Kiongozi wa genge la majambazi awatishia Polisi Nairobi kwa clip ya video

Kiongozi wa genge la majambazi awatishia Polisi Nairobi kwa clip ya video

Secret Star

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2011
Posts
1,734
Reaction score
1,709
Kanda ya video ya kiongozi wa genge moja la majambazi kwa jina Gaza akijigamba kuhusu uhalifu aliotekeleza imesambaa katika mitandao ya kijamii na kuwawacha wengi vinywa wazi

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya kiongozi huyu wa genge ambaye polisi wanamtambua kwa jina Seba alias Johnnie alionekana katika kanda hiyo ya video akijigamba kwamba bado yeye ndiye mfalme wa uhalifu nchini Kenya na kwamba hakuna kile ambacho polisi wataweza kufanya.

Katika video hiyo Seba ambaye alikuwa akitekeleza operesheni zake kutoka eneo la Mlango Kubwa jijini Nairobi anasikika akiwatishia maafisa wa polisi kwamba atawashambulia na visu.

Kiongozi huyo wa gengi ambaye kwa sasa anadaiwa kutekeleza uhalifu wake kutoka kaunti ya Tana River anaendelea kujigamba kwamba kufikia sasa ameweza kuiba simu 86 kutoka kwa raia na kwamba maafisa wa polisi walifanya makosa kwa kudai kwamba ameiba simu 46 pekee.

Kulingana na gazeti hilo Jamaa huyo anayejiita Mfalme wa Gaza anaendelea kuelezea kwamba hatosita kutekeleza uhalifu hivi karibuni na kwamba polisi wanaweza kumtafuta.

Seba ambaye alikuwa ameandamana na wenzake wanne katika video hiyo amewaonya raia wanaopeleka ujumbe kwa polisi kwamba atawashambulia kwa visu iwapo wataendelea kufanya hivyo.

Wakenya katika mitandao ya kijamii wamewataka polisi kumtafuta Seba na kundi lake wakidai kwamba wameyafanya maisha ya wakaazi wa Nairobi kuwa magumu.

''Maafisa wa polisi wanatakiwa kuchukua hatua za haraka kabla ya kutekeleza vitisho vyao'', Robert Jakoriw aliandika katika mtandao wa facebook.

''Je DCI kinoti yuko wapi, hawa vijana wanafaa kuchukuliwa hatu'' , alisema Frank Rapemo mtumiaji mwengi wa mtandao wa Facebook.

Eneo la Kayole jijini Nairobi limesemekana kuwa nyumbani kwa wanachama wa Genge hilo la Gaza , ambalo ni mojawapo ya megenge yanayoogopwa sana eneo la Eastaland.

Wakaazi wengi katika eneo hili wanaishi chini ya dola moja kwa siku , hatua inayowashinikiza vijana wengi kujiingiza katika uhalifu.

Kulingana na gazeti la The Standard nchini Kenya genge hilo la Gaza linaaminika kutekeleza idadi kadhaa ya mauaji na uhalifu katika eneo hilo lakini operesheni zake hazijulikani.

Wanachama wake hutumia visu na bunduki kama vifaa vya biashara yao.

Video..

Genge hilo pia linadaiwa kuanzisha genge jingine la Yakuza ambalo uhusika na uhalifu wa hali ya juu kama vile wizi wa benki na ule wa barabara kuu.

Mapema mwaka huu, maafisa wa polisi walikiri kwamba kundi hilo limekuwa likiwatishia wakaazi lakini wamesema kuwa wanatumia kila njia kuimarisha usalama wa wakaazi wa eneo hilo.
 
Attachments

  • _107391640_screengrab.jpg
    _107391640_screengrab.jpg
    11.4 KB · Views: 34
Duh itakuwa haya magenge yanalelewa na polisi wenyewe kifupi yanadhaminiwa na idara ya polisi
 
Ukijitia kimbelembele utaambulia Bisu la Mat**o .. hahahaa kweli Yesu Yupo Chalinze, kakaribia kufika
 
Serikali Dhaifu ya Kenya, kila mtu anaweza kuitishia anavyotaka.
Kuna wengine 14 wamekufa jana kule mpaka na Somalia. yaani kila mtu anafanya analoona lina faa.
Mbona umechelewa kufungua Uzi wa Al shabab kejeli zianze? Hapa naona umefurahi sana kukuondolea aibu ya $14b budget na misaada 49%
 
Serikali Dhaifu ya Kenya, kila mtu anaweza kuitishia anavyotaka.
Kuna wengine 14 wamekufa jana kule mpaka na Somalia. yaani kila mtu anafanya analoona lina faa.
Unamaanisha hata kuteleza huwa tunawatelezesha tunavyotaka au? Alafu mambo ya kishirikina pia huwa tunayafanya tunavotaka, tukitaka kuua vijitoto vichanga tunaua, albino tukitaka kiungo chake tunakinyofoa! Nimekuelewa sana.
 
Mbona hao wamechoka sana? Yaani hao ndio Genge la majambazi? Polisi Kenya wajipange sawasawa kama hao ndio wanaowatisha basi ndio maana westgate waliendeshwa na vijana wanne tu kwa siku karibia tatu.

Sijaona Majambazi zaidi ya wavuta bangi tu wa vijiweni walioamua kurusha clip yao mtandaoni baada ya kuvuta BANGI.
 
Mbona umechelewa kufungua Uzi wa Al shabab kejeli zianze? Hapa naona umefurahi sana kukuondolea aibu ya $14b budget na misaada 49%

Siwezi fungua uzi kwa uuaji wa huko Kenya. Ilibidi ufungue wewe mkenya ili tutoe condolence. Or you are no longer shocked with alshabab related carnage??
 
Unamaanisha hata kuteleza huwa tunawatelezesha tunavyotaka au? Alafu mambo ya kishirikina pia huwa tunayafanya tunavotaka, tukitaka kuua vijitoto vichanga tunaua, albino tukitaka kiungo chake tunakinyofoa! Nimekuelewa sana.

The Government of Kenya is very weak bro. How could a person throw such serious word to the authority and nothing happens. do you know the effects of that public annoucement??
 
Siwezi fungua uzi kwa uuaji wa huko Kenya. Ilibidi ufungue wewe mkenya ili tutoe condolence. Or you are no longer shocked with alshabab related carnage??
Hata Sasa hujatoa condolences hata ingawa ulijua kitambo... ulikuwa anachekea chini chini Kama kawaida. Mazishi ya mwanisiasa wa Chadema(RIP) aliyepigwa risasi ni lini?
 
The Government of Kenya is very weak bro. How could a person throw such serious word to the authority and nothing happens. do you know the effects of that public annoucement??
Tumia akili bro, the police cannot prevent you from making a a video with your phone and posting it on the internet.
 
The Government of Kenya is very weak bro. How could a person throw such serious word to the authority and nothing happens. do you know the effects of that public annoucement??
Sikujua kwamba video kwenye facebook ni public announcement. Kuna ule uzi wa Dula aliyeuliwa Mombasa. Humo ndani mnasema ni uhuni kuwaua hawa vibaka. Hamjielewi nyinyi viumbe. Huyu naye atalishwa ndengu hivi karibuni na uzi utakapofunguliwa humu utaibuka na porojo zingine.
 
Ni hatari kweli
Sikujua kwamba video kwenye facebook ni public announcement. Kuna ule uzi wa Dula aliyeuliwa Mombasa. Humo ndani mnasema ni uhuni kuwaua hawa vibaka. Hamjielewi nyinyi viumbe. Huyu naye atalishwa ndengu hivi karibuni na uzi utakapofunguliwa humu utaibuka na porojo zingine.
 
Hata Sasa hujatoa condolences hata ingawa ulijua kitambo... ulikuwa anachekea chini chini Kama kawaida. Mazishi ya mwanisiasa wa Chadema(RIP) aliyepigwa risasi ni lini?

Hiyo si desturi yetu ya kuchekelea mtu akifa. Ndiyo maana hutasikia Tanzania tunauana kwa misingi ya tofauti zetu. Sisi sote ni ndugu.
 
Tumia akili bro, the police cannot prevent you from making a a video with your phone and posting it on the internet.

You are right, the police can not prevent you not only from making a video, but also to rob, still, to kill etc etc, you can do all that. but the issue is to be free after these bad deed. That is the issue. Mkijiongeza ndiyo mtaweza kuwakamata.
 
Sikujua kwamba video kwenye facebook ni public announcement. Kuna ule uzi wa Dula aliyeuliwa Mombasa. Humo ndani mnasema ni uhuni kuwaua hawa vibaka. Hamjielewi nyinyi viumbe. Huyu naye atalishwa ndengu hivi karibuni na uzi utakapofunguliwa humu utaibuka na porojo zingine.

ahaa ha ha
hukujua kwamba ni bango la matangazo.
Trump issue za serikali anazipeleka kwenye mitandao ya jamii. Huko ili kila mmwanainchi azione.
 
ahaa ha ha
hukujua kwamba ni bango la matangazo.
Trump issue za serikali anazipeleka kwenye mitandao ya jamii. Huko ili kila mmwanainchi azione.
Jiwe huwa anafanyia wapi public announcement zake? Instagram au?
 
Back
Top Bottom