmoja wetu na kuwa tayari kukabiliana na changamoto hizo. Ni lazima tujenge watu wetu kujitambua kuhusu utaifa na nafasi yao na wajibu wao kama raia was taifa hili. Kwasababu wasipojua wajibu wao itakuwa ni tatizo.
Ni lazima tujenge taasisi ambazo zinatumikia watu na sio kutumikiwa. Shule zetu lazima ziimarishwe ili watu wetu wapate elimu bora itakayowafanya wajitambue. Wajue wajibu wao kwa taifa na kwa jamii. Na watumie elimu yao kuleta mabadiliko chanya. Ni lazima tujenge kujitambua na uzalendo kwa taifa letu. Muhimu zaidi ni kujenga taifa la watu wanaofikiri badala ya kufungua tu mdomo hata kwa jambo wasilolijua. Kwahiyo misingi imara ya taifa letu itajengwa kwa kwas watu. Ni muhimu watu wetu kupata elimu bora na kutengeneza raia wawajibikaji kwa taifa lakini pia kwa familia zao. Kwasababu bila watoto wetu kulelewa vizuri hatutaweza kupata viongozi bora wala raia bora. Tunahitaji uwajibikaji katika taifa letu kwa ngazi zote sio tu katika uongozi wa juu ni lazima tujue matatizo yetu ili tupate tiba yake.
Uchumi wetu unakua ingawaje idadi ya watu wengi hasa vijana hawana ajira. Umaskini unaongeka. uchumi wa nchi uko mikononi mwa watu wachache. kwahiyo kuna haja ya kusambaza uchumi huu na kupunguza hali ya umaskini ya watu wetu. serikali yetu au kiongozi anayekuja ni muhimu kupunguza matumizi ya serikali na kuangalia miktaba ya madini na maliasili nyingine upya ili watanzania wanufaike nayo. Wapunguze misamaha ya kodi na kutafuta vyanzo vipya vya kodi. Lakini pia wawekeze kwa kiwango kikubwa katika elimu ya watu wetu ili waweze kukabiliana na changamoto za dunia ya sasa. Lakini pia ni lazima tuhamasishe watu wetu kufanya kazi kwasababu uchumi wetu hauwezi kukua pasipo watu wetu kufanya kazi. Tunaweza kuwekeza katika kilimo na kuhamasisha watu wengi zaidi kushiriki katika kilimo na kuwawezesha kuzalisha na kupata masoko. Lakini muhimu zaidi ni utayari wa vijana kutaka kubadilisha maisha yao na kuishi maisha ya uwajibikaji. pasipo kuzalisha nchi yetu haiwezi kuendelea. Tupambane na rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali serikalini.
Katika mambo yanayonipa kichefuchefu ni siasa zetu ndizo zilizotufikisha hapa kama taifa. Tunahitaji kubadili siasa hizi. Aina za siasa tulizonazo sasa hazito tupeleka mbali kama taifa.Tunahitaji kujenga siasa za watu ambao watakuwa much responsible kwa wanayoongea na kutenda. Maendeleo ya jamii yetu na taifa letu yanategemea sana siasa zetu. Wanasiasa ndio huzalisha viongozi na viongozi bora huzalishwa na siasa bora. Siasa za watu ambao wanajadili mambo kwa hoja na kusoma matatizo ya jamii kisha kutafuta tiba mbadala. Tunahitaji siasa zenye akili zitakazowafanya watu wetu kufikiri na kuwa wenye akili zaidi na sio siasa za ulaghai. Wanasiasa wanatakiwa wawe much sensible. Kwahiyo ni common sense kwamba siasa zetu zinahitaji mabadiliko ili zilete transformation kwenye jamii yetu. Na kuwaleta watu wetu pamoja zaidi badala ya kuwagawa. Kama tunashindwa kuenda mbele kama taifa ni sababu ya ujinga wetu. Kuna nafasi kubwa sana kwetu kuendelea zaidi ya tulipo sasa kama tutasikilizana na kuwa na sauti moja kama watanzania bila kuangalia itikadi zetu za kisiasa. Tunaweza kujenga taifa ambalo linaheshimiwa na mataifa mengine. Taifa ambalo limesimama na kujitegemea.