ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Kumekucha, Chadema wamegusa pabaya.
========
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Unguja Ali Ebrahim, akizungumzia Sakata la Ukodishwaji wa Bandari za Tanzania amezungumzia umuhimu wa kutokuwahukumu Wazanzibari kwa kuzingatia vitendo vya watu wachache na si haki kusema "Wazanzibari wameuza bandari"
Akizungumza na Jambo TV, Katibu huyo amesisitiza umuhimu wa kuangalia uongozi wa sasa kwa mtazamo mpana, akibainisha kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na utawala wake hautakiwi kuunganishwa tu na Uzanzibar bali anawakilisha Watanzania wote.
Aidha, aliashauri kuwa watu wanapotoa maoni , ni muhimu kuzingatia athari zinazoweza kutokea kwa pande zote. "Wazanzibari wanaweza kuwa kimya kwenye masuala mbalimbali, lakini masuala ya muungano na utambulisho wa Zanzibar, hawawezi kukaa kimya" amesisitiza Ebrahim. Hata hivyo, Ali Ebrahim ametambua kuwa hii ni changamoto kwa vyama vya siasa katika kufikisha ujumbe wao kwa ufanisi na kuhakikisha kuwa watu wanaelewa.
Ali Ebrahim alihitimisha kwa kusema “Yote kwa yote tumekuwa watanzania kwa sababu ya muungano,Sioni haja ya kunyoosheana vidole”.